Total Pageviews

Tuesday, June 6, 2017

MMEA WA MMOYOMOYO KATIKA TIBA NA KINGA DHIDI YA MARADHI YA MOYOMamilioni  ya  watu  duniani  wanasumbuliwa  na  maradhi  mbalimbali  ya  moyo.
 Inapotajwa  maradhi  ya  moyo  maana  yake  ni  uwepo  wa  hitilafu  mbalimbali  ndani ya  moyo  au  zinazo  husiana  na  moyo  ambazo  husababisha  moyo  kutokufanya  kazi  sawa  sawa. 

 Kupanuka  kwa  moyo  , mapigo  ya  moyo  kwenda  kasi  na  shinikizo  kuu la  damu    ni  miongoni  mwa  maradhi  yanayo  tajwa  na  wataalamu  wa  afya  kama  maradhi  ya  moyo.

Katika   tiba  asilia,  mmea  wa   Mmoyomoyo  unatajwa  kuwa  na  uwezo mkubwa  wa  kudhibiti  na  kupambana  na  maradhi  mbalimbali  yanayo husiana  na   moyo .  
Watu   wanao  tumia  mmea  wa   Mmoyomoyo  katika  kupambana  na  maradhi  mbalimbali  ya  moyo  hupata nafuu  kubwa.

Mbali  na  kusaidia  katika  kutibu  maradhi  mbalimbali  ya  moyo, mmea  wa  Mmoyomoyo  unatumika  zaidi  katika  kinga  dhidi  ya  maradhi  mbalimbali  ya  moyo.

Matumizi  mabaya  ya  chakula, hasa  hasa  utumiaji  wa vyakula  vya  mafuta , vyakula  vyenye sukari, ulevi kupita  kiasi  pamoja  na  kutokufanya  mazoezi  ya  mwili  ( Physical  Exercises ) ni miongoni  mwa  mambo  yanayo  weza  kumuweka  mtu  katika  hatari kuu  ya  kupatwa  na  magonjwa  ya moyo.


Matumizi  ya  mara  kwa  mara  ya  mmea  wa   Mmoyomoyo  yanaweza   kupunguza  hatari  ya  kupatwa  na  maradhi  ya  moyo.
Mmea  huu  pia  unatumika  katika     kuondoa  na   kudhibiti  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini.

Makala  haya  yamekuja  kwenu  kwa  hisani  ya  NEEMA  HERBALIST. Duka  la  kuuza  dawa  mbalimbali  za  asili. Tunapatikana  jijini  DAR  ES SALAAM, katika  eneo  la UBUNGO  jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONA  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.  
Tunapatikana  kwa  simu  namba  0766  53  83 84
Na  kwa  makala  kuhusu  tiba  asilia  ya  magonjwa  mbalimbali, tembelea   blogu yetu kila  siku :
Sunday, April 23, 2017

MTI WA MCHOCHO NA TIBA YA WATOTO KUKOJOA KITANDANI

MTI  WA  MCHOCHO  NA  TIBA  YA WATOTO KUKOJOA  KITANDANI


Kukojoa  bila  kukusudia  ama  kujikojolea  ni  tatizo  linalo  wakabili  watu wengi duniani .
Kukojoa  bila  kukusudia  ama  kujikojolea  ni  ile  hali  ya   mtoto  mwenye  umri  wa  miaka  mitano  au zaidi  kushindwa  kuzuia  mkojo  wakati  wa  mchana  au  usiku  na  hivyo  kujikojolea  kitandani wakati  wa  usiku  au kujikojolea   kwenye  nguo  wakati  wa  mchana.
Tafiti  mbalimbali  za  kitaalamu  zinaeleza  kuwa  watoto wengi wanaacha kukojoa kitandani wakati  wa usiku katika umri wa miaka mitatu.   

Kuchelewa kukomaa kwa uwezo wa kibofu kuzuia mkojo kunaelezwa  kuwa  ndio  chanzo  kikuu  cha  tatizo  la  kujikojolea  kitandani kwa  watoto  wadogo.
Katika  tiba  asilia, ipo  mimea  mbalimbali  inayo  tajwa  kuwa  na  uwezo  wa  kutibu  tatizo  la  mtoto  kukojoa  kitandani. 
Kati    ya  mimea  hiyo, upo  mti  wa  mchocho. Mmea  huu  umekuwa  ukitumiwa  na  wenyeji  wa  mkoa  wa Pwani  nchini  Tanzania  katika  kuwatibu  watoto  wenye tatizo  la  kukojoa  kitandani  au  kujikojolea.
Jinsi  unavyo  tumika, mizizi, magamba  na  majani ya  mmea  huu  wenye  ukubwa  kama  mti  wa  muembe  huchukuliwa  hukaushwa  na  kusagwa  kupata  unga  unga  wake,. Unga  wa  mti  huu  huchemshwa  kwenye  maji  kisha  kimiminika  chake  hupewa  kunywa  mtoto  mwenye  tatizo  la  kukojoa  kitandani  kwa muda  wa  siku  ishirini  na  moja. Mtoto  huanza  kuonyesha  nafuu kuanzia  siku  ya  saba  na  inapofika  siku  ya  ishirini  na  moja, mtoto huyu  anakuwa  amepona  kabisa  tatizo  la  kukojoa  bila  kukusudia  ama  kujikojolea  kwa  lugha  nyingine.

MAKALA  HAYA  YAMEANDALIWA  NA  DUKA  LA  NEEMA  HERBALIST. TUNAPATIKANA  UBUNGO  JIJINI  DAR  ES  SALAAM, NYUMA  YA  JENGO  LA  UBUNGO  PLAZA  JIRANI NA  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING.
TUNAPATIKANA  KWA  SIMU  NAMBA  0766 53 83 84.  KUFAHAMU  ZAIDI  KUHUSU  TIBA ASILIA  YA  MAGONJWA  MBALIMBALI. TUTEMBELEE  KUPITIA  BLOGU  YETU:

Tuesday, April 18, 2017

Diandra Forrest, mwanamitindo anaetumia fani ya mitindo kuielimisha jamii yake kuhusu changamoto wanazo kutana nazo albino.

Diandra Forrest
Diandra  Forest
Anafahamika  kwa  jina  la  Diandra  Forest. Mwanamitindo  kutoka  nchini  Marekani  ambae  ameonyesha  uwezo  wa  hali  ya  juu  katika  tasnia  ya  mitindo  nchini  Marekani  na  duniani  kwa  ujumla.  Fahamu  zaidi  kuhusu  maisha  ya  mwanamitindo  huyu  kupitia  maelezo  hapo  chini.  PICHA  NA  MAELEZO  KWA  HISANI  YA  MTANDAO  WA BORAPANDA.COM

============================================

Model and Actress

Diandra Forrest is an African-American model and actress. She is the first female model with albinism to be signed to a major modelling agency. Her striking beauty has caught the attention of many magazines and she has walked in numerous international fashion shows. Her passion for art and creativity has also drawn her into the world of acting.
Diandra Forrest

Early Years

I realised I had albinism at the age of nine. I grew up in a family of five children, in which only my younger brother and I had the condition. As a child, I often felt out of place.
I had neighbourhood friends who asked my older brother if I was adopted. In school, or even on the train with my mum, there would be parents, adults, who stared at my brother and me and laughed at us. I didn’t understand why.

New Found Confidence

It is not easy being a person with albinism because of the lack of understanding of what the condition is, even in the modelling industry where I have been working for the past few years.
People with albinism are looked at as something that is maybe extra-terrestrial, an odd beauty, not just a regular beauty, whatever that is. It can be fun and entertaining but it should not be a freak show.
Over the years, I have found my confidence, as a person with albinism, as just a woman, so that sort of thing does not bother me anymore.
Diandra Forrest
Diandra Forrest

Role Models

But I still hope for change: for children with albinism to know their beauty, and for their parents to instil that confidence in them.
I have always wanted to undertake a kind of ‘Big brother’, ‘Big Sister’ programme to mentor younger children with albinism, and to help their parents understand the condition and how it affects their children physically and emotionally.
Growing up, I would have loved to have someone older around who had albinism so I could see what I was going to look like when I grew up, just to motivate me, and who could understand some of the things I was going through.

Monday, April 17, 2017

MKATABAWAZIRI; DAWA ASILIA INAYO TIBU MARADHI YA BAWAZIRI KWA NAMNA YA KIPEKEE

Mkomavikali; Huu ni  miongoni  mwa  mimea  michache  inayo  weza  kutumika  kama  tiba  dhidi  ya  maradhi  ya  bawaziri,


Kutokwa  na  kinyama  ama  uvimbe  kwenye sehemu  ya  haja  kubwa  ni  tatizo  linalo  wakabili mamilioni  ya watu  duniani.

Tatizo  hujulikana  kwa  Kiswahili  kama  Bwaziri,  katika  lugha  za kisukuma  na  kinyamwezi  huitwa  “Man’gondi” na  katika  lugha  ya  kiingereza  hujulikana  kama  Hemorrhoids.
Ufwambo. Moja  kati  ya  dawa  zinazo  tumika  katika  tiba  dhidi ya  maradhi ya  bawaziri. Majani  ya  luwambo  yanaweza  kutumika  kutengeneza  sukari  ya  asili, kwa  sababu  ni  matamu  kama  sukari.


AINA  ZA  BAWAZIRI : Kwa mujibu  wa  tafiti mbalimbali  za  kitaalamu, zipo  bawaziri  za  aina  mbili, bawaziri  ya  ndani  na  bawaziri  ya  nje. Kwa  kawaida  mtu  huweza  kuwa  na  moja  wapo kati  ya  aina  hizo   na  wakati  mwingine, mtu  mmoja  anaweza  kuwa  na  bawaziri  za  aina  zote  mbili  kwa  wakati  mmoja.
Ufwambo  ukiwa  umestawi  porini


NINI  HUSABABISHA  BAWAZIRI ? 

Mchicha pori

Mchicha  pori  au  Mnunganunga. Mizizi  ya  mmea  hutumika  kama  sehemu  ya  tiba  ya  maradhi  ya  bawaziri.

Mpaka   sasa  wataalamu  bado  hawaja  baini  chanzo  halisi  cha  tatizo  la  bawaziri. Hata  hivyo  tafiti  mbalimbali za  kitaalamu  zinabainisha  mambo  kadhaa  yanayo  changia  kutokea  kwa  tatizo  la  bawaziri.
Mambo  hayo  ni  pamoja  na :

i.                   Kukosa  choo  kwa  muda  mrefu
ii.                Kuharisha  kwa  muda  mrefu
iii.             Kukaa  kwenye  choo  kwa  muda  mrefu
iv.             Kukaa  kwa  muda  mrefu
v.                Unene  na  uzito  kupita  kiasi: Tafiti  mbalimbali  zina onyesha  kuwa, asilimia  kubwa  ya  watu wenye  tatizo  la  unene  na  uzito  ulio zidi, huwa  katika  hatari  kubwa  ya  kupatwa  na  tatizo  la  bawaziri.

vi.             Ujauzito :  Tafiti  mbalimbali  za  kitaalamu  zinaonyesha  kuwa, asilimia  kubwa  ya  wanawake  wajawazito  huwa  katika  hatari  ya  kupatwa  na  tatizo  la  bawaziri, sababu  ikiwa  ni  kuongezeka  kwa  shinikizo  ndani  ya  mfuko  wa  uzazi.

vii.          Kutofanya  mazoezi  kwa  muda  mrefu

viii.       Kutotumia  vyakula  vyenye  nyuzi nyuzi

ix.             Sababu za  kinasaba : Tafiti  zinaonyesha  kuwa, wapo  watu wanao  patwa  na  bawaziri, kwa  sababu  za  kijenetiki

NINI  DALILI  ZA  BAWAZIRI ?

Dalili  kuu  za  bawaziri  ni  pamoja  na  kutokwa  na  kinyama  ama  uvimbe  kwenye  sehemu  ya  haja  kubwa, kukosa  choo, kupatwa  maumivu makali  sana  wakati  wa  kujisaidia  au wakati  unatembea  na  wakati  mwingine  maumivu  huendelea  hata  ukiwa haupo katika  matendo  yaliyo tajwa   hapo  juu. Dalili  nyingine  ni  pamoja na  kuhara  damu  ama  kutoa  kinyesi  chenye  damu.

JINSI  YA  KUJIKINGA  USIPATWE  NA  BAWAZIRI :

Kujikinga  usipatwe  na  bawaziri, unashauriwa
i.                   Kujenga  tabia  ya  kuwa  unakula  vyakula vyenye  nyuzi nyuzi ( fibre) kwa wingi
ii.                kula  matunda  kwa wingi
iii.             Kunywa  maji mengi
iv.             Fanya  mazoezi  ya  mwili  mara  kwa  mara
v.                Usikae   maliwatoni kwa  muda  mrefu
vi.             Usiruhusu  unene  na  uzito  kubwa.

TIBA  ASILIA  YA  TATIZO  LA  BAWAZIRI :
Zipo  dawa   mbalimbali  za  asilia  ambazo  zina  tibu  na  kuponyesha  kabisa  maradhi  ya  bawaziri.  Baadhi  ya dawa  hizo  ni  pamoja  na Lufwambo  ama Ufwambo,  Mkomavikali, Nun’ganun’ga  au  Mchicha  Pori,  Zumanguku, Luwawa  na  Mkatabawaziri.

Kati  ya  dawa  zilizo  orodheshwa  hapo  juu, dawa  ya  Mkatabwaziri inakubalika  zaidi  kwa  sababu  kuu  mbili, kwanza  ni  ufanisi  wake  katika kutibu  maradhi  ya  bawaziri  na  pili  ni  namna inavyo  tumika  katika  tiba  ya  bawaziri.

Wakati  dawa  nyingine  za  kutibu  maradhi  ya  bawaziri, zinatumika  kwa  mgonjwa  kunywa  au  kupaka.  Mkatabawaziri  yenyewe  inatumika  kwa  namna  ya  kipekee  sana.

JINSI  MKATABAWAZIRI  INAVYO  TUMIKA  KATIKA  TIBA  YA  MARADHI  YA  BAWAZIRI.
Mgonjwa  anatumia  kunywa  halafu  anatumia  kujifukiza  mvuke  wa dawa  ya  mkatabawaziri.  Katika  kujifukiza, dawa  hii  huchemshwa  kisha  huwekwa  kwenye  ndoo halafu  mgonjwa  anakalia  juu  ya  ndoo  ili  mvuke  wa  dawa  hii  uweze  kufika  kwenye  sehemu  iliyo  athirika  ( sehemu  yenye  bawaziri ).

Zoezi  hili  hufanyika  mara  mbili  kwa  siku  kwa  muda  wa  siku  ishirini  na  moja   mfululizo.

Ufanisi  wa  tiba  hii  ni  mkubwa  sana. Mgonjwa  huanza  kuona  mabadiliko  ndani  ya  siku  saba  na  baada  ya  siku  ishirini  na  moja  tatizo  la  bawaziri  linakuwa  limekwisha  kabisa  na  mgonjwa  anakuwa  amepona  kabisa  tatizo  la  bawaziri.

Tiba  hii  imemsaidia  na  kumponyesha  kila  alie  itumia. Kama  umesumbuliwa  na  maradhi  ya  bawaziri  kwa  muda  mrefu  na  umehanganika  kutafuta  tiba  bila  mafanikio, basi  jaribu  kutumia  tiba  ya  Mkatabawaziri, ili uweze  kuondokana  na mateso  ya  tatizo  la  bawaziri.

JINSI  DAWA  ASILIA  YA  MKATABAWAZIRI  INAVYO PATIKANA.

Kupata  dawa  ya  Mkatabawaziri, fika  katika  duka  la  NEEMA  HERBALIST.
TUNAPATIKANA UBUNGO  JIJINI  DAR  ES SALAAM,  JIRANI  NA  SHULE YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING, NYUMA  YA JENGO  LA  UBUNGO  PLAZA.
Wasiliana  nasi  kwa  simu  namba  0766  53 83  84.

Kwa  wateja  waliopo  jijini  Dar  Es  Salaam, ambao  hawana  nafasi  ya  kufika  dukani kwetu  Ubungo, tunayo  huduma  ya  kuwapelekea  dawa  mahali  walipo  ( HOME & OFFICE  DELIVERY )
Kwa wateja  waliopo  mikoani , tunawatumia  dawa  kwa  njia  ya  mabasi  mbalimbali.

Kwa  wateja  waliopo  Zanzibar, tunawatumia  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  boti.
Kwa  wateja  waliopo  NAIROBI na  MOMBASA , tunawatumia  dawa  kwa  njia  ya  usafiri wa  magari mbalimbali.
Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI, tunawatumia  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  au  DHL.

Na  kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  tiba mbalimbali  za  asili, tutembelee  kila  siku  katika  blogu  yetu:Friday, April 7, 2017

KISUKARI NI UGONJWA UNAO WEZA KUDHIBITIWA KWA KUTUMIA TIBA ASILIA

Kisukari  ni  tatizo  la  kiafya  linalo wasumbua  na  kuwatesa  mamilioni  ya  watu  duniani. Miongoni  mwa  dalili  za  ugonjwa  wa  kisukari ni pamoja  na
i.                   Kukojoa  mara  kwa  mara  ( Watoto kukojoa  kitandani )
ii.                 Kunywa maji mengi kuliko kawaida na kusikia kiu kila wakati.
iii.              Kuwa dhaifu, kukosa nguvu na kujisikia mchovu kila wakati.
iv.               Kupungua uzito  kwa  kasi  au kukonda pamoja na kwamba unakula  vizuri  tena kila  wakati  kwa  sababu  ya  kusikia  njaa kila  wakati  kunakosababishwa  na  maradhi  ya  kisukari
v.                 Wanawake  kupatwa  na  tatizo  la kuwashwa ukeni.
vi.              Kupoteza  uwezo  wa Kuona  vizuri.
vii.            Wanaume  kupatwa  na  tatizo  la  ukosefu na / ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume  na  wanawake  kukosa  hamu  ya  tendo  la  ndoa.
viii.         Kupatwa  na  ganzi,  kusikia  hali  ya  kama  kuchomwachomwa au kutohisi chochote  pindi  unapoguswa  kwenye  sehemu za miguu, viganjani na  kwenye  vidole.
ix.              Miguu kuoza na hata kupata gangrini.
x.                 Kukaukwa na ngozi na pia kupata aina ya ngazi katika miguu.
xi.              Vidonda au majeraha sehemu yoyote ya mwili kutopona haraka.
xii.            Kutokwa  na   Majipu kwenye  sehemu  mbalimbali  mwilini.

 
NanasiKwa  mujibu  wa  tafiti mbalimbali  za  kitaalamu , watu walio katika makundi yafuatayo  wapo katika  hatari  kubwa  ya  kupatwa  na  ugonjwa wa kisukari kuliko watu wengine.  Watu  hao  ni  kama  ifuatavyo :

i.                   Watu  wenye   uzito uliozidi,
ii.                 Watu  wanao  toka  katika  familia  zenye  historia  ya  kuwa  na  wagonjwa  wa  kisukari.
iii.              Wanawake waliozaa watoto wenye kilo 4 au zaidi,
iv.              Watu   wasio  fanya  mazoezi 
v.                 Wagonjwa  wa  shinikizo la damu,
vi.              Watu wenye  kiasi  kikubwa  cha  lehemu  mbaya  ( Bad  Cholestrol ) kwenye  damu.
vii.            Watu  wenye   virimba  tumo (  vitambi):  Wataalamu  wa  afya  wanaeleza  kuwa, kuna hatari kubwa ya kupatwa na maradhi  ya  kisukari ikiwa mtu ana mafuta mengi katika tumbo na kiuno chake kuliko katika mapaja yake. Mafuta katika kongosho na ini huvuruga uwezo wa mwili wa kudhibiti kiasi cha sukari kwenye damu
viii.         Watu  wenye msongo wa mawazo na
ix.              Watu  wanao tumia  pombe  na kupita  kiasi  pamoja  na  wale  wavutaji  wa  sigara  kupita  kiasi: Wavutaji wa sigara wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi ya kupatwa  na  tatizo  la  kisukari,kwani kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali za  kitaalamu, uvutaji  sigara huathiri  moyo na mfumo wa mzunguko wa damu na kubana mishipa ya damu.  Tafiti  mbalimbali  za  kiafya  zinaeleza  kwamba asilimia 95 ya watu wanaougua kisukari ambao hulazimika kukatwa viungo ni wavutaji wa sigara.
x.                 Kundi  jinginge  la  watu  walio  katika  hatari  ya  kupatwa  na  maradhi  ya  kisukari  ni  watu wenye  umri  mkubwa  kuanzia  miaka  55  na  kuendelea


Wataalamu  wa  afya  wanashauri  watu walio  kwenye   orodha  iliyo  tajwa  hapo  juu, kujiwekea  utaratibu  wa  kuwa  wanapima  afya  zao  walao  mara  moja  kila  mwakaili waweze  kuchukua  hatua  stahiki  za  kiafya endapo  watakutwa  na  tatizo  la  sukari.
.

TIBA   ASILIA   KWA   WAGONJWA   WA  KISUKARI

Zipo  tiba  asilia  mbalimbali  zinazo  saidia  kkupunguza  maradhi  ya  kisukari. Miongoni  mwa  tiba  hizo  ni  pamoja  na  tiba  ijulikanayo  kama  Mkatasukari. Tiba  hii  inasaidia kushusha  na  kudhibiti  kiwango  cha  sukari  kwa  mgonjwa mwenye  sukari  ya  kupanda. Kama  unasumbuliwa na  maradhi  ya  kisukari ( Sukari  ya  kupanda ), unaweza  kujaribu  kutumia  tiba  hii.

 JINSI   YA   KUANDAA  TIBA  ASILIA  YA  MKATASUKARI

Mahitaji  ;

i.                   Nanasi  moja  kubwa
ii.                 Majani  ya  chai  vijiko vitatu vya  chakula
iii.              Maji  lita  tano
iv.              Dawa asilia  ya  Mkatasukari  vijiko  vikubwa  vitatu.

MATAYARISHO  :  Chukua  nanasi  lako  lililo  iva  vizuri, limenye  kisha  likate  vipande  vidogo vidogo,  kisha  liweke  kwenye  sufuria  halafu ndani  ya  sufuria  hilo, ongeza  lita  tano  ya  maji  safi.  Baada  ya  hapo  weka  majani ya  chai vijiko  vikubwa  vitatu, kisha  ongeza  vijiko  vikubwa vitatu  vya  dawa asilia  ya  Mkatasukari, kisha  chemsha  kwa  muda  wa  dakika  thelathini (30).
Baada  ya  dakika  thelathini, ipua   na  uchuje, makapi  weka  pembeni, kisha  hifadhi  kimiminika  chako  kwenye  chombo  safi.

MATUMIZI  :
Tumia  kunywa  kikombe  kidogo chenye ujazo milimita  mia  mbili  na  hamsini  ( 250 mills ) au  robo  lita  kwa  lugha  nyepesi. Utafanya  hivyo  mara  tatu  kwa  siku, asubuhi  mchana  na  jioni  hadi  dozi  yako  itakapo  kamilika.
Baada  ya  kutumia  dozi  hii, unashauriwa  kwenda  hospitali  kupima   tena  sukari  ili  ujue  sukari  yako  imeshuka  kwa  kiasi  gani  pamoja  na  kupata  ushauri  wa  daktari  wako.
Kwa  mahitaji  yako ya  tiba  asilia  ya  Mkatasukari, fika  katika  duka  la  NEEMA  HERBALIST. Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR ES  SALAAM,  jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.
Kwa wateja  wetu  waliopo  jijini DAR  ES  SALAAM, ambao  hawawezi  kufika  ofisini kwetu., tunatoa  huduma  ya  kuwapelekea  dawa  mahali  walipo  ( HOME & OFFICE  DELIVERY ), kwa  wateja  waliopo  Zanzibar  watasafirishiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  boti, kwa  wateja  waliopo  mikoani  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  mabasi mbalimbali. Wateja  waliopo NAIROBI  na  MOMBASA  watatumiwa  dawa  kwa  njia ya  usafiri  wa  mabasi  mbalimbali.
Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  au  DHL.
Wasiliana  nasi  kwa  simu  namba  0766  53 83 84
Na  kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee  kila  siku  katika  blogu  yetu ;

Monday, March 13, 2017

JINSI YA KUANDAA NA KUTAYARISHA LISHE MAALUMU YA KUONGEZA NA KUNENEPESHA MWILIAsali  ya  Tende

Kama umekonda  na  kudhoofika  mwili  kutokana  na  sababu  mbalimbali  kama  vile kuugua  magonjwa  na  maradhi  mbalimbali  au  kupatwa  na  msongo  mawazo, basi  fuata  maelekezo  yafuatayo  ili  upate  kujua  namna  ya  kuandaa  na  kutayarishe  lishe  maalumu  ya  asili  itakayo  kusaidia kunenepa  na  kurejesha  afya  ya  mwili  wako  katika  hali  yake  ya  kawaida.
Asali  ya  Tende: Habari njema  kwa  wateja  wetu  ni  kwamba, asali  ya  tende  sasa  inapatikana  moja  kwa  moja  dukani  kwetu.

MAHITAJI:

1.    Dawa  Lishe  ya  kuongeza  na  kunenepesha  mwili
2.   Asali  ya  tende
3.   Ufuta
4.     Ukwaju
5.    Kitunguu  swaumu
6.   Giligiliani
7.    Juisi  ya  Komamanga na  AsaliMATAYARISHO  NA  MATUMIZI
Matumizi  ya  lishe  hii, yame  gawanyika  katika  awamu  kuu  mbili. Awamu  ya  kwanza, itachukua  siku thelathini  na  awamu  ya  pili  itachukua  siku  thelathini pia. 
Katika  awamu  ya  kwanza , mgonjwa  atatumia  DAWA  LISHE  YA  KUNENEPESHA  MWILI, ASALI  YA  TENDE  NA  UFUTA  na  awamu  ya  pili, mgonjwa  atatumia   UKWAJU, KITUNGUU  SWAUMU, GILIGILIANI  na  JUISI  YA  KOMAMANGA  & ASALI  kwa  kufuata  utaratibu  utakao  elezwa  hapo  chini.

AWAMU   YA   KWANZA 
SIKU   THELATHINI  ZA  KWANZA
Mahitaji
1.   Dawa  lishe  ya  kuongeza  na  kunenepesha  mwili
2.   Ufuta
3.   Asali  ya  Tende  (   Dates  Syrup )

MATAYARISHO  , MAELEKEZO  NA  MATUMIZI

1.   Dawa –Lishe  ya  Kunenepesha  Mwili
Chukua  vijiko   vitatu vikubwa  vyenye  dawa  yako, kisha  changanya  na  maji  nusu  lita halafu chemsha  hadi  itokote, Ikiisha  tokota, ipua  acha  ipoe  kidogo kisha  tumia  kunywa  pamoja  na  machicha  yake.  Utafanya  hivyo  mara  mbili  kwa  siku  asubuhi  na  jioni  kwa  muda wa  siku  thelathini.
2.   Ufuta : Matayarisho : Chukua  vijiko  vikubwa  vinane  vyenye  ufuta, kisha  changanya  na  lita  moja  na  nusu  ya  maji. Kama  hauna  tatizo  na  sukari, unaweza  kuongeza  na  sukari  kiasi ili  kuipa  ladha.  Ikisha  tokota, ipua iache  ipoe  kiasi  kisha  tumia  kula  ufuta wote  pamoja  na  supu  yake  ama  juisi  yake. Utafanya  hivyo mara  mbili  kwa siku  asubuhi  na  jioni  kwa  muda  wa  siku  thelathini.
(N.B:   KAMA  UNA  NAFASI,  BADALA  YA  KUTUMIA  VIJIKO  VINANE  TU VYA  UFUTA  KWENYE LITA  MOJA  NA  NUSU  YA  MAJI, WEWE  TUMIA  ROBO KILO  YA  UFUTA  KWENYE  LITA  TATU  YA  MAJI, CHEMSHA  HADI  ITOKOTE,  IACHE  IPOE, KISHA  TUMIA  KULA . FANYA  HIVYO  MARA  MBILI  KWA  SIKU  ASUBUHI NA  JIONI  KWA  MUDA  WA SIKU  THELATHINI )

2.   ASALI  YA  TENDE
3.   Tumia  kula  vijiko vikubwa  vinne  vya  tende  mara  mbili  kwa siku  asubuhi  na  usiku   kwa  muda  wa  siku  thelathini. Yaani  asubuhi  kula  vijiko  vikubwa vinne  na  usiku  kula  vijiko  vikubwa vinne  vya  asali  ya  tende.
( HABARI  NJEMA  KWA  WATEJA  WETU  NI  KWAMBA, ASALI  YA  TENDE  SASA  INAPATIKANA  MOJA  KWA  MOJA  DUKANI   KWETU . UTAPATIWA  DAWA  LISHE  PAMOJA  NA  ASALI  YA  TENDE  UTAKAYO  ITUMIA  KWA  MUDA  WA  SIKU  THELATHINI  KWA  UTARATIBU  WA  MAELEKEZO  HAYO  HAPO  JUU )

AWAMU   YA  PILI
Awamu  ya  pili  ya  lishe  hii, itaanza  baada  ya  kukamilika  kwa  siku  thelathini  za  kutumia  dawa  lishe, ufuta  pamoja  na  asali  ya  tende. Kama  ilivyo  kuwa  kwa  awamu  ya  kwanza, awamu  ya  pili  pia  itachukua  muda  wa  siku  thelathini

MAHITAJI, MATAYARISHO   NA  MATUMIZI

1.                           UKWAJU
Matayarisho na  Maandalizi
Chukua ukwaju  kiasi  cha  robo kilo , weka  kwenye  maji  kiasi  cha  lita  moja, ongeza pilipili  manga kiasi cha  kijiko kimoja kidogo  ( tea spoon ) halafu ongeza sukari  vijiko  vitatu vikubwa, ongeza karafuu  ya unga  kijiko kimoja kidogo, pamoja  na hiriki vijiko  vikubwa  viwili.
Ukisha  fanya  hivyo, chemsha  hadi  mchanganyiko  wako  utokote. Ukisha  tokota, ipua  na  kuchuja  kisha  weka  kwenye  chombo  kisafi.
MATUMIZI :
            
Tumia  kunywa  mchanganyiko  huu kila  siku  asubuhi  baada  ya  kunywa  chai. Utafanya  hivyo  kwa  muda  wa  siku  thelathini  mfululizo.

2.   JUISI   YA  KOMAMANGA  NA  ASALI
Matayarisho  na  Matumizi
Tayarisha  juisi  ya  komamanga  kiasi  cha  nusu  lita, changanya  na asali ya  kawaida  vijiko vikubwa    vinane, kisha  ongeza  chumvi kijiko kidogo( tea spoon)
Koroga  mchanganyiko  wako  halafu  tumia  kunywa. Utafanya  hivyo  mara  moja   kwa  siku kwa  muda  wa  siku thelathini.
Matunda  ya  makomamanga  yanapatikana  masokoni, ingawa  mara  nyingi  hupatikana  kwa  uchache. Kama  utabahatika  kupata matunda  mengi, basi  unashauriwa  kuyachukua  kwa  wingi  na  kuyahifadhi, sehemu  salama ili usipate  usumbufu  wakati  wa  kutumia  tiba  yako.
Mbali  na  kutumika  katika lishe  ya  kuongeza  na  kunenepesha  mwili, tunda  la  komamanga, linasaidia  kuondoa  harufu  mbaya  ya  kinywa. Kwa  kuondoa  harufu  mbaya  ya  kinywa, kula  walau  tunda  moja  la  komamanga  kwa  siku  kwa  muda  wa  siku  thelathini  mfululizo. Utapata  matokeo  mazuri . ( HII  ITAWASAIDIA  ZAIDI  WALE  AMBAO  TATIZO  LAO  LA  KUTOKWA  NA  HARUFU  MBAYA  YA  KINYWA  LIMEANZIA  KINYWANI  NA  SIO  TUMBONI


ALTERNATIVE (MBADALA )  WA JUISI  YA  KOMAMANGA  ILIYO  UNGWA  NA  ASALI.
Kama  utashindwa  kupata makoma manga, basi  utafanya  kama  ifuatavyo :

KITUNGUU  SWAUMU

Chukua punje  nne  za  vitunguu  swaumu, zitwange kisha  tia  kwenye  maji nusu lita halafu ongeza  juisi  ya  ndimu  moja  au  limao  moja kisha  chemsha hadi mchanganyiko  wako  uchemke.
Matumizi :  Tumia  hivyo kila  siku  usiku baada  ya  kula  chakula cha  usiku. Utafanya  hivyo  kwa  muda  wa  siku  thelathini mfululizo.

AU
Vile vile , mbadala  mwingine wa  kutumia  juisi  ya komamanga  iliyo  changanywa  na  asali, unaweza  kutumia  JUISI  YA  GILIGILIANI  kwa  kufuata  utaratibu  ufuatao :


JUISI   YA   GILIGILIANI
MATAYARISHO   NA   MATUMIZI YA  JUISI  YA  GILI GILIANI

Chukua giligiliani  fresh, kisha zi -blend ( ZISAGE ) ili  kupata  juice  yake  kiasi  cha  robo  lita.
 Ndani  ya  juisi  yako  ya  giligiliani, kamuliamo ndimu fresh moja, halafu  ongeza  chumvi  kiasi robo  kijiko  kidogo ( tea spoon), koroga  kisha  tumia  kunywa.  Utakunywa  usiku  baada  ya  kula  chakula  cha  usiku. Utafanya  hivyo mara   moja  kwa  siku  kwa  muda  wa  siku  thelathini  mfululizo.
PIA : Jenga  utaratibu  wa  kuwa  unakula    giligiliani kwa wingi. Hakikisha  katika  kila  mlo  wako, inakuwepo  mboga  ya  giligiliani  pembeni.

VITU   VINGINE VYA   KUZINGATIA..
Pamoja na kutumia  lishe  hii  ya  asili  kwa  kufuata  utaratibu  huo  hapo  juu, unashauriwa  kuzingatia  matumizi  ya  vyakula  vifuatavyo:

TANGAWIZI
Jenga  tabia  ya  kuwa  una tumia  tangawizi, kila  mara  upatapo  nafasi.  Utaratibu  wa  jinsi  ya  kutayarisha  tangawizi ni  kama  ifuatavyo :
Chukua kipande  kimoja  cha  tangawizi, kisha  kitwange  halafu ongeza  vikombe  viwili vya  maji  vyenye  ujazo  wa  milimita  mia  mbili  na  hamsini ( 250 mills). Chemsha pamoja  kisha ongeza  maziwa  kiasi cha  robo lita  na  sukari ili kupata  ladha.  Fanya  hivi  kila  mara  uapatapo  nafasi. Ukiweza kufanya  hivyo walau  mara  mbili  kwa  siku, itakuwa  vizuri  zaidi.

  AU  chukua  kipande  kimoja  cha  tangawizi, kitwange kisha  chemsha pamoja  na  chumvi nusu  kijiko  kidogo  kwenye  maji kiasi  cha  nusu   lita  halafu tumia  kunywa  kikombe  kimoja  nusu  saa  kabla  ya  kula  chakula chako  cha  asubuhi, mchana  na usiku. 
HIRIKI
Jenga utaratibu  wa  kuwa  unakunywa  mara  kwa  mara  chai  iliyo  changanywa  na  hiriki.
MACHUNGWA
Jenga utaratibu  wa  kuwa  unakula  machungwa kwa  wingi,  kwa  kadri utakavyo  weza. Unashauriwa  kuwa  unachanganya na  chumvi  kidogo  pamoja  na  pilipili  manga.

KWA  MAHITAJI  YAKO  YA  DAWA-LISHE  YA  KUNENEPESHA  & KUONGEZA  MWILI  PAMOJA  NA  ASALI  YA  TENDE.
Kwa  mahitaji  yako  ya  DAWA-LISHE ya  kuongeza & kunenepesha  mwili, pamoja  na  asali  ya  tende, fika  katika  duka  la  NEEMA  HERBALIST. 
Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR  ES  SALAAM, jirani  na  SHULE  YA  MSINGI   UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.
WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA  0766 53 83 84.
Kwa wateja  wetu  waliopo  jijini  Dar  Es  Salaam, ambao  hawana  nafasi  ya  kufika  dukani  kwetu  Ubungo, tunayo  huduma  ya  kuwapelekea  dawa  mahali  walipo ( HOME & OFFICE  DELIVERY  )
Kwa wateja  waliopo  nje  ya  mkoa   wa  Dar  Es  Salaam,  watatumiwa  dawa  kwa  kutumia  mabasi  mbalimbali.
Kwa  wateja  waliopo  Zanzibar, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  boti.
Kwa  wateja  waliopo  ughaibuni, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  au  DHL.
Na kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee  kila  siku  katika  blogu  yetu :