Skip to main content

UJUE UGONJWA WA PUMU (ASTHMA)


Utangulizi

Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa sugu ambao huathiri njia za hewa ambazo huingiza na kutoa hewa katika mapafu. Upatapo ugonjwa wa pumu, kuta za ndani za njia ya hewa hupata maumivu (inflammation) na kuvimba.

Maumivu katika njia za hewa huzifanya kujihami kwa kusinyaa na hivyo kupunguza kiasi cha hewa kinachopita kwenda kwenye mapafu. Hali hii husababisha muathirika kutoa mlio kama wa filimbi au mluzi wakati wa kupumua.

Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa sugu lakini unaotibika. Unaweza kudhibitiwa kama vile ugonjwa wa kisukari na moyo unavyoweza kudhibitiwa.


Aina za Pumu

Kuna aina kuu mbili za pumu. Aina ya kwanza ni ile inayoanza mapema (early onset asthma) na aina ya pili ni ile inayochelewa kuanza (late onset asthma).
Kwa kifupi tutaenda kuangalia tofauti chache kati ya aina hizi za pumu.

Pumu inayoanza mapema

Ni kawaida kwa aina hii ya pumu kuanza utotoni na kwa kawaida huwatokea waathirika ambao miili yao hutengeneza kingamwili (antibodies) za IgE.
Waathirika wa aina hii ya pumu hutambuliwa kwa vipimo maalum vya ngozi ambapo huonesha kuathirika kwa asilimia kubwa vipimo hivyo vinapofanywa.

Pia waathirika hawa huwa na matatizo mengine ya mzio (allergic disorders) kama mafua na ukurutu (eczema).

Pumu inayochelewa kuanza
Aina hii ya pumu tofauti na iliyopita huanza katika umri wowote na asilimia kubwa ya waathirika ni watu wazima. Hakuna ushahidi wowote unaohusianisha vizio (allergens) vinavyotokana na mazingira na uwezo wa kusababisha aina hii ya pumu.

Pumu husababishwa na nini?


Bila shaka mpenzi msomaji umekua ukijiuliza swali hili mara kwa mara. Haifahamiki haswa ni sababu zipi zinazopelekea njia za hewa kupata maumivu na hivyo kupelekea mtu kupata pumu.

Vyanzo mbali mbali vinaonyesha kuwa inatokana na mseto wa vitu kama tumbaku, maradhi na baadhi ya vizio.

Pia kuna vitu katika mazingira ambavyo vinaweza kusababisha mtu kushambuliwa na pumu. Vitu kama vile mazoezi, vizio, viwasho (irritants) na maradhi yatokanayo na virusi.

Baadhi ya vizio ni kama vifuatavyo:

-Vumbi
-Mende
-Chavua (pollen) kutoka kwenye miti na majani
-Magamba ya wanyama, manyoya n.k

Viwasho kama:
-Moshi wa sigara
-Uchafuzi wa hewa
-Harufu kali (kutoka kwenye rangi au chakula)
-Msongo wa mawazo

Vingine ni kama:
-Dawa kama Aspirin
-Ugonjwa wa kucheua
-Viwasho au vizio vitokanavyo na kemikali
-Magonjwa ya njia ya hewa n.k

Ieleweke kwamba orodha iliyotajwa hapo juu siyo kamilifu kwa maana kwamba haijasheheni vitu vyote vinavyoweza kuleta dalili za pumu na pia muathirika anaweza kuathirika na kimoja wapo au zaidi.

Vigezo hatarishi

Baadhi ya vigezo hatarishi vinavyoweza kuongeza uwezekano wa kusababisha ugonjwa wa pumu ni pamoja na:

-Kuishi katika miji mikubwa, haswa katikati ya mji ambapo huongeza uwezekano wa kukutana na vizio

-Kuvuta hewa iliyo na moshi

-Kemikali zitokanazo na kilimo, dawa za kutengeneza nywele, rangi, vyuma, plastiki au vifaa vya elektroniki

-Kuwa na mzazi mmoja au wawili wenye pumu
-Kuathirika na maradhi ya mfumo wa hewa kama kikohozi na mafua wakati wa utoto.

-Unene wa kupita kiasi (obesity)

-Ugonjwa wa kucheua na kiungulia (Gastro esophageal reflux disease)

Dalili za Pumu

Baadhi ya dalili za kawaida za ugonjwa wa pumu ni kama zifuatazo:

-Kikohozi: Mara nyingi kikohozi cha pumu huwa kikali nyakati za usiku au alfajiri na hivyo kumfanya mwathirika kutolala vizuri

-Kutoa sauti ya mfano wa mtu anayepiga mluzi au filimbi wakati wa kupumua

-Kifua kubana: Mgonjwa husikia kama kitu kinakandamiza kifuani au wakati mwingine husikia kama mtu amemkalia kifuani.

-Kukosa hewa: Baadhi hujisikia kama hawawezi kupumua na kukosa hewa ya kutosha inayoingia au kutoka kwenye mapafu.

-Kupumua haraka haraka

Ikumbukwe kwamba si watu wote huwa na dalili zilizokwisha tajwa hapo juu na dalili zaweza kutofautiana kati ya mtu na mtu.

Dalili pia zinatofautiana ukali. Wakati kwa mwingine dalili zinakuwa za wastani, wengine zinakuwa za kukera tu au mbaya kiasi cha kumzuia muathirika kufanya shughuli zake za kila siku.

Vile vile wapo wengine ambao dalili zinakuwa mbaya kiasi cha kuhatarisha maisha. Dalili pia zaweza kutofautiana kwa kipindi zinapotokea.

Wengine hupata dalili mara moja tu kwa mwezi, wengine kila wiki na wengine hupata dalili kila siku.

Hata hivyo iwapo muathirika atapata matibabu sahihi anaweza kuishi na dalili chache au bila dalili kabisa.

Uchunguzi

Kipimo cha muhimu katika uchunguzi iwapo mtu ameathirika na pumu ni kuangalia jinsi mapafu yanavyofanya kazi.

Kipimo hicho kijulikanacho kwa lugha ya kitaalamu kama spirometry hutathmini kiasi cha hewa mtu awezacho kukitoa baada ya kuvuta hewa kwa nguvu na kwa haraka kiasi gani.

Viwango huwa chini ya kawaida iwapo njia za hewa zina maumivu na zimesinyaa. Kipimo hicho cha spirometry pia hutumika kutathmini jinsi mgonjwa wa pumu anavyoendelea kupata nafuu au tatizo kuongezeka.

Hata hivyo kipimo hicho ni kwa ajili ya watoto wenye zaidi ya miaka mitano na watu wazima tu.

Baadhi ya vipimo vingine vinavyoweza kufanywa iwapo kipimo cha spirometry hakitaonesha tatizo ni:

Kipimo cha Kizio (Allergy test)


Husadia kugundua iwapo kuna vizio mbalimbali vinavyoathiri mwili wako.

Kipimo cha Mazoezi


Kugundua iwapo kuna mabadiliko yoyote katika njia ya hewa kutokana na mazoezi.

Kipimo cha Ugonjwa wa Kucheua na Kiungulia


Kipimo hiki ni muhimu pia kutokana na uhusiano uliopo kati ya kiungulia, kucheua na ugonjwa wa pumu.

Kipimo cha Picha ya Mapafu (X-ray)

Kipimo hiki pia hutumika kuona iwapo kuna kitu chochote kilichoziba njia ya hewa au kama kuna maradhi yoyote katika mapafu au moyo.

Kutokana na vipimo daktari wako atapata picha ya ukali wa pumu yako na kukuanzishia tiba muafaka.

Matibabu

Kuna aina mbili za matibabu ya pumu. Moja ni ile ya dharura ili kutoa msaada au nafuu ya haraka. Dawa hizi ni zile zinazosaidia kutanua njia za hewa ambazo zimesinyaa (bronchodilators) pia husaidia kuilainisha misuli ya njia za hewa iliyosinyaa ili iweze kutanuka na kuruhusu hewa ya kutosha kuingia.

Ni vizuri kutumia dawa za kuleta nafuu haraka punde uonapo dalili za pumu zilizoorodheshwa hapo juu.

Aina nyingine ya dawa ni zile za muda mrefu. Aina hizi za dawa hutumiwa mara kwa mara kwa kipindi kirefu kuzuia dalili za pumu na mashambulizi.

Watu wenye pumu isiyoisha wanahitaji matumizi ya dawa ya muda mrefu. Kotikosteroidi za kuvuta (inhaled corticosteroids) ni nzuri kwa aina hii ya pumu.

Matibabu ya pumu kwa watoto

Watoto wenye pumu kama ilivyo kwa watu wazima wanapaswa kumwona daktari kwa matibabu. Watoto walio na umri mdogo wanahitaji uangalizi wa wazazi/walezi ili kudhibiti pumu.

Watoto wenye umri mkubwa wanaweza kujifunza wenyewe jinsi ya kutumia dawa chini ya uangalizi mdogo kutoka kwa wazazi.

Matibabu ya pumu kwa watu wazima

Watu wazima wanaweza kutakiwa kupunguza au kuongeza matumizi ya dawa za pumu kutokana na maradhi mengine waliyonayo.

Dawa kama ya kutibu shinikizo la juu la damu, ugonjwa unaotanua mboni ya jicho na kutatiza kuona (glaucoma), aspirini na dawa za maumivu (non steroidal anti inflammatory drugs) huingiliana na utendaji wa dawa za pumu au zenyewe kusababisha pumu.

Matibabu wakati wa ujauzito

Ni muhimu kudhibiti vyema ugonjwa wa pumu wakati wa mimba kwani iwapo utasababisha kusinyaa kwa njia ya hewa basi waweza kupelekea upungufu wa hewa ya oksijeni kwa mtoto hali ambayo ni hatari kwa mtoto.

Dawa nyingi za pumu hazina madhara kwa kichanga hivyo ni muhimu kuendelea na matibabu wakati wa mimba kuliko kuacha.

Kinga

Njia pekee ya kujikinga na pumu ni kuepuka vizio vinavyoweza kusababisha kuanza kwa dalili za pumu. Waweza fanya hivyo kwa kusafisha nyumba kila wiki kupunguza vumbi.

Pia unatakiwa kuepuka kufanya mazoezi kwenye baridi, epuka moshi wa sigara, dhibiti ugonjwa wa kucheua na kiungulia, epuka kukaa na wanyama na epuka kuishi katika mazingira yenye hewa yenye unyevunyevu.

Ushauri

Jinsi ya kumsaidia mtoto mwenye pumu

-Mpeleke kwa daktari kwa uchunguzi wa mara kwa mara na matibabu.

-Mueleweshe kuhusu pumu na jinsi ya kuidhibiti.

-Mueleweshe ajue vitu vinavyoweza kusababisha yeye kupata dalili za pumu na jinsi ya kuepukana navyo.

-Muepushe na moshi wa sigara kwa kutovuta sigara na kutoruhusu watu kuvuta sigara nyumbani kwako.

-Tafuta jinsi ya kumpunguzia mtoto wako kukutana na vizio kama vumbi, chavua, mende n.k

-Hakikisha anatumia dawa kama inavyotakiwa

-Mhimize kufanya mazoezi ya viungo.

Chanzo : Gazeti la Majira (Mtandao)www.majira.co.tz


 

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ya  kupata  wapenzi  wa  kike  ama  kuoa  na  wengine  huendelea  na  tabia  hiyo  hata  baada  ya  kuoa .  Zipo  sababu  mbalimbali  zinazo  wapelekea  wanaume  kupiga  punyeto, ila  kubwa  kati  ya  hizo  ni  pamoja  na  kutokuwa  na  wapenzi, kutokuwa  na  wapenzi  wanao  kidhi vigezo  vyao, kuwa  katika  mazingira  yasiyokuwa  na  wanawake  ( mfano  katika  shule  za  sekonda

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS

Dawa ya TONSILS ni (kugargar)  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto. Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia. Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako. Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafanya ka

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na  kuwa  mgumu  kama  msumari. Na  hatua  ya  pili   ni  lazima, uume  wake  uendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa  STRONGER  AND  LONGER  ERECTION JINSI  HATUA  ZA  KUSIMAMA  KWA  UUME  ZINAVYO  TOKEA. 1. HATUA    YA  KWANZA: DAMU  KUTIRIRIKA  KWA