Skip to main content

Ushauri wa lishe na ulaji kwa mtu mwenye ugonjwa wa figo




Figo
Magonjwa ya figo

Figo hufanya kazi muhimu mwilini ambazo ni:-
Kudhibiti na kuhifadhi virutubishi na maji na kuondoa mabaki kupitia mkojo.
Kuchuja damu ili kuondoa mabaki ambayo ni sumu mwilini. Baadhi ya mabaki hayo ni urea, uric acid, creatinine na ammonia.
Kudhibiti viwango vya electrolyte mwilini, yaani Sodium (Na+ ) na Potassium (K+). Sodium husaidia kudhibiti wingi wa maji mwilini na pia huwezesha mawasiliano kati ya mfumo wa fahamu na misuli (enhances commucacation between brain/nerves and muscles). Potassium husaidia mapigo ya moyo between brain/nerves and muscles). Potassimu husaidia mapigo ya moyo (regulates heart beats) na kazi ya misuli (muscle function). Viwango vya kawaida kwa Sodium ni 135-145 mmol/L na Potassimu ni 3.5-5 mmol/L.
Kudhibiti shinikizo la damu kupitia mfumo wa rennin-angiotension.
Kutengeneza kichocheo cha Erythropoietin ambacho huchochea utengenezaji wa chembechembe nyekundu za damu.
Kuchochea vitamin D ambayo hutumika katika kudhibiti kiwango cha Calcium na Phosphorous kwenye mifupa.

Iwapo mtu atapata ugonjwa wa figo ambao utaathiri figo zote mbili, kazi zote hizo hapo juu huathirika au kushindwa kufanyika kwa ufanisi na
madhara hutokea kutengemea kiwango cha athari. Figo zinaweza kushindwa kufanya kazi aidha kwa sababu za kipindi kifupi (acute renal failure) au kwa sababu za muda mrefu (chronic renal failure).
Sababu zinazoweza kufanya figo zishindwe kufanya kazi:
i) Katika muda mfupi:
o Upungufu mkubwa wa ujazo wa damu (kupoteza damu kwa kiasi kikubwa)
o Upungufu wa maji mwilini kutokana na kutapika, kuhara, na homa
o Matumizi ya baadhi ya dawa kama diuretics
o Mawe kwenye figo (kidney stones)
o Maambukizi kwenye figo mfano sepsis
o Uvimbe –uchungu (inflammation) kwenye mfumo wa uchujaji kwenye figo (acute glomerulonephritis)
o Uvimbe mkubwa wa tezi dume (prostatic hypertrophy)
o Saratani ya tezi dume (prostate cancer)

ii) Katika muda mrefu
o Kisukari kisichodhibitiwa
o Shinikizo kubwa la damu lisilodhibitiwa
o Uvimbe-uchungu wa kudumu kwenye mfumo wa uchujaji wa figo(chronic glomerulonephritis)
o Mawe kwenye figo
o Magonjwa ya tezi dume (Prostate disease)

Dalili za ugonjwa wa figo:-
Mwanzoni, ugonjwa wa figo hauoneshi dalili yeyote. Mara utendaji kazi wa figo unapopungua, dalili hujitokeza kuendana na udhaifu wa kudhibiti maji na electrolyte mwilini; kuondoa mabaki mwili; kutengeneza erythropoietin ambayo huchochea utengenezaji wa chembechembe nyekundu za damu, na pia udhaifu wa kuchochea Vitamini D ambayo ni muhimu katika kuweka viwango sahihi vya calcium-phosphorous kwenye mifupa, misuli na neva.
• Dalili za mwanzo ni kama:-
o Kudhoofika,
o Kuchoka mara kwa mara
o Kukosa nguvu,
o Kukosa pumzi/kupumua kwa shida
o Kuvimba mwili (hasa usoni), na
o Homa isiyokuwa kali

Hali hii isipogundulika mapema huweza kusababisha hatari ya kupoteza maisha.
Udhaifu wa kutoa Sodium (Na+) mwilini husababisha wingi wa Sodium mwilini (hypernatremia) ambao huambatana na kujaa kwa maji mwilini (generalized oedema) kuongonzeka uzito ghafla, ongezeko la shinikizo la damu, kushindwa kupumua mwisho husababisha ugonjwa wa moyo (congestive heart failure).
Udhaifu wa Potassium (K+) mwilini husababisha wingi wa potassium mwilini (hyperkalemia) ambao husababisha misuli kukosa nguvu au kuwa dhaifu na mapigo ya moyo kuenda ovyo ovyo (arrhythmias) na ikizidi huweza kusababisha kifo cha ghafla.
Kushindwa kutolewa kwa urea mwilini husababisha uharibifu kwenye ubongo (encephalopathy).
Udhaifu kwa ujumla husababishwa na upungufu mkubwa wa damu ambao husababishwa na kushuka kwa uwezo wa figo kutengeneza erythropoietin hivyo chembechembe nyekundu za damu kupungua.
Kukosekana kwa uwiano unaotakiwa kati ya phosphorous na calcium huweza kufanya mifupa kuwa miepesi kuvunjika.

Ushauri wa lishe na ulaji kwa mtu mwenye ugonjwa wa figo
Ulaji wa mtu mwenye ugonjwa wa figo unapaswa kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwani figo haziwezi tena kutoa mabaki ya protin, maji, chumvi na potassium kwa urahisi inapozidi mwilini. Vyakula vyenye chumvi na potassium nyingi viepukwe ikiwa ni pamoja na kuzingatia mambo yafuatayo:
Mambo ya kuzingatia katika ulaji:-
Punguza kiasi cha nishati-lishe. Kiasi cha nishati-lishe na protini kinapozidi mwilini huzipatia figo ambazo zimeathirika kazi kubwa.

Punguza kiasi cha vinywaji/vimiminika- ili kupunguza kujaa kwa maji mwilini ambako husababishwa na kushindwa kwa figo kutoa maji mwilini. Maji yakizidi mwilini husababisha kushindwa kupumua, shinikizo kuwa la damu, kuvimba mwili na huweza kusababisha
ugonjwa wa moyo (heart failure). Dhibiti ongezeko la uzito wa mwili kwani huweza kuonesha kuwa maji yamezidi mwilini.
Punguza kiasi cha sodium: Kiasi cha maji mwilini hudhibitiwa na sodium. Pale sodium inapozidi mwilini husababisha maji kubaki mwilini. Hali hii huweza kusababisha ongezeko la uzito ghafla, kuvimba kwa viungio vya mwili, shinikizo kubwa la damu, kushindwa kupumua na huweza kusababisha ugonjwa wa moyo. Vyakula vyenye sodium kwa wingi ni vyakula vilivyosindikiwa kwa chumvi (nyama, samaki, soseji, bacon). Jenga tabia ya kutoongeza chumvi kwenye chakula wakati wa kula.

Punguza kiasi cha potassium: Madini ya potassium yanapozidi mwilini husababisha misuli kuwa dhaifu na mapigo ya moyo kubadilika na yakizidi sana hueza kusababisha kifo cha ghafla. Ni muhimu kudhibiti kiasi cha potassium kwa ukaribu. Vyakula vyenye potassium kwa kiasi kikubwa ni pamoja na maparachichi, ndizi mbivu, maboga, machungwa, pichesi, peasi, matunda yaliyokaushwa na maharagwe. Vyakula vyenye potassium kwa kiasi kidogo ni pamoja na zabibu, machenza, mahindi mabichi, cauliflower, na matango.

Unaweza kupunguza kiasi cha potassium kwenye chakula kwa kuchemsha na kumwaga maji za ziada.
Kiasi cha potassium kinachoshauriwa kwa siku kwa mtu wa kawaida ni gramu 4.7 (milligram 4,700). Kwa mgonjwa wa figo inashauriwa gramu 1.5-2.7 (milligram 1500-2700) kwa siku na kila mlo asizidishe gramu 0.25 (miligramu 250).
Punguza kiasi cha phosphorus

Uwiano wa calcium na phosphorus mwilini ni muhimu kuwezesha afya njema ya mifupa, misuli na neva. Phosphorus inapozidi mwilini mifupa huwa myepesi kuvunjika (brittle) na rahisi kuvunjika. Hii inatokana na mwili kutoa calcium kwenye mifupa vyakula ambavyo vina phosphorus kwa wingi ni pamoja na maziwa na mazao yake, nyama, shellfish, vyakula amvavyo havijakobolewa, maharage, karanga, korosho na chokoleti.

 Vitamini na madini ya nyongeza

Wagonjwa wa figo huhitaji vitamin na madini ya nyongeza kutokana na kutokula aina mbalimbali za vyakula na hivyo kuweza kusababisha
upunfugu wa baadhi ya virutubishi. Damu inapochujwa (dialysis) pia huondoa vitamin kwenye damu. Virutubishi vya nyongeza vitolewe kwa mgonjwa wa figo kwa ushauri wa daktari.

Comments

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ya  kupata  wapenzi  wa  kike  ama  kuoa  na  wengine  huendelea  na  tabia  hiyo  hata  baada  ya  kuoa .  Zipo  sababu  mbalimbali  zinazo  wapelekea  wanaume  kupiga  punyeto, ila  kubwa  kati  ya  hizo  ni  pamoja  na  kutokuwa  na  wapenzi, kutokuwa  na  wapenzi  wanao  kidhi vigezo  vyao, kuwa  katika  mazingira  yasiyokuwa  na  wanawake  ( mfano  katika  shule  za  sekonda

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS

Dawa ya TONSILS ni (kugargar)  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto. Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia. Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako. Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafanya ka

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na  kuwa  mgumu  kama  msumari. Na  hatua  ya  pili   ni  lazima, uume  wake  uendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa  STRONGER  AND  LONGER  ERECTION JINSI  HATUA  ZA  KUSIMAMA  KWA  UUME  ZINAVYO  TOKEA. 1. HATUA    YA  KWANZA: DAMU  KUTIRIRIKA  KWA