Skip to main content

Posts

Showing posts from June, 2016

UKATILI MASHULENI

UKATILI.......Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Isevya iliyoko Manispaa ya Tabora wakionesha majeraha ya magoti yao baada ya kupewa adhabu ya kinyama na mwalimu wao. Walipigishwa magoti kwa saa 5 kwenye mchanga uliopata joto la jua kwa zaidi ya saa tano. Fikiria mwanao anakuja nyumbani hivi! Ukatili mkubwa na sijui mafunzo ya adhabu hizi walimu walipewa wapi? Maana hata JKT na CCP haya hayapo! Vitendo vya namna hii vinapaswa kuibua mjadala mkubwa kijamii na kutusaidia kufumua mfumo wa elimu yetu. Mtatiro J