Skip to main content

JINSI YA KUANDAA NA KUTAYARISHA LISHE MAALUMU YA KUONGEZA NA KUNENEPESHA MWILI



Asali  ya  Tende

Kama umekonda  na  kudhoofika  mwili  kutokana  na  sababu  mbalimbali  kama  vile kuugua  magonjwa  na  maradhi  mbalimbali  au  kupatwa  na  msongo  mawazo, basi  fuata  maelekezo  yafuatayo  ili  upate  kujua  namna  ya  kuandaa  na  kutayarishe  lishe  maalumu  ya  asili  itakayo  kusaidia kunenepa  na  kurejesha  afya  ya  mwili  wako  katika  hali  yake  ya  kawaida.
Asali  ya  Tende: Habari njema  kwa  wateja  wetu  ni  kwamba, asali  ya  tende  sasa  inapatikana  moja  kwa  moja  dukani  kwetu.

MAHITAJI:

1.    Dawa  Lishe  ya  kuongeza  na  kunenepesha  mwili
2.   Asali  ya  tende
3.   Ufuta
4.     Ukwaju
5.    Kitunguu  swaumu
6.   Giligiliani
7.    Juisi  ya  Komamanga na  Asali







MATAYARISHO  NA  MATUMIZI
Matumizi  ya  lishe  hii, yame  gawanyika  katika  awamu  kuu  mbili. Awamu  ya  kwanza, itachukua  siku thelathini  na  awamu  ya  pili  itachukua  siku  thelathini pia. 
Katika  awamu  ya  kwanza , mgonjwa  atatumia  DAWA  LISHE  YA  KUNENEPESHA  MWILI, ASALI  YA  TENDE  NA  UFUTA  na  awamu  ya  pili, mgonjwa  atatumia   UKWAJU, KITUNGUU  SWAUMU, GILIGILIANI  na  JUISI  YA  KOMAMANGA  & ASALI  kwa  kufuata  utaratibu  utakao  elezwa  hapo  chini.

AWAMU   YA   KWANZA 
SIKU   THELATHINI  ZA  KWANZA
Mahitaji
1.   Dawa  lishe  ya  kuongeza  na  kunenepesha  mwili
2.   Ufuta
3.   Asali  ya  Tende  (   Dates  Syrup )

MATAYARISHO  , MAELEKEZO  NA  MATUMIZI

1.   Dawa –Lishe  ya  Kunenepesha  Mwili
Chukua  vijiko   vitatu vikubwa  vyenye  dawa  yako, kisha  changanya  na  maji  nusu  lita halafu chemsha  hadi  itokote, Ikiisha  tokota, ipua  acha  ipoe  kidogo kisha  tumia  kunywa  pamoja  na  machicha  yake.  Utafanya  hivyo  mara  mbili  kwa  siku  asubuhi  na  jioni  kwa  muda wa  siku  thelathini.
2.   Ufuta : Matayarisho : Chukua  vijiko  vikubwa  vinane  vyenye  ufuta, kisha  changanya  na  lita  moja  na  nusu  ya  maji. Kama  hauna  tatizo  na  sukari, unaweza  kuongeza  na  sukari  kiasi ili  kuipa  ladha.  Ikisha  tokota, ipua iache  ipoe  kiasi  kisha  tumia  kula  ufuta wote  pamoja  na  supu  yake  ama  juisi  yake. Utafanya  hivyo mara  mbili  kwa siku  asubuhi  na  jioni  kwa  muda  wa  siku  thelathini.
(N.B:   KAMA  UNA  NAFASI,  BADALA  YA  KUTUMIA  VIJIKO  VINANE  TU VYA  UFUTA  KWENYE LITA  MOJA  NA  NUSU  YA  MAJI, WEWE  TUMIA  ROBO KILO  YA  UFUTA  KWENYE  LITA  TATU  YA  MAJI, CHEMSHA  HADI  ITOKOTE,  IACHE  IPOE, KISHA  TUMIA  KULA . FANYA  HIVYO  MARA  MBILI  KWA  SIKU  ASUBUHI NA  JIONI  KWA  MUDA  WA SIKU  THELATHINI )

2.   ASALI  YA  TENDE
3.   Tumia  kula  vijiko vikubwa  vinne  vya  tende  mara  mbili  kwa siku  asubuhi  na  usiku   kwa  muda  wa  siku  thelathini. Yaani  asubuhi  kula  vijiko  vikubwa vinne  na  usiku  kula  vijiko  vikubwa vinne  vya  asali  ya  tende.
( HABARI  NJEMA  KWA  WATEJA  WETU  NI  KWAMBA, ASALI  YA  TENDE  SASA  INAPATIKANA  MOJA  KWA  MOJA  DUKANI   KWETU . UTAPATIWA  DAWA  LISHE  PAMOJA  NA  ASALI  YA  TENDE  UTAKAYO  ITUMIA  KWA  MUDA  WA  SIKU  THELATHINI  KWA  UTARATIBU  WA  MAELEKEZO  HAYO  HAPO  JUU )

AWAMU   YA  PILI
Awamu  ya  pili  ya  lishe  hii, itaanza  baada  ya  kukamilika  kwa  siku  thelathini  za  kutumia  dawa  lishe, ufuta  pamoja  na  asali  ya  tende. Kama  ilivyo  kuwa  kwa  awamu  ya  kwanza, awamu  ya  pili  pia  itachukua  muda  wa  siku  thelathini

MAHITAJI, MATAYARISHO   NA  MATUMIZI

1.                           UKWAJU
Matayarisho na  Maandalizi
Chukua ukwaju  kiasi  cha  robo kilo , weka  kwenye  maji  kiasi  cha  lita  moja, ongeza pilipili  manga kiasi cha  kijiko kimoja kidogo  ( tea spoon ) halafu ongeza sukari  vijiko  vitatu vikubwa, ongeza karafuu  ya unga  kijiko kimoja kidogo, pamoja  na hiriki vijiko  vikubwa  viwili.
Ukisha  fanya  hivyo, chemsha  hadi  mchanganyiko  wako  utokote. Ukisha  tokota, ipua  na  kuchuja  kisha  weka  kwenye  chombo  kisafi.
MATUMIZI :
            
Tumia  kunywa  mchanganyiko  huu kila  siku  asubuhi  baada  ya  kunywa  chai. Utafanya  hivyo  kwa  muda  wa  siku  thelathini  mfululizo.

2.   JUISI   YA  KOMAMANGA  NA  ASALI
Matayarisho  na  Matumizi
Tayarisha  juisi  ya  komamanga  kiasi  cha  nusu  lita, changanya  na asali ya  kawaida  vijiko vikubwa    vinane, kisha  ongeza  chumvi kijiko kidogo( tea spoon)
Koroga  mchanganyiko  wako  halafu  tumia  kunywa. Utafanya  hivyo  mara  moja   kwa  siku kwa  muda  wa  siku thelathini.
Matunda  ya  makomamanga  yanapatikana  masokoni, ingawa  mara  nyingi  hupatikana  kwa  uchache. Kama  utabahatika  kupata matunda  mengi, basi  unashauriwa  kuyachukua  kwa  wingi  na  kuyahifadhi, sehemu  salama ili usipate  usumbufu  wakati  wa  kutumia  tiba  yako.
Mbali  na  kutumika  katika lishe  ya  kuongeza  na  kunenepesha  mwili, tunda  la  komamanga, linasaidia  kuondoa  harufu  mbaya  ya  kinywa. Kwa  kuondoa  harufu  mbaya  ya  kinywa, kula  walau  tunda  moja  la  komamanga  kwa  siku  kwa  muda  wa  siku  thelathini  mfululizo. Utapata  matokeo  mazuri . ( HII  ITAWASAIDIA  ZAIDI  WALE  AMBAO  TATIZO  LAO  LA  KUTOKWA  NA  HARUFU  MBAYA  YA  KINYWA  LIMEANZIA  KINYWANI  NA  SIO  TUMBONI


ALTERNATIVE (MBADALA )  WA JUISI  YA  KOMAMANGA  ILIYO  UNGWA  NA  ASALI.
Kama  utashindwa  kupata makoma manga, basi  utafanya  kama  ifuatavyo :

KITUNGUU  SWAUMU

Chukua punje  nne  za  vitunguu  swaumu, zitwange kisha  tia  kwenye  maji nusu lita halafu ongeza  juisi  ya  ndimu  moja  au  limao  moja kisha  chemsha hadi mchanganyiko  wako  uchemke.
Matumizi :  Tumia  hivyo kila  siku  usiku baada  ya  kula  chakula cha  usiku. Utafanya  hivyo  kwa  muda  wa  siku  thelathini mfululizo.

AU
Vile vile , mbadala  mwingine wa  kutumia  juisi  ya komamanga  iliyo  changanywa  na  asali, unaweza  kutumia  JUISI  YA  GILIGILIANI  kwa  kufuata  utaratibu  ufuatao :


JUISI   YA   GILIGILIANI
MATAYARISHO   NA   MATUMIZI YA  JUISI  YA  GILI GILIANI

Chukua giligiliani  fresh, kisha zi -blend ( ZISAGE ) ili  kupata  juice  yake  kiasi  cha  robo  lita.
 Ndani  ya  juisi  yako  ya  giligiliani, kamuliamo ndimu fresh moja, halafu  ongeza  chumvi  kiasi robo  kijiko  kidogo ( tea spoon), koroga  kisha  tumia  kunywa.  Utakunywa  usiku  baada  ya  kula  chakula  cha  usiku. Utafanya  hivyo mara   moja  kwa  siku  kwa  muda  wa  siku  thelathini  mfululizo.
PIA : Jenga  utaratibu  wa  kuwa  unakula    giligiliani kwa wingi. Hakikisha  katika  kila  mlo  wako, inakuwepo  mboga  ya  giligiliani  pembeni.

VITU   VINGINE VYA   KUZINGATIA..
Pamoja na kutumia  lishe  hii  ya  asili  kwa  kufuata  utaratibu  huo  hapo  juu, unashauriwa  kuzingatia  matumizi  ya  vyakula  vifuatavyo:

TANGAWIZI
Jenga  tabia  ya  kuwa  una tumia  tangawizi, kila  mara  upatapo  nafasi.  Utaratibu  wa  jinsi  ya  kutayarisha  tangawizi ni  kama  ifuatavyo :
Chukua kipande  kimoja  cha  tangawizi, kisha  kitwange  halafu ongeza  vikombe  viwili vya  maji  vyenye  ujazo  wa  milimita  mia  mbili  na  hamsini ( 250 mills). Chemsha pamoja  kisha ongeza  maziwa  kiasi cha  robo lita  na  sukari ili kupata  ladha.  Fanya  hivi  kila  mara  uapatapo  nafasi. Ukiweza kufanya  hivyo walau  mara  mbili  kwa  siku, itakuwa  vizuri  zaidi.

  AU  chukua  kipande  kimoja  cha  tangawizi, kitwange kisha  chemsha pamoja  na  chumvi nusu  kijiko  kidogo  kwenye  maji kiasi  cha  nusu   lita  halafu tumia  kunywa  kikombe  kimoja  nusu  saa  kabla  ya  kula  chakula chako  cha  asubuhi, mchana  na usiku. 
HIRIKI
Jenga utaratibu  wa  kuwa  unakunywa  mara  kwa  mara  chai  iliyo  changanywa  na  hiriki.
MACHUNGWA
Jenga utaratibu  wa  kuwa  unakula  machungwa kwa  wingi,  kwa  kadri utakavyo  weza. Unashauriwa  kuwa  unachanganya na  chumvi  kidogo  pamoja  na  pilipili  manga.

KWA  MAHITAJI  YAKO  YA  DAWA-LISHE  YA  KUNENEPESHA  & KUONGEZA  MWILI  PAMOJA  NA  ASALI  YA  TENDE.
Kwa  mahitaji  yako  ya  DAWA-LISHE ya  kuongeza & kunenepesha  mwili, pamoja  na  asali  ya  tende, fika  katika  duka  la  NEEMA  HERBALIST. 
Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR  ES  SALAAM, jirani  na  SHULE  YA  MSINGI   UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.
WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA  0766 53 83 84.
Kwa wateja  wetu  waliopo  jijini  Dar  Es  Salaam, ambao  hawana  nafasi  ya  kufika  dukani  kwetu  Ubungo, tunayo  huduma  ya  kuwapelekea  dawa  mahali  walipo ( HOME & OFFICE  DELIVERY  )
Kwa wateja  waliopo  nje  ya  mkoa   wa  Dar  Es  Salaam,  watatumiwa  dawa  kwa  kutumia  mabasi  mbalimbali.
Kwa  wateja  waliopo  Zanzibar, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  boti.
Kwa  wateja  waliopo  ughaibuni, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  au  DHL.
Na kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee  kila  siku  katika  blogu  yetu :

Comments

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ya  kupata  wapenzi  wa  kike  ama  kuoa  na  wengine  huendelea  na  tabia  hiyo  hata  baada  ya  kuoa .  Zipo  sababu  mbalimbali  zinazo  wapelekea  wanaume  kupiga  punyeto, ila  kubwa  kati  ya  hizo  ni  pamoja  na  kutokuwa  na  wapenzi, kutokuwa  na  wapenzi  wanao  kidhi vigezo  vyao, kuwa  katika  mazingira  yasiyokuwa  na  wanawake  ( mfano  katika  shule  za  sekonda

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS

Dawa ya TONSILS ni (kugargar)  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto. Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia. Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako. Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafanya ka

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na  kuwa  mgumu  kama  msumari. Na  hatua  ya  pili   ni  lazima, uume  wake  uendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa  STRONGER  AND  LONGER  ERECTION JINSI  HATUA  ZA  KUSIMAMA  KWA  UUME  ZINAVYO  TOKEA. 1. HATUA    YA  KWANZA: DAMU  KUTIRIRIKA  KWA