Mamilioni ya watu duniani wanasumbuliwa na maradhi mbalimbali ya moyo. Inapotajwa maradhi ya moyo maana yake ni uwepo wa hitilafu mbalimbali ndani ya moyo au zinazo husiana na moyo ambazo husababisha moyo kutokufanya kazi sawa sawa. Kupanuka kwa moyo , mapigo ya moyo kwenda kasi na shinikizo kuu la damu ni miongoni mwa maradhi yanayo tajwa na wataalamu wa afya kama maradhi ya moyo. Katika tiba asilia, mmea wa Mmoyomoyo unatajwa kuwa na uwezo mkubwa wa kudhibiti na kupambana na maradhi mbalimba...