UHUSIANO KATI YA KITAMBI NA TATIZO LA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME Kuna andiko linasema “ ASIYE FANYA KAZI NA ASILE “ Msingi wa andiko hili ni ku promote spirit ya kujishughulisha na ku discourage spirit ya uvivu “ iddleness” katika jamii. Hata hivyo andiko hilo linaweza kuwa na maana nyingine ya ziada. Maana hii ya ziada ni tafsiri yangu binafsi kulingana na muktadha wa makala hii ya leo. Maana hii ya ziada ndio msingi wa mada yetu hii ya leo. Kama nilivyo dokeza hapo juu, andiko asiye fanya kazi na asile linaweza kuwa na maana nyingine ya ziada ambayo kimsingi haitofautiani sana na maana ya msingi ya andiko lenyewe. Maana hii inaweza kuwa “ ASIYE USHUGHULISHA MWILI WAKE NA ASILE CHAKULA “ kwa sababu mtu akila chakula bila kuushughulisha mwili wake chakula hicho kitaenda kubadilika na kuwa sumu ambayo itaenda kumdhuru mtu huyo, madhara ya