NAFASI ZA KAZI YA UWAKALA WA USAMBAZAJI VITABU
Neema Herbalist & Nutritional Foods Clinic ni wauzaji wa dawa za asili kutoka Tanzania. Pia ni waratibu wa Mradi wa Vitabu Vya Elimu Ya Tiba Mbadala. “ MRAVIETI”. Mradi uliolenga katika kutoa elimu ya tiba ya ya asili kwa njia ya vitabu kuhusu magonjwa mbalimbali yanayo wakabili wanadamu.
Kupitia Mradi huu, tunatangaza nafasi za kazi ya uwakala wa usambazaji vitabu vyetu katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.
SIFA ZA MWOMBAJI
1. Umri miaka 18 hadi 45.
2. Elimu kuanzia kidato cha nne, sita na kuendelea.
3. Awe raia wa Tanzania.
4. Uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha kwa lugha za Kiswahili na kiingereza.
5. Awe maridadi na anaye jituma sana kazini.
6. Akiwa na uzoefu na masuala ya usambazaji vitabu itakuwa ni sifa ya ziada itakayo muongezea nafasi ya kupata kazi katika mradi huu.
Tuma barua yako ya maombi ukiambatanisha na CV yako kwenda kwa :
Managing Director,
Neema Herbalist & Nutritional Foods Clinic
P.O.Box 35967
Changanyikeni Street,
Dar Es Salaam.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 21 Februari 2012.
Mradi kuanza tarehe 01 Machi 2012
Tunapokea maombi kutoka kwa waombaji waliopo katika wilaya zote za Tanzania Bara Na Visiwani.
Au wasiliana nasi kwa simu :
Comments
Post a Comment