Kutokwa na kinyama ama uvimbe kwenye sehemu ya haja kubwa ni tatizo linalo wakabili maelfu ya watu duniani. Tatizo hujulikana kwa Kiswahili kama Bwaziri, katika lugha ya kisukuma na kinyamwezi huitwa “Man’gondi” na katika lugha ya kiingereza hujulikana kama Hemorrhoids. Mti wa ufwambo Tunda la mti wa ufwambo. AINA ZA BAWAZIRI : Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kitaalamu, zipo bawaziri za aina mbili, bawaziri ya ndani na bawaziri ya nje. Kwa kawaida mtu huweza kuwa na moja wapo kati ya aina hizo na wakati mwingine, mtu mmoja anaweza k...