Skip to main content

JIKINGE NA KANSA KWA VYAKULA VYA ASILI

Nyanya
Kitunguu  Saumu
Brokolini
Beri
Kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  duniani, ugonjwa  wa  kansa  unatajwa  kuwa  ndio  ugonjwa  wa  hatari  zaidi  pengine  kuliko  ugonjwa  mwingine  wowote  uliowahi  kutokea  katika  historia  ya  mwanadamu.   Nchini   Tanzania  pekee  kiasi cha watu 100 hufariki dunia KILA SIKU kutokana na magonjwa ya saratani, hii  ni  kwa  mujibu  wa  taarifa  ya  Taasisi  ya  Saratani  ya  Hospitali  ya  Ocean  Road a  jijini  Dar  es  salaam  kupitia  Mkurugenzi  wake  Dk. Twalib  Ngoma.

Hali i  mbaya  zaidi katika  nchi  zilizoendelea   ambako  tunataarifiwa  ya  kwamba   kuna  idadi  kubwa  sana  ya  watu  wanaopoteza  maisha  yao  kila  siku  kutokana  na  magonjwa  ya  kansa ambayo  kimsingi  yanasababishwa  na  na ulaji wa vyakula tunavyokula kila siku. Mfano  nchini  Marekani  pekee  karibu  theluthi  moja  ya  wagonjwa  wa  kansa  inasababishwa  na  vyakula  wanavyokula  kila  siku, na  hii  ni  kwa  mujibu  wa Taasisi  ya  Saratani  ya  nchini  Marekani.
Pamoja na kuwepo habari hiyo mbaya na ya kusikitisha ya kupoteza mamia ya ndugu zetu kila siku, kuna habari njema pia kuwa unaweza kabisa kujikinga na ugonjwa huu hatari kwa kula vyakula vinavyostahili na kuepuka vinavyochangia saratani.
Kwa leo hebu tuangalie orodha ya baadhi ya vyakula ambavyo vinaaminika kuwa na uwezo mkubwa wa kupambana na seli zinazosababisha saratani mwilini. Mwenyekiti wa Taasisi ya Kuzuia na Kutibu Saratani, DK. Richard Béliveau wa Chuo Kikuu cha Québec, Montreal Canada, anasema kuwa tafiti zote zinaonesha kuwa kinga ya saratani iko kwenye ulaji wa vyakula vitokanavyo na mimea (Plant-based foods).
Unachotakiwa kufanya ili kuupa mwili wako kinga dhidi ya saratani, kula matunda na mboga za majani za aina mbalimbali kila siku, hasa hizi zifuatazo:
BROKOLI (BROCCOLI)Hii ni ana fulani ya mboga ya majani, iko kama maua ya maboga au uyoga, inapatikana katika masoko mengi makubwa nchini. Aina hii ya mboga inaelezwa kuwa na kiasi kingi cha kirutubisho aina ya ‘sulforaphane’ ambacho uwezo wake wa kutoa kinga ni mkubwa. Inatoa kinga dhidi ya saratani ya matiti, ini, mapafu, kibofu, ngozi, tumbo na kizazi.
BERI (BERRIES)Haya ni matunda maarufu ambayo hujulikana pia kama matunda ya kuongeza damu au ‘matunda damu’ kutokana na kuwa na rangi nyekundu na mengine meusi na kijani. Ulaji wa matunda haya hutoa kinga dhidi ya saratani ya utumbo, koo, mdomo na ngozi.
NYANYA (TOMATOES)Wengi tunaidharau nyanya na kuipuuzia kwa kutoila katika milo yetu ya kila siku, wakati nyanya ziko nyingi kiasi zingine zinaoza mitaani. Nyanya inaelezwa kuwa na kirutubisho aina ya ‘Lycopene’ ambacho kina uwezo mkubwa wa kuzuia saratani ya kizazi ambayo nchini Marekani inaua zaidi ya watu 8,000 kila mwaka, kwa Tanzania hali ni mbaya zaidi. Nyanya huzuia pia saratani ya mapafu, tumbo na kibofu.
KITUNGUU SAUMU (GARLIC)Faida za kitunguu saumu zipo nyingi, lakini miongoni mwa hizo faida ni kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani. Kwa kuweka mazoea ya kula mara kwa mara, kwa kuchanganya katika mlo wako au saladi yako utakuwa umejijengea kinga mwilini. Hutoa kinga dhidi ya saratani ya utumbo, matita, koo na tumbo kwa ujumla.
MAHARAGE (BEANS)Wengi wetu hatupendi kula maharage tukiamini ni mboga ya kimaskini! Ukweli ni kwamba maharage ni mboga muhimu na ina faida nyingi mwilini, ikiwemo kutoa kinga dhidi ya saratani ya utumbo na matiti. Utafiti kuhusu faida za maharage uliofanywa na Chuo Kikuu cha Michigan nchini Marekani umethibitisha faida hizo.
Kwa ujumla, magonjwa ya saratani yanaweza kuepukwa iwapo mtu atazingatia ulaji wa mboga na matunda asilia kila siku na kujiepusha na ulaji wa vyakula vya ‘kutengeneza’. Wiki ijayo nitakuletea orodha ya vyakula vinavyosababisha saratani ambavyo unatakiwa kuviepuka kama ukoma!

MAKALA  HAYA  YAMEANDALIWA  NA  NEEMA  HERBALIST   KUTOKA  KATIKA  VYANZO  MBALIMBALI  VYA  HABARI  NA  MASHIRIKA  YA  AFYA  DUNIANI.

Comments

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ...

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na...

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS

Dawa ya TONSILS ni (kugargar)  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto. Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia. Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako. Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafany...