Skip to main content

Kolesteroli na namna iwezavyo kudhibitiwa bila dawa:

Karibu nusu ya watu wazima nchini Marekani wanatatizwa na kolesteroli.

Kwa kusikia tu sentensi ‘’Una kolesteroli iliyozidi’’ toka kwa daktari kunaweza kumfanya mtu yeyote kuingiwa na hofu. Hata hivyo, linapokuja suala la kuishi, kila mmoja angependa kuishi maisha marefu na yenye furaha na hivyo kolesteroli inaweza kuwa kizingiti kwa hilo.

Kolesteroli au helemu ni nini? Ni dhahiri na rahisi kabisa, ni kama nta laini ambayo huelea katika damu na katika seli zako zote za mwili muda wote. 
Kwa baadhi ya watu kolesteroli ina mwelekeo wa kujilundika kwenye ateri karibu na moyo au shingoni. Ikiwa mkusanyiko huu wa kolesteroli unaendelea kuwa mwingi kiasi cha kuanza kuzifunga ateri, huweza kusababisha mishtuko au shambulio la moyo (heart attack).

Ukweli ni kuwa kolesteroli si mojawapo ya vitu ambavyo watu hupenda kujichunguza. Isitoshe mwili unaitengeneza kila siku ili kwamba unaweza kufurahi kuwa mzima. Ubongo umetengenezwa kwa kolesteroli, homoni zako zimetengenezwa kwa kolesteroli na hata neva zako zimefunikwa na kolesteroli (myelin sheaths). Bila kolesteroli huwezi kuishi.

Ikiwa kolesteroli ni kitu kibaya sana, kwanini Ini lako huizarisha kwa wingi kiasi hicho?:

Asilimia 75 ya kolesteroli katika damu hutengenezwa na Ini. Asilimia nyingine 25 hutujia toka kwa kile tunachokula. Kadiri ulavyo kolesteroli nyingi, ndivyo na Ini huitengeneza chache ili kukuweka wa furaha. Ini lako linatengeneza wastani wa mg 900 kwa siku. Kwa wastani, watu hula mpaka mg 300 za kolesteroli kwa siku. Ukichanganya pamoja, mtu wa kawaida ana mg 1200 za kolesteroli katika mfumo wake wakati wowote.

Kwanini katika maisha Ini letu litakuwa linatengeneza mg 900 za kolesteroli kila siku huku tunaambiwa chochote zaidi ya mg 200 ni hatari?, tunaweza kusema tu haileti maana (Nonesense).

Unapokula chakula chochote chenye kolesteroli, kolesteroli lazima iende kwanza katika kuta za tumbo kwa ajili ya kuingia kwenye mkondo wa damu.
Cha kushangaza ni kuwa tumbo (intestine) lina uwezo mdogo sana wa kuimeng’enya kolesteroli unayokula. Katika hali hii mwili wako ndio hasa hukulinda usipate kolesteroli nyingi kupitia chakula ulacho. Ikiwa itatokea umekula chakula ambacho kina kolesteroli nyingi, sehemu kubwa ya kolesteroli itatoka nje wakati unapata choo.

Hautapata ishara yeyote ya onyo kwamba una kolesteroli iliyozidi. Namna moja ya kutambua kwa hakika ni kufanya kipimo kiitwacho “lipoprotein profile” . kipimo hiki kitaonesha jumla ya kolesteroli uliyonayo, HDL cholesterol, LDL cholesterol na usawa wa triglyceride. Kipimo hufanyika baada ya kufunga masaa tisa mpaka kumi na mbili bila chakula, kimiminika au dawa.

Katika miaka ya 1970 kiasi kilichokuwa kinakubalika kama cha kawaida cha kolesteroli mwilini kwa mtu chini ya miaka 30 kilikuwa mg 120 mpaka 290 huku ikikubalika 150 mpaka 340 kwa mtu wa miaka zaidi ya 40.

Kwa mjibu wa viwango vinavyokubalika sasa, ikiwa majibu ya kipimo cha “lipoprotein (protini inapochanganyana na mafuta) profile” yanaangukia katika usawa ufuatao, utachukuliwa kama huna tatizo na hutakiwi kuwa na wasiwasi juu ya hilo:

  • Jumla ya kolesteroli: chini ya 200 mg/dl
  • Msongamano wa juu wa lipoprotini kolesteroli: zaidi ya 40 mg/dl
  • Msongamano wa chini wa lipoprotini kolesteroli: kati ya 100-129 mg/dl
  • Triglycerides: chini ya 150 mg/dl

Umeona tofauti kubwa ya kiasi cha kolesteroli iliyokuwa inakubalika 1970 na ile inayokubalika siku hizi?.  Kwanini kiasi hiki kilipunguzwa?
Ni watu milioni ngapi zaidi wanatumia dawa za kupungunguza/kudhibiti kolesteroli siku hizi kwa sababu kiasi kilichokuwa kinakubalika kilipunguzwa na kwa gharama gani?.

Kwa mjibu wa William Campbell Douglass, M.D., ambaye amekuwa akitibu watu wenye kolesteroli duniani kote kwa zaidi ya miaka arobaini sasa, ikiwa jumla ya kolesteroli yako ni kati ya 200 na 300 na unatumia chakula safi chenye wanga mchache, usijisumbuwe kuwaza kuhusu kolesteroli.

Edward R. Pinckney, M.D. katika kitabu chake “The Cholesterol Controversy” anatuambia kwamba watu waliolazimishwa kupunguza kiasi chao cha kolesteroli kwa sababu wameonekana kuwa na shambulio la moyo walijikuta wakitokewa kupatwa na shambulio jingine la moyo kuliko wale walioendelea kula kawaida bila kuzidisha.

Je kutoa damu kunaweza kusababisha kiasi chako cha kolesteroli kupanda ju?:

Amini usiamini, kwa baadhi ya watu, wazo tu la kutoa damu linaweza pelekea kolesteroli zao kupanda juu mpaka 400 hata kama hawana tatizo na kolesteroli kwa ujumla.

Tuchukulie mfano umefadhaishwa kiasi kidogo tu kwa kupimwa kiasi cha kolesteroli – labda kwa sababu ya kushikiwa tu sindano juu ya mkono wako kunakuudhi au kwa sababu tayari unahofu kupima kiasi cha kolesteroli ulichonacho kinachoelea katika mkondo wako wa damu kunaweza kumaanisha una ugonjwa wa moyo – hivyo majibu ya kiasi cha kolesteroli yatakayopatikana ukiwa katika hali hii yanaweza kuwa si ya kweli kwa karibu ya asilimia 100.

Wakati unaweza kuwa tu na kolesteroli ya kiasi cha 180 mg ambacho kinachukuliwa kuwa ni cha kawaida, hofu, wasiwasi au woga vyaweza pelekea kupanda kwa kiasi cha kolesteroli na majibu ya maabara yanaweza kutoka na 360 mg kiasi kinachotosha kukufanya wewe (pengine hata daktari wako) kuanza mzunguko usioisha (vicious cycle) kutibu ugonjwa wa moyo kwa madawa.

''Tangu mwaka 1936, utafiti baada ya utafiti umeonesha
hakuna uhusiano kati ya kolesteroli na ugonjwa wa moyo.''


Utafiti wa kwanza kuhusu kolesteroli na ujikusanyikaji wake katika ateri (atherosclerosis) umewahi kuchapishwa 1936. majibu ya mwisho yalionesha kuwa hakukuwa na uhusiano kabisa kati ya kiasi cha kolesteroli katika damu na dipositi za kolesteroli katika ateri.

Utafiti mwingine mwaka 1963 ukihusisha askari wastaafu 800 (wa Marekani) juu ya miaka 60, ulionesha kwamba ateri za waliokuwa na kolesteroli chache hazikuwa na tofauti na za wale wenye kolesteroli kuzidi.

Dr. Michael DeBakey mtaalamu maarufu mmarekani katika masuala ya upasuaji wa moyo na timu yake ya utafiti walitafiti waathirika 1700 wenye ateri zilizozibika au kukazika (arteriosclerosis). Nane kati ya kumi ya waathirika hawa walikutwa na kolesteroli ya kawaida inayokubalika kwa wamarekani.

Dr. William P. Catelli, mkurugenzi wa utafiti maarufu wa Framingham study, ambaye ametafiti sababu zote zinazoweza pelekea ateri kuzibika au kukazika na ugonjwa wa moyo, alitamka kwa mara ya kwanza katika historia mwaka 1992 kwamba....

“….ndani ya Framingham, wengi wa watu, kadiri walivyokula mafuta yatokanayo na wanyama (saturated fat) ndivyo walivyopata kolesteroli nyingi, na ndivyo watu hao walipata kuwa na kalori/nishati nyingi, na ndivyo watu hao walivyokutwa na damu chache yenye kolesteroli…”  !!!
Anaendelea...

“Tulipata kujuwa kuwa watu waliokuwa wakila vyakula vyenye kolesteroli nyingi, walikula kolesteroli itokanayo na wanyama (saturated fat), walikutwa na kalori nyingi, uzito wa wastani na walikuwa na miili yenye nguvu (physically active.)”


Hadithi tisa kuhusu kolesteroli:

  • Vyakula vyenye mafuta mengi husababisha ugonjwa wa moyo.
  • Kolesteroli nyingi husababisha ugonjwa wa moyo.
  • Vyakula vyenye mafuta mengi hupandisha kolesteroli kwenye damu.
  • Kolesteroli huziba ateri
  • Utafiti kwa wanyama unathibitisha wazo la lishe kwa ajili ya moyo.
  • Kupunguza kolesteroli yako kunaongeza urefu wa kuishi.
  • Mafuta yatokanayo na mbogamboga (Polyunsaturated) ni bora kwa afya yako.
  • Kampeni dhidi ya kolesteroli imeegemea katika sayansi chanya/ukweli.
  • Wanasayansi wote wanaunga mkono lishe yenye kolesteroli chache ili kulinda moyo.


Hadithi zote tisa hapo juu zimethibitishwa kuwa si za kweli na zimeelezewa kwa kina zaidi katika kitabu: “The Cholesterol Myths” kilichoandikwa na Uffe Ravnskov, MD, PhD. Kitabu kizuri kwa anayependa kujifunza ukweli kuhusu kolesteroli.

Zifuatazo ni baadhi ya kweli:
  • Watu wenye kolesteroli chache hutokewa pia na kuzibika au kukazika kwa ateri (atherosclerotic) kama ilivyo kwa watu wenye kolesteroli kuzidi.
  • Watu wazee wenye kolesteroli nyingi huishi miaka mingi.
  • Kolesteroli nyingi hukukinga dhidi ya magonjwa ya kuambukizana (infectious diseases).

Alipoulizwa ikiwa mafuta yatokanayo na wanyama (saturated fats) husababisha ugonjwa wa moyo, Mary G. Enig, MD PhD, alijibu:  “Wazo kwamba mafuta yatokanayo na wanyama husababisha ugonjwa wa moyo halina ukweli hata kidogo, lakini taarifa hizo zimechapishwa mara nyingi zaidi katika miongo mitatu au zaidi iliyopita kiasi kwamba ni vigumu kuwashawishi watu tofauti labda kama wapo tayari kuchukuwa muda kusoma na kujifunza sababu za kiuchumi na kisiasa zilizotengeneza ajenda dhidi ya mafuta yatokanayo na wanyama (anti-saturated-fat agenda).”




Triglycerides na Trans fats:


Kitu kingine unachohitaji kuwa makini nacho ni triglycerides. Trglcerides (mafuta yapatikanayo katika damu) yanaweza kuchangia kutika kukazika kwa ateri (atherosclerosis) au kuzifanya ateri kuwa na kuta zenye maki kubwa jambo linaloweza pelekea kuongezeka kwa hatari ya kupatwa na shambulio la moyo, ugonjwa wa moyo, mishtuko au kisukari.

Triglycerides ni aina ya mafuta yapatikanayo katika damu yako. Wakati unakula, mwili wako hubadilisha kalori yeyote ambayo haina matumizi nayo muda huo na kuwa triglycerides na kuihifadhi katika seli zako za mafuta. Baadaye, wakati mwili unahitaji diseli ili kutembea, utayatumia mafuta hayo yanayohifadhiwa katika damu (triglycerides) ili kuzarisha nguvu.

Ikiwa unazoea kula chakula kuzidi ya ulivyopaswa na haujishughulishi kutembea kwa miguu au kufanya mazoezi japo kidogo na kukaa tu muda wote ukiangalia televisheni muda wote, inaweza kukutokea kuwa na usawa uliozidi wa triglyceride.

Linapokuja suala la aina za mafuta katika lishe zako, unajitahidi kukwepa mafuta magumu/ya mgando (trans fats) kwa gharama zozote .

mwaka 1958, Ancel Keys, ambaye alisomea magonjwa yahusianayo na moyo, alikuwa mmoja wa watu wa mwanzo kuandika kuwa mafuta yatokanayo na mboga mboga yaliyoongezwa haidrojeni (hydrogenated vegetable oils) na mafuta yake magumu/mazito (trans fatty acids) ndio wahusika wakuu katika kutengeneza ugonjwa wa moyo.

Yanachofanya mafuta haya:
  • Yanashusha msongamano wako wa juu wa lipoprotini (HDL) kolesteroli.
  • Yanapandisha msongamano wako wa chini wa lipoprotini (LDL) Kolesteroli
  • Yanaweza kuupandisha usawa usawa wako wa triglyceride
  • Yanaweza kuharakisha pumu/asthma za utotoni

Badala ya kukupatia afya, trans fats yanakusaidia kukusogeza hatua moja zaidi karibu na kaburi.

Ni mafuta gani hayo? Trans fats (transifatsi) ni mafuta yanayotengenezwa kwa kuchanganya haidrojeni na mafuta yatokanayo na mboga mboga kupitia mbinu iitwayo ‘’hydrogenation’’.  Trans fats huwa ni magumu (kama mafuta ya mgando) zaidi ya mafuta mepesi jambo linalosaidia yasiharibike haraka.

Kwahiyo, utakapoenda nje tena kufanya manunuzi ya chakula, tafadhari soma vibandiko vya bidhaa (labels). Ikiwa utasoma kibandiko chenye neno ‘’hydrogenated’’ sehemu yeyote, fikiria mara mbili kabla hujanunua.

Mwishoni mwa miaka ya tisini (1990) tafiti katika mishtuko ya moyo zilionesha watu waliokuwa wanapendelea zaidi mafuta yatokanayo na mboga mboga (polyunsaturated fats) walikuwa na uwezekano zaidi wa kupatwa na mishtuko ya moyo (strokes), na kupungukiwa usawa wa mafuta yatokanayo na wanyama (saturated fats). Iliripotiwa pia kuwa watu wa rika la juu waliokuwa na usawa wa kolesteroli chini ya mg 200 katika damu walikuwa na hatari kubwa zaidi ya kupatwa na mishtuko ya moyo.

Ikiwa una mojawapo ya hali hatarishi zifuatazo, unaweza kuwa kandideti wa kolesteroli kuzidi:
  • Lishe duni: kutumia vyakula pekee vyenye mafuta ya mboga mboga, kutumia mafuta yaliyochanganywa na haidrojeni na kutumia trans fats
  • Usawa uliozidi wa triglyceride mwilini
  • Ukosefu wa mazoezi: Mazoezi husaidia kuuongeza msongamano wako wa juu wa lipoprotini (kolesteroli nzuri) huku yakishusha msongamano wako wa chini wa lipoprotini (kolesteroli mbaya)..
  • Shinikizo la juu la damu: kuongezeka kwa presha katika kuta zako za ateri huharibu ateri zako jambo linaloweza kuongeza spidi ujikusanyikaji wa dipositi za mafuta

Kolesteroli huokoa maisha yetu: 

Nini ungefanya ikikutokea umeanguka na kujichubua goti vibaya? Kwanza utaliosha goti vizuri kwa maji kisha utapaka mafuta kidogo na kufunika na bandeji. Baada ya siku kadhaa, utaitoa bandeji na goti litaonekana kama halijawahi kupatwa na mchubuko wowote.  Ndiyo, mwili wako unao uwezo wa kutenda kama wewe ulivyotenda na bandeji.

Dr. Batmanghelidj anasema damu yenye asidi inayotokea mapafuni inaweza kuelea mpaka kwenye moyo. Wakati damu hii yenye asidi inapoondoka katika moyo wako huanza kuvuta maji nje ya seli zinazozunguka ateri zako na kusababisha michubuko midogo midogo (microscopic abrasions) na machozi.

Hii michubuko midogo midogo na machozi katika ateri ni kama mchubuko ulioupata ulipojikwaa na kuanguka kama tulivyoona hapo juu. Mwili wako sasa utatumia hayo ‘’mafuta’’ kama bandeji isiyopitika maji (water proof bandage) yaani Kolesteroli ili kuzifunika seli zinazozunguka ateri.
Kwa watu wenye afya zao, miili yao sasa itaiita kinga ya mwili kwenda katika ‘’bandeji’’ hiyo (kolesteroli) na kuanza kuliripea tatizo na mwishowe kuiondoa bandeji ya kolesteroli.
Ndiyo, mwili wako unao uwezo wa kujiripea wenyewe. Isitoshe mchubuko ule kwenye goti lako ulipona, au siyo?.

Ni kweli, kama hautabadili tabia katika lishe na staili za maisha yako, mwili kamwe hautapata nafasi ya kujiripea wenyewe. Kolesteroli zaidi na zaidi itatupwa juu ya hii michubuko na pengine kukupatia mapigo au shambulio la moyo katika siku za baadaye.

Kama miili yetu haitengenezi kolesteroli kufunika michubuko ambayo hujitokeza katika ateri kwa baadhi yetu, hatimaye michubuko hiyo midogo midogo (microscopic abrasions) huendelea kuwa mikubwa na yenye kina kiasi cha ateri kuachana wazi na kusababisha kifo cha ghafla.

Dr Batmanghelidj anasema katika vitabu vyake nilivyosoma: “kama tunaupatia mwili maji yake ya mhimu kabla ya kula chakula, mapigano yote dhidi ya uundwaji wa kolesteroli katika mishipa ya damu yatakuwa yameonywa.”

Kwanini?….kwa sababu kwa kunywa maji halisi pamoja na kiasi kidogo cha chumvi nusu saa kabla ya chakula, seli ndani ya mwili zitakuwa zimefanikiwa kujazwa maji (hydrated). Mwili wako hautahitaji kuvuta maji toka katika ateri zako kusaidia kumeng’enya chakula.
Fanya hivi kila siku na damu yako haitakuwa ikijikusanya tena (concentrate), kwahiyo haitaendelea kuvuta maji toka katika seli kuzunguka kuta za ateri jambo litakalokomesha kujitokeza kwa michubuko midogo midogo.
Zoezi hili (la kunywa maji kabla ya kula) litazuia dipositi za kolesteroli kujikusanya katika ateri zako. Hatimaye, baada ya muda, dipositi hizi za kolesteroli zitapotea labda kama zitakuwa zimeshaunguzwa (calcified).

Mazoezi, Mazoezi, Mazoezi:

Wakati mmoja Dr. Batman alikutana na bwana mmoja mwenye rika la miaka arobaini hivi akisumbuliwa na kuzibika kiasi ateri zake ziendazo katika moyo, jambo lililokuwa likimsababishia maumivu ya kifua.
Bwana huyo alikuwa afanyiwe upasuwaji, lakini Dr Batman akamshauri kujaribu tiba mubadala kabla ya kujaribu kujiingiza katika upasuwaji kuona kama ingemsaidia. Bwana huyo alikubali na akanza kurekebisha unywaji wake wa maji na utumiaji wa chumvi na akaanza kunywa maji kila nusu saa kabla ya kila mlo. Pia akaanza kutembea kwa miguu dakika ishirini mpaka therathini asubuhi na jioni (akiongeza dakika kidogo kidogo mpaka lisaa limoja). .

Miezi mitatu baadaye, mtu huyo akaenda kufanya vipimo vyake vya mwisho kuona kama bado anahitaji kuhamia kufanya upasuwaji. Vipimo vya maumivu kifuani (angiogram test) havikuonesha ishara yeyote ya kuzibika kwa ateri. Hakuwa anahitaji tena upasuwaji.

Tunazaliwa na miguu ili kutembea. Mazoezi ni kutembea na kutembea ni afya bora. Ikiwa unaweza kutembea tu dakika tano, anzia hapo. Unatakiwa tu kuongeza tu dakika tano kila siku asubuhi na jioni mpaka utakapoweza kutembea lisaa lizima kwa pamoja asubuhi na jioni. Kutembea ni jambo jema kwa mifupa yako, mzunguko wa damu, kolesteroli na kudhibiti mafuta kuzidi.


Swali: Ni sehemu gani mwilini ambako sehemu kubwa ya kuzibika kwa ateri sababu ya kolesteroli hutokea?.

Jibu: Katika ateri karibu na moyo wako na katika ateri zilizopo shingoni mwako.

Tumeambiwa kuwa ni ‘’usawa wa kolesteroli’’ katika damu zetu ambao husababisha dipositi za kolesteroli ndiyo husababisha mapigo na shambulio la moyo.

Swali: Unapofanyiwa vipimo vya usawa wa kolesteroli, kwa kawaida sampuli ya damu hutolewa toka kwenye veini katika mkono wako.
Ikiwa ni kweli ni ‘’usawa wa kolesteroli’’ katika damu yako ndiyo unaoweza kusema iwapo upo katika hatari ya kuwa na ugonjwa wa moyo, kwanini sasa hakujawahi kuwa na rekodi ya kuzibika kwa veini au kapilari?... Kwa sababu damu huelea kupitia ‘’veini na kapilari’’ hizi ndogo taratibu zaidi kuliko katika ateri, siyo tulipaswa kupata kuzibika kwa veini na kapilari kabla hatujapatwa na kuzibika kwa ateri?.

Jibu: Muulize Daktari wako…….lakini ikiwa tu unahitaji kukodolewa naye macho!


Mwanga wa jua husaidia kushusha usawa wa kolestroli:

Je wajuwa kuwa mwanga wa jua huibadilisha kolesteroli iliyomo kwenye damu yako na kuwa vitamini D?.
Maana yake ni kuwa unaweza kuipunguza kolesteroli yako kwa kutembea nje katika mwanga wa jua. Kwanza, unahitaji kuuweka mwili wako zaidi kadili iwezekanavyo moja kwa moja katika miale ya jua. Usipake chochote juu ya ngozi (sunscreen) kuzuia ukali wa mwanga wa jua, kwani nyingi ya hizo zimetajwa kuwa na kemikali zinazosadikika kusababisha kansa na zinazuia miale yote ya jua kuingia mwilini.

Kiasi gani hasa cha jua?:

Jua la kutosha kuweza kufanya ngozi yako kuwa ya uwaridi hivi. Unapofikia hali hii ya uwaridi, mwili wako hautaweza kuendelea kutengeneza vitamini D. Ukiendelea kubaki juani baada ya ngozi kufikia hali hii utakuwa unaenda kuleta madhara tu katika ngozi yako.
Mimi kwa kawaida hutoa kabisa shati na kubaki nakaptula na ndipo naanza kuzunguka juani mpaka nichoke (huwa porini lakini).

Kwa hakika kabisa unaweza kuzarisha mpaka uniti 20,000 za vitamini D kwa siku kupitia staili hii ya kujianika juani. Hata hivyo, hauhitaji kujishughurisha sana na kiasi gani cha vitamini D unatengeneza kwani ngozi yako inayo majibu ambayo yatafunga uzarishaji wa vitamini D ukifikia hatua ya uwaridi.
Kadili unavyopata usawa mahususi wa kolesteroli katika mwili wako utakuwa pia ukitengeneza vitamini D chache kwa kawaida, kwa hiyo hakutakuwa kamwe na hatari ya kuzidisha dozi ya kupata vitamini D yako toka katika jua.

Mstari mmoja wa habari, kukaa nyuma ya dirisha au kupaka chochote kuzuia mwanga wa jua usikukute moja kwa moja katika ngozi yako, vitaizuia miale ya jua (ultraviolet-B) kuweza kugonga juu ya ngozi yako na hivyo kushindikana kwa kolesteroli kuwa vitamini D.

MAKALA HAYA  YANATOKA :  WWW.  MAAJABUYAMAJI.NET

Comments

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ...

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na...

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS

Dawa ya TONSILS ni (kugargar)  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto. Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia. Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako. Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafany...