Tangawizi ina
faida nyingi sana kwa mwili wa
mwanadamu. Baadhi ya faida hizo ni kama
ifuatavyo :
1. Kutibu kutokusagika kwa chakula
tumboni,.
2. Kutibu tatizo la gesi
tumboni
3. Kuondoa tatizo la
msokoto wa tumbo (bila kuharisha)
4. Husaidia kuzuia
kutapika.
5. Mshtuko/Mkazo wa ghafula (wa
msuli),
6. Maumivu ya tumbo na Kibofu cha
mkojo ikiambatana na Homa, Mafua, Kukohoa na Pumu.
JAM YA
TANGAWIZI.
Unaweza kutumia Jam
ya Tangawizi kujitibu magonjwa mbalimbali
kama ilivyo onyeshwa hapo juu.
JINSI YA KUTENGENEZA JAM YA
TANGAWIZI.
Kamua TANGAWIZI mbichi
kisha changanya maji yake (Juice) na Sukari. Chemsha mpaka mchanganyiko huo uwe
mzito. Ongeza Zafarani iliyosagwa,Iliki iliyosagwa, Kungumanga zilizosagwa na
karafuu iliosagwa. Iweke dawa hii vizuri na tumia inapo hitajika.
MUONGOZO WA KUJITIBU MAGONJWA
MBALIMBALI KWA KUTUMIA TANGAWIZI.
Unaweza kujitibu
magonjwa mbalimbali kwa kutumia zao la
Tangawizi kwa kufuata maelekezo yafuatayo :
KUJITIBU TATIZO LA
KUVIMBIWA NA KUKOSA HAMU YA KULA.
Changanya Juice ya TANGAWIZI, Juice
ya Limau na Chumvi Mawe kwa vipimo vilivyo sawa. Hakikisha umechanganya vizuri.
Kunywa dawa hii kabla ya Chakula.
Vingineyo changanya vipimo vilivyo
sawa sawa vya Juice ya TANGAWIZI na Sukari Mawe. Koroga vizuri, kunywa kabla ya
kula chakula. Dawa hii husafisha Ulimi na Koo na hukuongeza hamu ya kula na
kukufanya mchangamfu.
KUJITIBU TATIZO LA
MAUMIVU YA KUKOO NA KUKAUKA SAUTI
Tafuna vipande vidogo vya Tangawizi.
KUJITIBU TATIZO
LA KUHARISHA.
Chua sehemu zinazozunguka kitovu kwa
Juice ya Tangawizi.
KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA
Kunywa mchanganyiko wa Juice ya
Tangawizi na Juice ya Kitunguu.
MAUMIVU YA KICHWA CHA WASIWASI
Changanya Juice ya Tangawizi na
Maziwa, kisha kausha. Nusa unga huo kama Tumbaku.
MAUMIVU MAKALI YA TUMBO
Changanya kijiko kimoja cha au
viwili vya Tangawizi iliyosagwa na kijiko kimoja au viwili vya mafuta ya
Kastoroli. Kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa siku.
BARIDI YABISI SUGU
Changanya kijiko kimoja cha
Tangawizi ya unga na vijiko 24 vya maji kunywa mchanganyiko huu ukiwa vuguvugu.
Ulale na ujifunike mpaka utoe jasho.
KUUMWA JINO NA MAUMIVU YA KICHWA
Chukua Tangawizi ya Unga koroga na
maji kidogo iwe nzito kama tope. Jipake na uchue kwenye paji lako la uso kabla
ya kulala. Kwa Jino jipake na uchuwe kwenye Shavu.
Kwa
maelezo zaidi kuhusu tiba zetu , wasiliana
nasi kwa simu 0767010756 au 0766538384
Comments
Post a Comment