Katika makala iliyopita, tumeufahamu kwa undani ugonjwa wa pumu, makala haya yanaelezea tiba lishe ya ugonjwa wa pumu. Zipo aina mbalimbali za lishe zinazo weza kutumika kama tiba ya ugonjwa wa pumu, leo tutaanza na aina ya kwanza.
TIBA LISHE YA UGONJWA WA PUMU
Baadhi ya vyakula vinavyoaminika kutoa ahueni na kuwa kama tiba kwa mgonjwa wa pumu ni pamoja na asali, juisi ya limau, mchanganyiko wa vitunguu swaumu na maziwa na mchangayiko wa mdalasini pamoja na asali. Vyakula hivyo vikiwa sehemu ya mlo wa mgonjwa kila siku, atapata ahueni ya ajabu.Pamoja na kuepuka ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi, mgonjwa wa pumu anatakiwa pia kula kwa kiasi kidogo mlo wenye matunda, mboga za majani na vyakula vingine vitokanavyo na nafaka ambavyo hutoa ‘alikalaini’.
Aidha, wagonjwa wa pumu wanatakiwa kujiepusha na ulaji wa kiasi kikubwa cha wali, sukari, mtindi (yoghurt), unywaji mwingi wa chai, kahawa, pombe na vyakula vote vya kusindika au kwenye makopo.Mgonjwa anashauriwa pia kufanya mazoezi ya kuvuta hewa safi na kuishi katika hali ya hewa isiyo na baridi, kunywa maji mengi mara kwa mara, kufunga kula (fasting) japo mara moja kwa wiki. Kwa kufuata masharti hayo, mgonjwa anaweza kuishi na pumu bila kusumbuliwa wala kutumia dawa kali kwa maisha yake yote.Pia unatakiwa kuepuka kufanya mazoezi kwenye baridi, epuka moshi wa sigara, dhibiti ugonjwa wa kucheua na kiungulia, epuka kukaa na wanyama na epuka kuishi katika mazingira yenye hewa yenye unyevunyevu.
KWA MAHITAJI YA DAWA YA ASILI INAYO TIBU UGONJWA WA PUMU, TAFADHALI FIKA KATIKA OFISI ZETU ZILIZOPO KATIKA ENEO LA CHANGANYIKENI KARIBU NA CHUO CHA TAKIWMU, AU PIGA SIMU 0767010756 AU 0753644583.
Comments
Post a Comment