Kitambi ni ile hali ya tumbo kuwa kubwa na kuchomoza kwa mbele na wakati mwingine kufikia hatua ya kunin’ginia. JINSI KITAMBI KINAVYO PATIKANA Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kitaalamu, mwili wa binadamu una seli kati ya bilioni 50 hadi 200 za mafuta zilizogawanyika katika sehemu mbalimbali za mwili wa binadamu. Kwa wanawake seli hizo zipo sana katika maeneo ya matiti, kwenye nyonga, kiunoni na kwenye makalio. Kwa upande wa wanaume seli hizo zinapatikana sana kwenye kifua, tumboni na kwenye makalio pia. Mafuta ya tumbo yanayofanya kitambi hukusanywa kwa njia kuu mbili: i. ...