Skip to main content

CHANZO, ATHARI NA TIBA ASILIA YA SARATANI YA NGOZI.






Leo tutachambua kwa undani saratani ya ngozi iitwayo Melanoma kwani saratani si tu kwamba ni ugonjwa hatari lakini pia ni ugonjwa unaompa mwanadamu mateso makali kutokana na maumivu anayoyapata.

Maumivu hayo huyapata mgonjwa bila kujali kama anaugua saratani ya ngozi, ya mifupa, damu, tumbo au ya kizazi. Shida ya maradhi haya ni kwamba matibabu yake yanahitaji gharama kubwa mno.

Melanoma ni saratani ya hatari sana kwa maisha ya mwanadamu inapotokea mtu akaipata, basi maisha yake yanakuwa hatarini. Saratani hii si rahisi kuigundua ukilinganisha na saratani nyingine za ngozi lakini pia husambaa haraka zaidi mwilini kuliko saratani nyingine za ngozi.

Melanoma huweza kusambaa na kushambulia viungo vingine zaidi ya ngozi kama mifupa na ubongo. Inapofikia hatua hii saratani hii inakuwa ngumu sana kutibika.

Dalili

Dalili za saratani hii zipo nyingi na ni vema kila mtu afahamu, mojawapo ni kubadilika kwa ukubwa, rangi au ule muundo wa alama ya ngozi ambayo mtu amekuwa nayo kwa muda mrefu au umezaliwa nayo. Alama hii ni ile ambayo ina rangi nyeusi zaidi ukilinganisha na maeneo mengine ya ngozi.

Mabadiliko haya si lazima yawe yanatokea haraka haraka yanaweza kuwa yanatokea taratibu, hivyo kila mwenye baka anatakiwa kujichunguza ili kuona kama kuna mabadiliko kwenye alama hiyo ya ngozi.

Ni muhimu sana kutambua mabadiliko haya. Mabadiliko mengine ni kama yafuatayo, alama hii inaweza kuwa inavimba, kingo zake zinapoteza mzingo wake wa kawaida, alama inakua zaidi kwa eneo kwa mfano kutoka mzingo wa 4 mm na kuwa kubwa na kuzidi 6 mm.

Dalili nyingine ni alama kuanza kuwasha na kama mgonjwa atachelewa kugundua tatizo basi zitajitokeza alama kwenye ngozi ambayo itapasuka na kuwa kidonda.

Alama hiyo baadaye inaweza ikawa inatoa damu na kuwa na maumivu. Kama matibabu hayatafanyika basi saratani hii husambaa na dalili zifuatazo huweza kuonekana :

Tezi za mwili za kwenye makwapa na kwenye nyonga huvimba, mgonjwa atatokwa na uvimbe kwenye ngozi, atapoteza uzito kwa kasi bila kujua sababu, atapata kikohozi kisichoisha, atapoteza fahamu au kupata kifafa, ataumwa kichwa kuuma.

Tiba

Kuna tiba nyingi za kitabibu, zilizogawanyika katika makundi mbalimbali. Kuna zile za hospitali ambazo ni lazima zinunuliwe, lakini kuna tiba ambazo kwa ushauri wa daktari hata wewe unaweza kuziandaa bila kutumia gharama kubwa.

Moja ya tiba hizo ni kunywa maji ya moto ambayo yanatibu magonjwa mengi ikiwemo figo, kutoa sumu mwilini, kuyeyusha mafuta tumboni, kurahisisha mzunguko wa damu, kuondoa sumu kwenye ubongo na kusafisha haja ndogo.

Kunywa maji ya moto kila unapotaka kwenda kufanya kazi ya nguvu au mazoezi iwe kama kinga na inashauriwa kila siku mtu anywe glasi nane ili kutoa taka na kila kisichotakiwa kubaki mwilini, kupitia jasho au mkojo.

Wadau wa afya wanasema kuwa ni vyema pia kunywa maji ya moto yenye ndimu au limao kabla ya kifungua kinywa ili kurahisisha mfumo wa mwili kwa siku nzima.

Maji yanarahisisha uyeyushaji wa chakula na mafuta mwilini, hivyo kutokana na umuhimu huo ni vyema kunywa maji ya moto yatakayofanya kazi haraka na kwa ufanisi mkubwa bila kuchosha figo.

Faida nyingine ya kunywa maji ya moto kuwa ni kutoa sumu zilizopo kwenye mishipa ya fahamu na kuisaidia figo kufanya kazi kikamilifu, tofauti na maji baridi ambayo yanagandisha na kuilazimisha figo kuyeyusha kwanza na kisha kuchuja.
Ushauri

Unashauriwa kunywa maji moto kabla ya kufanya mazoezi kwani huko ni kujiandaa kwa ajili ya kuchuja jasho ambalo litatoa sumu. Maji ya moto yakifika tumboni yanaanza kufanya kazi moja kwa moja, kuliko yakiwa ya baridi yanaweza kusumbua kwa kuwa ni lazima yapate joto la mwili kwanza kabla ya kuanza kufanya kazi.

Unywaji wa maji ya moto kabla ya mazoezi ni mzuri kwani mtu anakuwa kama amekula chakula. Kunywa maji ya baridi bila kuweka kitu tumboni na kwenda kufanya mazoezi kunaweza kusababisha tumbo kuuma au maji kucheza wakati wa kukimbia kama unafanya mazoezi ya kukimbia. Lakini yakiwa ya moto ni kama umekunywa chai au kula chakula cha kawaida.

Maji ya moto ni mazuri hata kwa kupata choo, kwa vile kinarahisisha uyeyushaji na uchambuaji wa kinachotakiwa na kisichotakiwa, wanaokunywa ya baridi wana uwezekanao mkubwa wa kupata haja kubwa kwa shida.

Ni vyema kunywa maji moto yaliyochemshwa na kuyaacha yapoe na kuwa vuguvugu na kuongeza limao na asali mbali na kuongeza ladha, asali na limao vina faida kiafya.
Kunywa maji ya uvuguvugu au ya moto ni vyema kwa kuwa hufanya kazi moja kwa moja kutokana na hali ya tumbo kuwa na joto muda wote.

Maji ni muhimu kwa mwili wako, yakiwa ya moto ni bora zaidi, kwa kuwa yanatoa rangi ya njano ya mkojo na kuufanya uwe msafi na wenye rangi angavu.
Ushauri ni kuwa ukiwa na alama yoyote mwilini inayokuwa kamuone daktari haraka.

Tiba

Tengeneza juisi ya kitunguu maji.Changanya na maziwa ya unga na unga wa kibiriti upele as-far robo ya kijiko cha chai(1.25ml).Changanya pamoja mpaka iwe krimu.

Pakaa sehemu yenye matatizo kutwa mara moja (1×1).Baada ya kuoga jioni pakaa na mafuta ya zaituni.

IMETAYARISHWA  NA  KITUO  CHA  TIBA  MBADALA  CHA  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC.
TUNAPATIKANA  JIJINI  DAR  ES  SALAAM  KWA  SIMU  NAMBA  0766538384.

Comments

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ya  kupata  wapenzi  wa  kike  ama  kuoa  na  wengine  huendelea  na  tabia  hiyo  hata  baada  ya  kuoa .  Zipo  sababu  mbalimbali  zinazo  wapelekea  wanaume  kupiga  punyeto, ila  kubwa  kati  ya  hizo  ni  pamoja  na  kutokuwa  na  wapenzi, kutokuwa  na  wapenzi  wanao  kidhi vigezo  vyao, kuwa  katika  mazingira  yasiyokuwa  na  wanawake  ( mfano  katika  shule  za  sekonda

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS

Dawa ya TONSILS ni (kugargar)  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto. Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia. Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako. Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafanya ka

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na  kuwa  mgumu  kama  msumari. Na  hatua  ya  pili   ni  lazima, uume  wake  uendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa  STRONGER  AND  LONGER  ERECTION JINSI  HATUA  ZA  KUSIMAMA  KWA  UUME  ZINAVYO  TOKEA. 1. HATUA    YA  KWANZA: DAMU  KUTIRIRIKA  KWA