KAMA UNA MOYO MDOGO, USIMUULIZE MKE WAKO SWALI KAMA HILI. MIMI NILIMUULIZA, ILA MAJIBU ALIYO NIPA, NAJUTA KWANINI NILIMUULIZA.
Mimi ni mwanaume mwenye umri wa miaka 45. Nipo kwenye ndoa kwa miaka 14 sasa. Mke wangu ana miaka 38. Mtaani kwetu kuna kijana mmoja ambaye kwa kumkadiria, umri wake ni kati ya miaka 25 na 28 hivi. Kijana huyu ana sifa moja hapo mtaani. Wanawake mbalimbali wakiwemo wake za watu wamekuwa wakimpigania na kumgombania na inasemekana huwa wanamhonga sana. Wiki tatu zilizo pita, mwanaume mmoja ambae anaishi kwenye nyumba moja ya kupanga na huyo kijana alimfukuza mke wake, kwa kosa la kumpa chakula huyo kijana. Habari zilizo enea mtaani...