NIMEKAA KWENYE NDOA KWA MIAKA KUMI BILA KUPATA MTOTO NDIO MAANA NIMEIBA MTOTO WA MWANAMKE MWENZANGU.
Jeshi la
polisi nchini Nigeria, katika jimbo
la Akwa Ibom, linamshikilia mwanamama Peace
Chukwuemeka kwa kosa
la kumuiba mtoto
mwenye umri wa
mwezi mmoja kutoka
kwa mama yake
mzazi.
Akihojiwa na
polisi, mwanamama huyo alinukuliwa
akisema “ Nimekuwa katika ndoa
kwa muda wa
miaka kumi bila
kupata mtoto. Nilichukua uamuzi wa
kumuiba mtoto huyo
ili na mimi
niwe na mtoto
wangu mwenyewe na hivyo kuepuka
manyanyaso kutoka kwa
mama yangu na
mume wangu.”
Akielezea jinsi
alivyo fanikiwa kumuiba mtoto
huyo kutoka kwa
mama yake, Peace alisema :
“ Sikumewekea dawa
wala kitu chochote, nilimkuta mama
wa mtoto akiwa amesinzia hivyo
nikatumia fursa hiyo
kumuiba mtoto na kumpeleka kijijini
kwa mama yangu lakini
mama angu alikataa
kumpokea, hivyo nikaamua kurudi
hapa mjini, ambapo mama
wa mtoto aliposikia
uwepo wangu akaanza kuniuliza
kuhusu mtoto na
kwenda kutoa taarifa
polisi na mwishowe nikakamatwa.
CHANZO
: VYOMBO MBALIMBALI VYA
HABARI NCHINI NIGERIA.
Comments
Post a Comment