Skip to main content

KAMA UNA MOYO MDOGO, USIMUULIZE MKE WAKO SWALI KAMA HILI. MIMI NILIMUULIZA, ILA MAJIBU ALIYO NIPA, NAJUTA KWANINI NILIMUULIZA.

Image result for african sad man images

Mimi  ni  mwanaume  mwenye  umri  wa  miaka  45. Nipo kwenye  ndoa  kwa  miaka  14  sasa. Mke  wangu  ana  miaka  38.

Mtaani  kwetu  kuna  kijana  mmoja  ambaye  kwa  kumkadiria, umri  wake  ni  kati  ya  miaka  25  na  28  hivi. Kijana  huyu  ana  sifa moja hapo  mtaani. Wanawake  mbalimbali  wakiwemo  wake  za  watu  wamekuwa wakimpigania  na kumgombania  na  inasemekana   huwa  wanamhonga  sana.

Wiki  tatu  zilizo pita,  mwanaume  mmoja ambae  anaishi  kwenye  nyumba  moja  ya  kupanga  na  huyo  kijana alimfukuza  mke  wake, kwa  kosa  la  kumpa  chakula  huyo  kijana.

 Habari  zilizo  enea  mtaani  kwetu  ni  kwamba,  mume  wa  mwanamke  huyo  alimfuma  mke  wake  akiwa  anampatia  kijana  huyo  plate  yenye  wali  nyama , jambo  ambalo  mume  hakulielewa  kabisa, ikizingatiwa  sifa  mbaya  aliyo  nayo  kijana  huyo ya kutembea  na  wake  za  watu.

Ulitokea  ugomvi  mkubwa sana  kati  ya  mume  na  mke ambao  uliishia  kwa  mke  kufurushiwa  virago  vyake.

Tukio  la  kufukuzwa  kwa  mwanamke  huyo lilisambaa  sana  mtaani  kwetu, kama  unavyo   jua  tena  mambo  ya  huku  kwetu  uswahilini.  Tukio hilo  liliacha  gumzo kubwa  na karibu  kila  mtu alikuwa  analizungumzia.

Sasa  basi  siku  hiyo  jioni  wakati  mimi  na  wife  tunapiga  ‘ umbeya ‘ wa  mke  na  mume, likaja  suala  la  kijana  Yule  mtukutu  kuvunja  ndoa  ya  watu.  Mimi  nilimtetea  mwanamke, nikisema, jamaa  alichukua  maamuzi  ya  haraka, suala  la  mke  wake  kutoa  chakula  kwa  jirani  alimaanishi  kwamba  ana  uhusiano  wa  kimapenzi  na  huyo jirani.

  Mke  wangu  akaonekana  kulijua suala  hilo  kwa  undani  sana. Akaniambia  ni kweli  kabisa  huyo  mwanamke  anatembea  na  huyo  kijana.  Akaongeza  zaidi, kijana  huyo  ana  uhusiano  na  wake za  watu  wengi  tu  hapo  mtaani, na  siku ikija  kubumbuluka, patakuwa  hapatoshi  hapo mtaani.

Mimi  nikashawishika  kumuuliza  mke  wangu “ HIVI  NI  KITU  GANI HASA   KINACHO WAFANYA, WAKE  ZA  WATU  KUMPAPATIKIA HUYO  KIJANA?!!  MBONA  ANAONEKANA  KIJANA  WA  KAWAIDA  TU, SIO MTANASHATI, HANA  HELA, HANA  KAZI, YUPO  YUPO  TU “.

Mke  wangu  akanijibu  “  SIJUI, ILA  WENYEWE   WANAMSIFU  SANA  WANASEMA, ETI  ANA MASHINE  NZURI,  KUBWA  NENE  NA  NDEFU, NA  NI  MTUNDU  SANA  KITANDANI , NDO  MAANA  WANAMPAPATIKIA “.

Ilibidi  nibadilishe  mada  fasta  na  kuanza  kupiga  story zingine, ila  kusema  ukweli, maneno  ya  mke  wangu  yalinivunja  nguvu  sana kwa  sababu  sifa  alizo kuwa  anamwagiwa  kijana  huyo  mimi  sina  hata  moja.  

Usiku  wa  siku   hiyo   sikulala  kwa  mawazo.Nilijiuliza  maswali  mengi sana, Mke  wangu  ana  maana  gani  kuniambia  maneno  ya  ndani  kiasi  hicho? 

Ina  maana  haniheshimu  tena  kama  ilivyo  kuwa  zamani ? Ananipiga  vijembe  vya  kiutu  uzima ? Unajua  kwa  nini  nasema  ananipiga  vijembe  vya  kiutu  uzima ?  NAJIHISI  NINA  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME,. UUME  WANGU  UMELEGEA, NAWAHI  KUFIKA  KILELENI, NA  NIKIMALIZA  MARA  MOJA  TU NASINZIA  HADI  ASUBUHI. INGAWA  MKE  WANGU  HAJAWAHI  KUNIAMBIA  CHOCHOTE  ILA NAHISI  KABISA  HUWA  SIMTOSHELEZI”.

Sasa  kuniambia  habari  za  huyo  kijana  kwamba  eti  wake  za   watu  wanamsifu  kwamba  AMEJAALIWA   kulinichanganya  sana. Nilihisi  na  yeye  yupo kwenye  hilo  kundi  au  yupo  kwenye  mpango  wa  kujiunga  nalo. Inakuwaje  wanawake  wanakaa  wanazungumza  mpaka  wanafikia  kusema  maneno  hayo ?  Hawazungumzii  ubovu wetu  kitandani  kweli ?

Nikajaribu  kuvuta  kumbukumbu  zangu  kama  mke  wangu  na  huyo  kijana  wanafahamiana, nikakumbuka  miezi  kadhaa  iliyo  pita, Yule  kijana  alipita  nyumbani  kwetu, mimi  nilikuwa  ndani  na  mke  wangu  alikuwa  barazani, basi  wakati  kijana  Yule  anapita, mke  wangu  alimsalimia  kwa uchangamfu mkubwa  sana  huku  akimtaja  jina  lake  na  kumwambia  “ ( jina  la  kijana )  NIAMBIE!”. Kijana  akamjibu  “ poa tu shem mzima?”.

Mke  wangu  akamjibu  “ Mzima  karibu  sana”.   Then  mke  wangu  akataka  kama  kuendelea  kumuongelesha   Yule  kijana  lakini  nadhani  kwa  sababu  ya  heshima  yangu, yule kijana  hakutaka  kuongea  sana, akaongeza  mwendo  na  kuondoka  zake.

Uchangamfu  wa  mke  wangu  kwa  kijana  huyo , sifa  za  kijana  huyo  na  maelezo  ya  mke  wangu  kuhusu  kijana  huyo   vinanifanya  niunganishe  dot  na  kupata  hisia  mbaya  sana  kuhusu  mke wangu  na  kijana  huyo.

Hisia  za  mke  wangu  kuwa  na  mahusiano  na  kijana  huyo  zimenifikisha  mbali  sana  kimawazo . Nikifikiria  kuhama  naona  itakuwa  gharama  kwa  sababu  nitawadisturb watoto  wangu  ambao  wanasoma  kwenye  shule  zilizopo  karibu  na  tunapoishi. Nipo  njia  kwa kweli.
Kusema  kweli  hadi  sasa, sina  amani  kabisa  na uwezo  wangu  kitandani, ndio  na  kila  nisikiapo  jina  la  kijana  yule  nakosa  amana, nahisi  kabisa  huenda mke  wangu  akawa   ana mpango wa  kutembea  nae  au  ameisha  tembea  nae.

RAI  YANGU  KWA  WANAUME  WENZANGU. KAMA  UNAJIJUA  UNA MOYO  MWEPESI, USIMUULIZE  MKEO  SWALI  KAMA  HILO, KWA  SABABU  UNAWEZA  KUPATA  MAJIBU  YATAKAYO  KUUMIZA  MOYO KAMA  NILIYO YAPATA MIMI. NINAJUTA   KWA  NINI  NILIMUULIZA  MKE  WANGU  SWALI  HILO. MPAKA  SASA  HIVI  SINA  AMANI  KABISA NASHINDWA  NIFANYE  NINI.

Ndugu  Msomaji  wa  NeemaHerbalist  BLOG. Unamshauri  nini  jamaa  huyu?

Comments

  1. Tafuta hela tuu kaka utapata faraja na maumivu yote yataondoka yenyewe...faraja ya mwanamme ni pesa yake yakutosha mfukoni sio mwanamke...Mwanamke ni kama kiambatanisho cha furaha ya mwanamme sio msingi wa furaha yake.pole sana

    ReplyDelete
  2. Asante kwa ushauri mzuri.Hope muhusika atausoma na kuuganyia kazi.

    ReplyDelete
  3. Inasikitisha sana, ila ishauri ni kuenda hapo kliniki kwa neema ili kupata ushauri zaidi wa kisaikolojia, pamoja na matibabu.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ...

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na...

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS

Dawa ya TONSILS ni (kugargar)  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto. Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia. Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako. Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafany...