MTI WA MCHOCHO NA TIBA YA WATOTO KUKOJOA KITANDANI Kukojoa bila kukusudia ama kujikojolea ni tatizo linalo wakabili watu wengi duniani . Kukojoa bila kukusudia ama kujikojolea ni ile hali ya mtoto mwenye umri wa miaka mitano au zaidi kushindwa kuzuia mkojo wakati wa mchana au usiku na hivyo kujikojolea kitandani wakati wa usiku au kujikojolea kwenye nguo wakati wa mchana. Tafiti mbalimbali za kitaalamu zinaeleza kuwa watoto wengi wanaacha kukojoa kitandani wakati wa usiku katika umri wa miaka mitatu. Kuchelewa kukomaa kwa uwezo wa kibofu kuzuia mkojo kunaelezwa kuwa ndio chanzo...