MTI WA
MCHOCHO NA TIBA YA
WATOTO KUKOJOA KITANDANI
Kukojoa bila
kukusudia ama kujikojolea
ni tatizo linalo
wakabili watu wengi duniani .
Kukojoa
bila kukusudia ama
kujikojolea ni ile
hali ya mtoto
mwenye umri wa
miaka mitano au zaidi
kushindwa kuzuia mkojo
wakati wa mchana
au usiku na
hivyo kujikojolea kitandani wakati wa
usiku au kujikojolea kwenye
nguo wakati wa
mchana.
Tafiti mbalimbali
za kitaalamu zinaeleza
kuwa watoto wengi wanaacha
kukojoa kitandani wakati wa usiku katika
umri wa miaka mitatu.
Kuchelewa kukomaa kwa uwezo wa kibofu kuzuia
mkojo kunaelezwa kuwa
ndio chanzo kikuu
cha tatizo la
kujikojolea kitandani kwa watoto
wadogo.
Katika tiba
asilia, ipo mimea mbalimbali
inayo tajwa kuwa
na uwezo wa
kutibu tatizo la mtoto kukojoa
kitandani.
Kati ya
mimea hiyo, upo mti
wa mchocho. Mmea huu
umekuwa ukitumiwa na
wenyeji wa mkoa
wa Pwani nchini Tanzania
katika kuwatibu watoto
wenye tatizo la kukojoa
kitandani au kujikojolea.
Jinsi unavyo
tumika, mizizi, magamba na majani ya
mmea huu wenye
ukubwa kama mti
wa muembe huchukuliwa
hukaushwa na kusagwa
kupata unga unga
wake,. Unga wa mti
huu huchemshwa kwenye
maji kisha kimiminika
chake hupewa kunywa
mtoto mwenye tatizo
la kukojoa kitandani
kwa muda wa siku
ishirini na moja. Mtoto
huanza kuonyesha nafuu kuanzia
siku ya saba
na inapofika siku
ya ishirini na
moja, mtoto huyu anakuwa amepona
kabisa tatizo la
kukojoa bila kukusudia
ama kujikojolea kwa
lugha nyingine.
MAKALA HAYA
YAMEANDALIWA NA DUKA
LA NEEMA HERBALIST. TUNAPATIKANA UBUNGO
JIJINI DAR ES
SALAAM, NYUMA YA JENGO
LA UBUNGO PLAZA
JIRANI NA SHULE YA
MSINGI UBUNGO NATIONAL
HOUSING.
TUNAPATIKANA KWA
SIMU NAMBA 0766 53 83 84. KUFAHAMU
ZAIDI KUHUSU TIBA ASILIA
YA MAGONJWA MBALIMBALI. TUTEMBELEE KUPITIA
BLOGU YETU:
Comments
Post a Comment