Skip to main content

Posts

HII NDIO NYUMBA PEKEE YA MTUMISHI WA MUNGU ASKOFU ZAKARIA KAKOBE.

Hii hapa, ndiyo nyumba pekee ya Askofu Mkuu Zachary Kakobe, kama wanavyothibitisha waumini wake, na watu wengi wanaofahamu undani wa maisha yake binafsi. Ni nyumba ya kawaida sana ya vyumba vinne, iliyojengwa katika mtaa wenye nyumba ambazo zimebanana sana, bila kuacha nafasi; eneo la Kijitonyama, Dar-Es-Salaam; umbali mfupi kutoka Kituo cha Polisi, Mabatini. Kakobe, aliijenga nyumba hii, mwaka 1986, kutokana na kazi aliyokuwa akiifanya, na biashara zake binafsi alizokuwa akizifanya, nyakati hizo; kabla ya kuitika wito wa kumtumikia Mungu. Nyumba hii aliijenga kwa gharama ya shilingi milioni mbili tu (Tsh 2,000,000/=) miaka hiyo, ambapo gharama ya ujenzi Tanzania, ilikuwa haijakuwa kubwa, kama ilivyo sasa.  Wakati Kakobe anajenga nyumba hii, Kanisa analoliongoza sasa, la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), lilikuwa bado halijaanzishwa. Kanisa hili, lilianzishwa miaka mitatu baadaye, yaani tarehe 30.4.1989. Mpaka leo, miaka 25 tangu Kanisa hili lianzishwe, Kakob...

SABABU KUMI NA NANE ( 18 ) KWA NINI UNATAKIWA KUPUNGUZA UZITO.

Unene   ni tatizo   linalo   wakabili   watu   wengi   duniani. Kwa   mujibu   wa   tafiti   mbalimbali   za   kitaalamu, unene   una   madhara   makubwa   kuliko   inavyo   dhaniwa. Hizi   ni   sababu   18   kwa   nini   unatakiwa   kupunguza   unene. 1.     Unene   unaongeza   kiwango   cha   mafuta   mwilini, ambayo   huongeza   uwezekano   wa   kupata   kansa. 2.   Unene   unaongeza   mafuta   mwilini, ambayo   hufanya   matibabu   ya   kansa   kuwa   magumu   zaidi. 3.   Unene   huongeza mafuta   mwilini   ambayo   hushinikiza   na   kuubana   moyo. 4.   Mtu mnene   huwa   mvivu   kufanya   mazoezi, suala   ambalo   humuongez...

Walimu wanahitajika kwa haraka sana

Walimu wa masomo yafuatayo wanaitajika kwa haraka sana. Civics , History , Geography,Kiswahili, Mathematics, Physics na Chemistry .Kituo cha kazi kipo manispaa ya Bukoba mkoani Kagera . Shule inatoa huduma ya chakula,usafiri na makazi kwa walimu wanaoishi nje ya shule. Kwa mawasiliano piga 0757297942 au 0787974003 karibu sana. SOURCE : JAMII  FORUMS.

Kitabu; Richard Branson–Mafunzo Ya Maisha(Screw It, Let's Do It)

  Mwezi huu tutajisomea kitabu kilichoandikwa na Richard Branson kinachoitwa SREW IT, LETS DO IT, LESSONS IN LIFE. Richard Branson ni bilionea wa kiingereza ambaye utajiri wake unakadiriwa kufikia dola bilioni 5. Richard ni mwanzilishi na mwendeshaji mkuu wa kundi la makampuni lijulikanalo kama Virgin Group. Katika kundi hili anamiliki makampuni zaidi ya 400. Ni kitu cha kipekee sana kwa mtu mmoja kuweza kuendesha makampuni 400 yenye wafanyakazi zaidi ya 16,000. Richard Branson alianza ujasiriamali akiwa na miaka 16 baada ya kuacha shule. Kilichomfanya aache shule ni kutokana na tatizo la kushindwa kuelewa, yani alikuwa mzito sana kuelewa darasani. Anasema mwalimu mkuu wa shule yake alimwambia atakuwa bilionea au ataishia jela. Baada ya kuacha shule Richard alianzisha jarida lake ambalo alikuwa akiandika mambo yanayohusu wanafunzi. Baadae alifungua studio ya kurekodi muziki na biashara zake zikaendelea kukua mpaka kufikia makampuni zaidi ya 400. Katika kit...