Kuna
kundi la watu
ambao kimuonekano wanaonekana
kuwa na umri
mkubwa kuliko umri
wao halisi.. Unaweza ukakutana
na kijana wa
miaka 28 lakini kimuonekano
anaonekana kama ana
umri wa miaka arobaini.
Vivyo
hivyo wapo watu
ambao wana muonekano mchanga
kuliko umri wao
halisi. Unaweza ukakutana
na mtu ukiambiwa
ana umri wa
miaka hamsini na
nane lakini anaweza
ku pass kama mtu
mwenye umri wa
miaka thelathini na nane.
Adrienne Banfield-Norris katikati mama mzazi wa Jadda Pinket. Ukiona picha zake akiwa anafanya mazoezi gym au ufukweni unaweza kusema ni mdada wa miaka 35 kumbe ni mama wa miaka 66. |
Moja
kati ya sababu
zinazo tajwa kusababisha
baadhi ya watu waonekane
kuwa na umri
mchanga kuliko umri
wao halisi ni
pamoja na aina
ya vyakula wanavyo
tumia pamoja na
watu hao kuwa
na utaratibu w a kufanya
mazoezi ya mwili
na viungo ya
mara kwa mara.
Tafiti mbalimbali
za kitaalamu zinaonyesha
kuwa watu wenye utaratibu
wa kufanya mazoezi
ya mwili na
viungo husalia kuwa
na muonekano mchanga
kuliko umri wao.
Dada / Mama katika safari ya kupamabana na muonekano uzee kwa njia ya mazoezi na vyakula. |
Miongoni
mwa watu maarufu
walio katika kundi
hili ni Adrienne
Banfield-Norris ambae ni mama mzazi wa
Jada Pinket . Mama
huyu amezaliwa mwaka
1953 which means
mwaka huu anatimiza
umri w a miaka 66. Lakini
kimuonekano anaonekana kama
mdada wa miaka
arobaini vile.
Katika moja kati
ya mahojiano aliyo
fanya na vyombo
mbalimbali vya habari
nchini Marekani, mama huyu
anasema siri kubwa
ya kubaki katika
muonekano ujana licha
ya kuwa umri
umesonga ni ulaji
mzuri wa vyakula na
kufanya mazoezi ya mwili
na viungo ya
mara kwa mara.
Mama huyo anasema
mazoezi ya mwili na
viungo imekuwa ni kama
sehemu ya maisha
yake.
Mambo
yanayo weza kusababisha mtu
aonekane kuwa na
muonekano mkubwa kuliko
umri wake ni
pamoja na ulevi sugu, uvutaji sigara
sugu, ulaji mbaya wa
chakula pamoja na
kutofanya mazoezi ya
mwili na viungo.
Haya ni
mambo ambayo yapo
chini ya uwezo
wa karibu kila
mmoja wetu,. Ukizingatia
kula vyakula vizuri , kunywa kistaarabu
na kupunguza au
kuacha kabisa utumiaji
wa sigara pamoja
na kufanya mazoezi
ya mwili na viungo
mara kwa mara basi
unaweza kupambana na
suala la kuwa na muonekano
wa uzee kuliko
umri wako.
Vifuatavyo
ni baadhi vyakula vinavyo
tajwa kuwa uwezo
wa kupambana na
tatizo la kuwa
na muonekano wa uzee :
1.
Karanga za
aina zote
2.
Ufuta
3.
Maziwa ya
mchele au choya
4.
Mananasi
5.
Juisi ya
limao
6.
Juisi ya
ndimu
7.
Matikiti maji
8.
Machungwa
9.
Maparachichi
10. Mbegu
za makomamanga
11. Mafuta
ya Zeituni
12. Baadhi
ya aina ya
uyoga unaoliwa
13. Viazi
vitamu
14. Karoti
15. Brocoli
16. Nyanya
17. Maharage
18. Mtindi
19. Manjano
20. Spinach
21. Jibini
Hivyo ni
baadhi ya vyakula
lakini vipo vtakula
vya aina nyingi
ambavyo vinatajwa na
wataalamu kuwa na
uwezo wa kupambana
na tatizo la
kuwa na muonekano
wa uzee.
Hivyo ni
vyakula ambavyo vinatumika
kwa kula, lakini pia zipo
dawa mbalimbali za
asili ambazo zinatumika
kwa kula pamoja
na kupaka kwenye
ngozi. Dawa hizo za
asili husaidia kuimarisha afya
ya ngozi na
kuifanya iwe na
muonekano wa ujana.
Kwa maoni
na ushauri usisite
kuwasiliana nasi kupitia
namba zetu za
simu ambazo ni 0693
005 189. Pia unaweza kjufika
dukani kwetu. Tunapatikana UBUNGO
jijini DAR ES
SALAAM jirani na
SHULE YA MSINGI
UBUNGO NATIONAL HOUSING
nyuma ya jengo
la UBUNGO PLAZA.
Comments
Post a Comment