Kuna idadi kubwa ya watu ambao wana kabiliwa na tatizo la kuwa na uzito mdogo kupita kiasi. Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kitaalamu, kuwa na uzito mdogo kupita kiasi ni jambo linalo weza kuhatarisha afya ya mhusika Kama ilivyo kwa suala la kuwa na uzito mkubwa kupita kiasi, suala la kuwa na uzito mdogo kupita kiasi pia lina madhara mengi katika afya ya binadamu. MADHARA YA KUWA NA UZITO MDOGO KUPITA KIASI ( KUKONDA NA KUDHOOFU MWILI ) Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kitaalamu, yafuatayo ni madhara ya kiafya yanayo weza kumpata mtu mwenye tatizo la uzito mdogo kupita kiasi. 1. Kupungua na kudhoofika kwa kinga ya mwili 2. Kuwa katika hatari ya kushambuliwa na magonjwa ya mifupa kwa sababu mwili hushindwa kupokea na kutengeneza virutubisho muhimu vinavyo hitajika katika kuimarisha afya ya mifupa 3. Kuwa na nywele zisizo na afya ( Kinyonyoki) 4. Kuwa na ngozi isiyo na afya 5. Kuugua mara kwa mara kutokana na kuwa na kinga...