SHAYIRI TETEKUWANGA : Ugonjwa wa tetekuwanga husababishwa na vijidudu vidogo sana aina ya vijasumu. huanza wiki 2 hadi 3 baada ya mtoto kukaa na mtoto mwingine ambaye tayari anao ugonjwa huu. Kwanza kabisa, madoadoa au vipele vidogo sana vyekundu na ambavyo huwasha, huanza kutokea. Hivi, hubadilika na kuwa malengelenge na mwishowe, kufanya ganga vyote kwa wakati mmoja. Kawaida huanza kwenye mwili na baadaye hutokea kwenye uso, mikono na miguu. Kunaweza kukawa na vipele, malengelenge, na ganga vyote kwa wakati mmoja. Kwa kawaida homa ni kidogo tu. Tiba: Ugonjwa hupona baada ya wiki moja. Mkogeshe mtoto kila siku kwa sabuni na maji ya uvuguvugu ili kupunguza kuwasha. Tumia nguo baridi zilizoloweshwa kwenye maji yaliyotokana na shayiri iliyochemshwa na kukamuliwa. Kata kucha za mikono ziwe fupi kabisa. Kama ganga zinapata ugonjwa, paka gentia violet (g.v) au mafuta ya kuua vijidudu. SURUA Ugonjwa huu mkali ambao husababishwa na vijasumu pia ni wa hatari sana kwa wa...