Skip to main content

JINSI YA KUANDAA LISHE YA NDIZI KWA AJILI YA KUFANYA DIET YA KUPUNGUZA UZITO.




Tunda  la  ndizi  limekuwa  likitajwa  kama  tunda  linalopaswa  kuepukwa  na  mtu  anayetaka  kupunguza  uzito. Hata  hivyo jambo  hilo  sio  kweli.  Ukweli  wa  kustaajabisha  ni  kwamba,ndizi  ni  tunda  muhimu  sana  kwa  mtu  anayetaka  kufanya  diet  ya  kupunguza  uzito  kwa  sababu  lina  utajiri  mkubwa  sana  wa   madini  ya   Pottassium.
Madini  ya  Potassium  husaidia  kupunguza  ama  kuondoa  maji  ya  ziada  katika  mwili  wa  mwanadamu.
Vilevile  madini  haya  yana  uwezo wa  kuharakisha  mmen’ngenyo  wa  chakula  hasa  hasa  yanapotumika  pamoja  na  vyakula  vingine  vinavyo saidia  kuyeyusha  mafuta  ya  mwilini  kama   vile  spinachi  na mboga  ya  majani  iitwayo  lin.
Ndizi  moja  inaweza  kuwa  na  madini  ya  Potassium   kiasi  cha  Gramu  450  kulingana  na  ukubwa  wa  ndizi  yenyewe.
Tunda  la  ndizi  ni  chanzo  kizuri  cha  nishati  mwilini  kwa  sababu  lina   glucose, fructose  na  sucrose   ambavyo  ni  virutubisho  muhimu  katika  kuongeza  nguvu  katika  mwili  wa  mwanadamu .

Kutokana  na   virutubisho  ilivyo  navyo, tunda  la  ndizi  ni bora  sana  pale  linapokuja  suala  la kupunguza  njaa  na  hamu  ya  kula.

Hivyo  basi,  unashauriwa  kula  tunda  la  ndizi  badala  ya  kutumia  vitafunwa  ambavyo  vinaweza  kukuweka  katika  hatari  ya  kuongeza  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini.
Kama  nilivyo  eleza  hapo  awali, virutubisho  vinavyo  patikana  ndani  ya  tunda  la  ndizi  vitasaidia  kuharakisha  mfumo  wa  mmen’genyo  wa  chakula  katika  mwili  wako.
Tunda  la  ndizi  linasimama  kama  ingredient  muhimu  sana  katika  kutengeneza  vinywaji maalumu  kwa  kuyeyusha  mafuta  ya  mwilini.
Tengeneza  lishe  ya  ndizi  kwa  kuchanganya  na  spinachi, mbegu  za  lini, pamoja  na beri  pori  (wild  berries)

JINSI  YA  KUTENGENEZA  LISHE  YA  NDIZI  &  MBEGU  ZA  LIN  KWA  AJILI  YA  KUFANYA  DIET  YA  KUPUNGUZA  MWILI.
Mahitaji :
·         Ndizi  Moja
·         Chungwa  moja
·         Vijiko  viwili  vidogo  vya  mbegu  za  lin.
·         Vijiko  viwili  vidogo  vya  jibini.


MATAYARISHO:
Weka  mchanganyiko  wako  wote  katika  blenda  na  kuusaga  kwa  pamoja.

MATUMIZI :
Tumia  kunywa  glasi  moja  ya  mchanganyiko  wako, mara  mbili  kwa  siku  kwa  siku  ishirini  na  moja.
JINSI  YA  KUTENGENEZA  LISHE  YA  KUPUNGUZA  MWILI  KWA  KUTUMIA  MCHANGANYIKO  WA  NDIZI  & MATUNDA  PORI :
MAHITAJI :
·         Ndizi  moja
·         Kikombe  kimoja  cha  cranberries, raspberries  au  blue  berries.
·         Kijiko  kimoja  kidogo   cha  tangawizi  iliyo  sagwa
·         Kijiko  kimoja  kidogo  cha  asali
·         Nusu  kikombe  ya maji  vuguvugu.
MATAYARISHO  NA  MATUMIZI  YANAFANANA  NA  YA  HAPO  JUU.
  •  
  •  
  • JINSI  YA  KUTENGENEZA  LISHE  YA  NDIZI  YA  KUPUNGUZA  MWILI  KWA  KUTUMIA  NDIZI  NA  SPINACHI.

Mahitaji :
·         Ndizi  moja
·         Gramu  200  za  fresh  spinach
·         Nusu  kikombe  cha  mtindi
·         Nusu  kikombe  cha  ngano  iliyokobolewa
·         Kikombe  kimoja  kidogo  cha  asali.

MATAYARISHO  NA  MATUMIZI  YANAFANANA  NA  HAPO  JUU.

Makala  haya  yameandaliwa  na  NEEMA HERBALIST, wauzaji  wa  dawa  mbalimbali  za  asili. Tunapatikana  jijini  Dar  Es  salaam.
Wasiliana  nasi  kwa  simu  0766538384.

Comments

Popular posts from this blog

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na...

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ...

FAIDA KUMI ZA MTI WA MKOMAMANGA

Mti   wa   Mkomamanga   ni   mti   wenye   faida   nyingi   sana   katika   afya   ya   mwanadamu. Mti   huu   una   virutubisho –afya     mbalimbali   ambavyo   ni   muhimu   katika   afya   ya   mwanadamu.   Virutubisho   hivyo   vinapatikana   kwenye   magome, majani, mbegu, maganda   ya   matunda, juisi   ya   matunda   pamoja   na kwenye   maua   ya   mti   wa   mkomamanga. Zifuatazo   ni   faida   muhimu   za   mti   wa   mkomamanga : 1.           Maganda   ya   tunda   la   mkomamanga   yakichemshwa    hutoa   juisi    ambayo   hutumika   kama   dawa   ya   kufunga   kuhara. 2.   ...