Skip to main content

KULA NYANYA UJIEPUSHE NA KIHARUSI






SOTE tunajua ugonjwa wa kiharusi (stroke) ni miongoni mwa magonjwa hatari kwani ukikupata unaweza kudhoofisha baadhi ya viungo vyako vya mwili kama siyo vyote na kukufanya ushindwe kufanya kazi zako za kawaida na kuwa mtu wa ndani tu kwa maisha yako yote.
Lakini unaweza kujiepusha na ugonjwa huo hatari kwa kuzingatia ulaji wa vyakula sahihi pamoja na kufanya mazoezi. Utafiti wa hivi karibuni umebaini kwamba nyanya (tomatoes) hutoa kinga mwilini dhidi ya ugonjwa wa kiharusi au kupooza kama unavyojulikana na wengine.
Hivi karibuni, watafiti wa nchini Finland walifanya utafiti wa kina na kutoa taarifa kuhusu kirutubisho aina ya ‘lycopene’ kinachopatikana kwa wingi kwenye nyanya, matikitimaji na pilipili.  Wamesema katika taarifa yao kuwa watu zaidi ya 1,000 waliowafanyia utafiti wenye kiwango kingi cha ‘lycopene’ kwenye mfumo wa damu zao, hawakuonesha dalili kabisa za kupatwa na kiharusi.
Aidha, Chama cha Taifa cha wenye Kiharusi cha nchini Marekani (The National Stroke Association) kimesema kuwa wanawake wengi  hufariki dunia nchini humo kutokana na kiharusi kwa idadi sawa na wale wanaofariki kutokana na ugonjwa wa saratani ya matiti. Hii ina maana kwamba ugonjwa wa kiharusi nao ni tishio kama ilivyo kwa ugonjwa wa saratani ya matiti.
Utafiti mwingine katika eneo hilo umeonesha pia kuwa wanaume wana hatari kubwa zaidi ya kufariki dunia au kupatwa na matatizo mengi kutokana na ugonjwa wa kiharusi kuliko wanawake. Hivyo kati ya wanaume na wanawake, wanaume zaidi ndiyo hupatwa na kiharusi au matatizo yatokanayo na ugonjwa huo kuliko wanawake.
Utafiti huu mpya umeendelea kuthibitisha ukweli wa siku zote kuwa matunda na mbogamboga hutoa kinga katika mwili wa binadamu dhidi ya magonjwa mengi hatari, hivyo wito umetolewa tena wa watu kupenda kula matunda na mbogamboga hasa nyanya, matikitimaji pamoja na pilipili ambavyo vimeonekana kuwa na kinga kubwa zaidi mwilini.
Hata hivyo, imeelezwa kuwa baada ya matokeo ya utafiti huu, watu wamekumbushwa umuhimu wa kuendelea kula na aina nyingine ya matunda, kwani kila tunda au mboga ya majani ina faida na umuhimu wake katika mwili wa binadamu.
Mwisho imeelezwa kuwa ulaji wa nyanya za aina zote una faida, iwe ni ile inayopikwa pamoja na mboga au ile inayoliwa ikiwa imeiva bila kupikwa. Ni vizuri kuchangamkia ulaji wa vitu kama hivi ili kuipa miili yetu uwezo wa kujikinga wenyewe dhidi ya maradhi hatari, yakiwemo yale ya saratani ambayo kwa kiasi kikubwa huweza kuzuiwa kwa kula mboga za majani na matunda ya aina mbalimbali.

CREDIT : GPL

Comments

Popular posts from this blog

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na...

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ...

FAIDA KUMI ZA MTI WA MKOMAMANGA

Mti   wa   Mkomamanga   ni   mti   wenye   faida   nyingi   sana   katika   afya   ya   mwanadamu. Mti   huu   una   virutubisho –afya     mbalimbali   ambavyo   ni   muhimu   katika   afya   ya   mwanadamu.   Virutubisho   hivyo   vinapatikana   kwenye   magome, majani, mbegu, maganda   ya   matunda, juisi   ya   matunda   pamoja   na kwenye   maua   ya   mti   wa   mkomamanga. Zifuatazo   ni   faida   muhimu   za   mti   wa   mkomamanga : 1.           Maganda   ya   tunda   la   mkomamanga   yakichemshwa    hutoa   juisi    ambayo   hutumika   kama   dawa   ya   kufunga   kuhara. 2.   ...