Skip to main content

Mimea Inayo Tibu Tatizo La Homa Ya Mapafu ( Pneumonia ) Kwa Watoto.

Mbefu; unaotumika  katika  tiba  dhidi  ya  ugonjwa  wa  Homa  ya  Mapafu

Mbefu


Chimtemte: Majani  ya  mmea  huu  hutumika  katika  tiba  dhidi  ya  ugonjwa  wa  Homa  ya  Mapafu
Vigengegenge
Msada


Msada
Homa ya mapafu ni aina ya maambukizi yanayoathiri mapafu. Ni ugonjwa ambao unaua watoto wengi hasa katika nchi zinazoendelea duniani. Inakadiriwa kwamba watoto karibu milioni 1.6 walio chini ya miaka 5 wanakufa kila mwaka kutokana na ugonjwa huu. Kutokana na vifo vingi vinavyotokana na homa ya mapafu tarehe 12 ya mwezi wa Novemba kila mwaka imefanywa kuwa siku rasmi ya homa ya mapafu duniani, ambapo nembo ya siku hiyo ni nguo za rangi ya bluu.





Muundo wa Mapafu

Mapafu yanajumuisha mirija mikubwa ya hewa (bronchi) ambayo hugawanyika kufanya mirija midogo zaidi ya hewa (bronchioles), ambayo nayo hutengeneza vifuko vidogo vidogo ya hewa (alveoli). Vifuko hivi vidogo vya hewa (alveoli) vina mishipa ya kupitisha damu (capillaries) ambayo husaidia kuchuja na kusafirisha hewa safi ya oksijeni tunayovuta kuingia kwenye damu na hewa chafu ya ukaa (kaboni dioksidi) kuondolewa kwenye damu na kuingizwa kwenye mapafu tayari kwa kutolewa nje ya mwili.
Kwa kawaida vifuko hivi vidogo hujaa hewa muda wote tayari kwa kusafirishwa. Inapotokea mtu akapata homa ya mapafu, vifuko hivi hujaa maji au usaha hivyo kuathiri upitishaji wa hewa safi kwenye damu na kusababisha tatizo la kupumua.


Homa ya mapafu husababishwa na nini?
Kuna aina kadhaa ya vimelea ambao vinaweza kusababisha maambukizi ya mapafu. Vimelea hivi hujumuisha bakteria, virusi, parasite na fangasi.Vimelea hawa hushambulia mwili wa binadamu kulingana na umri na kinga ya mwili. Kwa mfano, bakteria wanaosababisha homa ya mapafu kwa watoto wachanga ni tofauti na wale wanaosababisha ugonjwa huo kwa watoto wakubwa.
Baadhi ya vimelea wa bakteria wanaoshambulia watoto ni pamoja na Streptococcus pneumoniae ambao ni aina ya bakteria wanaoongoza kusababisha homa ya mapafu kwa watoto. Wapo pia Haemophilus influenzae aina b (Hib) ambao ni aina ya pili ya bacteria walio maarufu zaidi kwa kusababisha ugonjwa wa homa mapafu kwa watoto. Staphylococcus aureus ni aina nyingine ya bacteria ambao hushambulia zaidi watoto wachanga. Kuna pia Group B streptococci ambao pia hushambulia zaidi watoto wachanga.
Kwa upande wa virusi, virusi wa aina ya Respiratory syncytial virus ndiyo wanaoongoza kwa kusababisha homa ya mapafu kwa watoto.
Aidha, vimelea wa Pneumocystis jiroveci ambao kwa sasa huwekwa kwenye kundi la parasite ni maarufu zaidi miongoni mwa parasite wanaosababisha homa ya mapafu kwa watoto wenye upungufu wa kinga mwilini hususani watoto wenye VVU.
Aina nyingine za bakteria ambao hushambulia zaidi watoto wakubwa ni pamoja na Mycoplasma pneumonia naChlamydia pneumonia.


Jinsi Homa ya Mapafu inavyoenezwa

Kuna namna nyingi za kuenea kwa homa ya mapafu. Kwa kawaida, virusi na bacteria hupatikana katika sehemu ya juu ya mfumo wa njia ya upumuaji (upper respiratory tract). Inapotokea kinga ya mwili ya mtoto imeshuka kwa sababu yeyote ile, vimelea hivi huweza kusambaa na kufika mpaka sehemu ya chini ya mfumo wa njia ya upumuaji (lower respiratory tract) na hatimaye kushambulia mapafu. Hali kadhalika, vimelea hawa wanaweza kuenea kwa njia ya damu kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kabla ya kuzaliwa yaani kipindi cha mimba.

Dalili za ugonjwa wa homa ya mapafu


Dalili za vichomi au homa ya mapafu kwa watoto hutegemea na umri wa mtoto. Kwa watoto wadogo, dalili za awali zinaweza kuwa homa kali pamoja na mtoto kuhangaika na kunyongonyea. Watoto wanaozaliwa wakiwa na uambukizi wa bacteria aina ya Streptococcus kundi B wanaweza kuwa na homa na kupumua kwa shida. Wakati mwingine mtoto anaweza kuwa na dalili ambazo si maalum (no-specific symptoms) kama vile kuhangaika na kushindwa kunyonya au kula vizuri bila kuwa na dalili yeyote ya kushindwa kupumua. Hali hii inaweza kutokea kwa mtoto wa umri wowote ule. Dalili za kawaida za homa ya mapafu ambazo huwapata karibu watoto wote wanaoathirika na ugonjwa huu ni pamoja na:

homa
Kuhisi baridi
kikohozi
Kupumua kwa haraka kuliko kawaida
kutoa sauti isiyo ya kawaida wakati wa kupumua
Mbavu za mtoto kuingia ndani wakati wa kupumua
maumivu ya tumbo
kupoteza hamu ya kucheza
kupoteza hamu ya kula na kushindwa kunyonya
Mtoto kubadilika rangi na kuwa na rangi bluu katika midomo na kucha
Hata hivyo, si lazima dalili zote hizi ziwepo kwa kila mtoto. Baadhi ya watoto huonesha kupumua kwa haraka kama dalili pekee ya homa ya mapafu. Iwapo vimelea vimeshambulia sehemu za chini ya mapafu karibu ya tumbo, sehemu ijulikanayo kama kiwambo au diaphragm, mtoto anaweza asioneshe hali yeyote ya kushindwa kupumua ingawa anaweza kuwa na homa na kujihisi maumivu makali ya tumbo, vichomi na pia kutapika.
Watoto wachanga wanaweza kushindwa kunyonya, na pia kupoteza fahamu na kupata degedege.


Vihatarishi vya homa ya mapafu (risk factors)

Katika hali ya kawaida kinga ya mtoto mwenye afya njema humlinda asishambuliwe na vimelea vinavyosababisha magonjwa mbalimbali. Hali huwa ni tofauti pale ambapo kinga ya mtoto ni ndogo au dhaifu, kwa vile mfumo mzima wa ulinzi huathirika na hivyo basi inakuwa ni rahisi kwa mtoto kupata homa ya mapafu.
Mfumo wa kinga wa mtoto unaweza kuwa dhaifu kwa ukosefu wa lishe bora hasa kwa watoto wachanga ambao hawanyonyeshwi ipasavyo. Aidha uwepo wa magonjwa mengine, kwa mfano, maambukizi ya VVU, saratani na ugonjwa wa Surua hupelekea kinga ya mwili kuwa dhaifu.
Lakini vile vile kuna mazingira yanayoweza kusababisha mtoto kuwa katika hatari ya kupata homa ya mapafu mfano moshi wa sigara, au moshi ndani ya nyumba unaosababishwa na kupikia kuni au mkaa. Vilevile msongamano ndani ya nyumba kutokana na watu kuwa wengi sehemu moja nayo huweza kusababisha watoto kupata homa ya mapafu.


Uchunguzi na Vipimo

Daktari humchunguza mtoto mgonjwa kwa kusikiliza dalili za ugonjwa kutoka kwa mzazi/mlezi wa mtoto, kuchunguza viashiria vya ugonjwa huu na kisha kumpima mtoto kwa kutumia kifaa kinachosaidia kusikia sauti mbalimbali katika mfumo wa hewa wa mgonjwa kiitwacho stethoscope.
Ili kujiridhisha na kuwa na uhakika wa tatizo hili, vipimo vifuatavyo vinaweza kufanywa kulingana na mazingira na upatikanaji wake. Vipimo hivyo ni pamoja na X-ray ya kifua, au CT-scan ya kifua, pamoja na damu ili kuchunguza madhara yaliyoletwa na homa hii ya mapafu.
Faida ya kipimo cha CT-scan ni ule uwezo wake wa kutofautisha aina tofauti za homa ya mapafu na aina ijulikanayo kama Atypical pneumonia ambayo si rahisi kuonekana kwa kutumia X-ray ya kawaida ya kifua. X-ray ya kifua na CT-scan ya kifua kwa pamoja vina uwezo wa kuonesha tatizo hata pale ambapo daktari ameshindwa kusikia sauti maalum kwa kutumia kifaa chake cha stethoscope.


Matibabu
Maamuzi ya Matibabu kwa watoto wenye homa ya mapafu hutegemea aina ya vimelea, umri na hali ya mtoto. Mara nyingi antibiotics ndizo hutumika katika kutibu homa ya mapafu inayosababishwa na maambukizi ya bakteria. Kwa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi, antibiotics hazina uwezo wowote wa kutibu. Ieleweke kuwa ni tabibu anayeweza kufahamu kama mtoto wako anahitaji antibiotics au dawa za aina nyingine, kwahiyo ni muhimu kwa mzazi ama mlezi kumpeleka mtoto hospitalini haraka pindi mtoto anapoonesha dalili za ugonjwa huu badala ya kuamua kumpa dawa bila kufuata ushauri wa wataalamu wa afya.


Namna ya kuzuia Homa ya mapafu
Homa ya mapafu inaweza kuzuiwa kwa chanjo, lishe bora na ya kutosha na mtoto kuishi katika mazingira yenye hewa safi.
Kuzuia homa ya mapafu kwa watoto ni sehemu muhimu ya mkakati wa Taifa wa kupunguza vifo vya watoto. Chanjo dhidi ya Hib, pneumococcus, surua na kifaduro ni njia mojawapo ya kuzuia homa ya mapafu.
Lishe ya kutosha ni muhimu kwa kuboresha kinga ya mwili ya mtoto ambapo inashauriwa mama kunyonyesha mtoto bila kuchanganya na kitu chochote walau kwa miezi sita ya mwanzo ya maisha yake.
Kuhimiza usafi katika makazi kama kutotumia jiko la mkaa au kuni ndani ya nyumba na uvutaji wa sigara ni jambo linaloshauriwa pia. Hii inasaidia kupunguza idadi ya watoto kupata homa ya mapafu. Kwa watoto wenye VVU, matumizi ya dawa ya cotrimoxazole kila siku husaidia kupunguza uwezekano wa kupata homa ya mapafu.

Utafiti umeonyesha kwamba kinga na tiba sahihi ya homa ya mapafu inaweza kuzuia vifo milioni moja kwa watoto duniani kila mwaka. Hivyo ni wajibu wetu sote kushirikiana kupambana na ugonjwa huu wa homa ya mapafu

Chimtemte  : Huu  ni  mmea  uliofanyiwa  utafiti  na  kuthibitishwa  kisayansi, kuwa  na  uwezo  wa  kutibu  tatizo  la  Homa  ya  Mapafu.
Jinsi  ya  kutumia  chemsha  majani  yake  yakiwa  mabichi  ( fresh) kisha  kunywa  kimiminika.

Mbefu : Huu mi  mmea  ulio fanyiwa  utafiti  na  kuthibitika  kuwa  na  uwezo  wa  kutibu  tatizo  la Homa  ya  mapafu. Jinsi  ya  kutumia  mmea  huu, chemsha  majani  yake  yakiwa bado  mabichi ( fresh ) halafu  mpatie  mgonjwa  kimiminika  atumie  kwa  kunywa. Atapata  nafuu  kubwa  sana.
 Mbali  na  kutibu  Homa  ya  Mapafu, mmea  huu  hutumika  pia  katika  tiba  dhidi  ya  kikohozi sugu.

Msada : Msada  ni  mmea  mwingine  ambao  umefanyiwa  utafiti  wa  kutosha  na  kuthibitika kuwa  na  uwezo  wa  kutibu  tatizo  la  Homa  ya  Mapafu.
Matunda  ya  mti  huu  huliwa  na  binadamu  na  huwa  yana  ladha  nzuri  inayo  fanana  sana  na  tunda  la  Tufaa  ( Apple ).
Majani  ya  mti  huu, yaki chemshwa    kwenye  maji  kisha  mgonjwa  akapewa   kimiminika   na  kutumia  kwa  kunywa, mara  tatu  kutwa  kwa  muda wa  siku  kumi  na  nne, hakika  atapata  nafuu  kubwa  sana.
Mbali  na  kutibu  Homa  ya  Mapafu, mti  wa  msada, una tumika  pia  katika  tiba  dhidi  ya  malaria, maumivu  ya  kifua  na  minyoo wa  tumboni.
Vigengegenge : Huu  ni  mmea  mwingine  ulio  fanyiwa  utafiti  na  kitabibu  na  kuthibitika  kuwa  na  uwezo  wa  kutibu  tatizo  la  Homa  Ya  Mapafu.  Sehemu  ya  mmea  huu  inayo  tumika  katika  tiba  dhidi  ya  Homa  Ya  Mapafu  ni  majani  yake.  Jinsi  ya  kutumia, chemsha  majani  yake  kwenye  maji  kisha  mpe  mgonjwa  anywe  kikombe  kimoja  chenye  ujazo  wa  milimita  mia mbili  hamsini, mara  tatu  kwa  siku  asubuhi  mchana  na  jioni  kwa  muda  wa  siku  tatu, na  kwa  hakika, atapata  nafuu kubwa  sana.
Hiyo  ni  baadhi  ya  mimea, inayo patikana  katika  ardhi  ya  Tanzania  ambayo  imefanyiwa  utafiti  na  kuthibitika. Ipo  mimea  mingine  mingi kwa  mamie  yake, ambayo  nayo  ina  uwezo  wa  kutibu tatizo  la  homa  ya  mapafu. Kufahamu  kuhusu  mimea  hiyo, tembelea  kila  siku hapa  Neema  Herbalist  Blog.





MAKALA  HAYA  YAMELETWA  KWETU  NA  NEEMA  HERBALIST  BLOG, KWA  UDHAMINI  MKUBWA  WA   NEEMA  HERBALIST &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC, WAUZAJI  WA  DAWA MBALIMBALI  ZA  ASILI  KAMA  VILE : 

1.                             Dawa  asilia ya  kuunganisha  mifupa, pingili  na kukomaza mifupa.
2.                             Dawa  asilia ya kuondoa  maumivu ya  misuli, kurekebisha  mishipa  na  misuli
3.                             Dawa  asilia  kwa  wagonjwa wa  kiharusi (Kupooza)
4.                             Dawa  asilia ya  kutibu  majeraha
5.                             Dawa  asilia  ya  kutibu  vidonda ndugu
6.                             Dawa asilia  ya  kuondoa  uchovu na  kuwashwa
7.                             Dawa  asilia  ya  kuondoa mafuta  kwenye damu ( kolestrol /lehemu)
8.                             Dawa  asilia  ya  kutibu tatizo  la  nyongo
9.                             Dawa  asilia  ya  kutibu  gauti
10.                        Dawa  asilia  ya  uzazi  wa  mpango
11.                        Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  Goita
12.                        Dawa asilia ya  kutibu  tatizo  la  change  la watoto wachanga.
13.                        Dawa  asilia  ya kutibu  vidonda  vya  tumbo
14.                        Dawa  asilia  ya  kutibu mzio     ( Allergy)
15.                        Dawa asilia  ya  kutibu  tatizo  la  degedege  kwa watoto  wenye  umri  wa  kati  ya  miezi  6  hadi  tisa.
16.                        Dawa asilia  ya  kurutubisha  mayai  ya  uzazi  na  kuzibua  mirija  ya  uzazi  kwa  wanawake.
17.                        Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  utasa  kwa  wanaume.
18.                        Dawa  asilia  ya  kusaidia  kugeuza  mtoto  aliye  kaa  vibaya  tumboni ( Mfano: Katanguliza mikono, makalio n.k )
19.                        Dawa  asilia  ya kupunguza  kitambi, uzito  na  unene  uliozidi.
20.                        Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  vinyama  vya  puani.
21.                        Dawa asilia  ya  kutibu  tatizo  la  bawaziri.
22.                        Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  uchungu  wa  pili  baada  ya  kujifungua.
23.                        Dawa  asilia  ya  kutibu  majeraha ya moto  pamoja na  makovu yatokanayo  na  moyo.
24.                        Dawa  asilia  ya  kutiu  tatizo  la  kwikwi
25.                        Dawa asilia  ya  kutibu  tatizo  la  kutokwa  na  harufu  mbaya  kinywani
26.                        Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  kutoa harufu  mbaya mwilini
27.                        Dawa  asilia  ya  kusaidia  kunenepesha  mtu  aliye  dhoofu  mwili
28.                        Dawa  asilia ya kutibu  tatizo  la  uvimbe  wa  tumboni  ( FIBROID )
29.                        Dawa  asilia  ya  kisukari
30.                        Dawa  asilia  kwa  watu  wenye  tatizo  la  moyo, presha  ya  kupanda, presha ya  kushuka, moyo  kupanuka  na  matundu  kwenye moyo.
31.                        Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  U.T.I, kaswende, kisonono sugu  na  Taifodi.
32.                        Dawa  asilia  ya  kutibu  magonjwa  mbalimbali ya  ngozi
33.                        Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo la  kubanwa mkojo na  maumivu  kwenye  njia  ya  mkojo
34.                        Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  kujikojolea
35.                        Dawa  asilia  ya  kusafisha  figo  na  kibofu  cha  mkojo
36.                        Dawa  asilia  ya  kuondoa  sumu  mwilini
37.                        Dawa asilia  ya  kuondoa  maumivu  ya  hedhi
38.                        Dawa  asilia  za  kuondoa  sumu  ya  nyoka, na  nge.
39.                        Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  pumu
40.                        Dawa  asilia  ya  kuyeyusha uvimbe  kwenye  lango  la  uzazi.
41.                        Dawa asilia ya kutibu  malaria  sugu
42.                        Dawa  asilia  ya kutibu  tatizo  la  upara  
43.                        Dawa  asilia ya  kutibu  tatizo la  kikohozi sugu  na  kimeo.
44.                        Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  ngiri
45.                        Mawe  kwenye  figo
46.                        Kukosa  choo
47.                        Kukosa  hamu  ya  kula
48.                        Chango  la  kike
49.                        Kutanua  nyonga ( Kuzaa  bila  kupasuliwa )
50.                        Nguvu za  kiume
51.                        Hamu  ya tendo  la  ndoa  kwa  wanawake.
52.                        Mtoto kuchelewa  kutembea

DAWA   ZOTE  HIZI  NI  ZA  ASILIA KABISA  NA  HAZINA   KEMIKALI ZA  VIWANDANI.
Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR ES  SALAAM, jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING, nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO PLAZA.
Kwa  wateja  waliopo  Dar  Es  Salaam, ambao  hawana  nafasi  ya  kufika  ofisini  kwetu, watapelekewa  dawa  mahali  popote  walipo.
Kwa  wateja  waliopo  mikoani, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  mabasi.
Kwa wateja  waliopo  Zanzibar, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  boti.
Kwa wateja  waliopo Mombasa, watatumiwa  dawa  kupitia  basi  la  TAHMEED.
Kwa  wateja waliopo  jijini  Nairobi, watatumiwa  dawa  kupitia  basi  la  DAR  EXRESS.
Na kwa  wateja  waliopo  ughaibuni, watatumiwa  dawa  kwa  njia ya  POSTA  au  DHL.
WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA:
0766 – 53 83  84.
Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu huduma zetu, tutembelee  kila  siku, kupitia :


Comments

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ...

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na...

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS

Dawa ya TONSILS ni (kugargar)  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto. Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia. Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako. Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafany...