Skip to main content

Lusangalala : Mmea Unao Tibu Ugonjwa wa Pumu, Na Magonjwa Mengine Lukuki.


Lusangalala : Mmea  Unao  Tibu  Ugonjwa  wa  Pumu, Na  Magonjwa Mengine  Lukuki



Mmea  wa  Lusangalala


Utangulizi


Tanzania  imebarikiwa  kwa  kuwa  na  utajiri   mkubwa, wa  mimea  yenye  uwezo  wa  kutibu na kuponyesha  kabisa,   magonjwa  na  matatizo  mbalimbali  ya  kiafya yanayo  msumbua  mwanadamu.

Kati  ya  mimea  inayo  patikana  nchini  Tanzania, ambayo  imethibitika kisayansi, kuwa  na  uwezo  wa  kutibu  na  kuponyesha  kabisa  idadi  kubwa  ya  magonjwa, ni  mmea hujulikanao  kwa  jina  la  Lusangalala.

Mizizi, majani  na  mbegu  za  mmea  wa  Lusangalala, hutumika  kama  tiba  ya  magonjwa  mbalimbali  kama  vile  pumu, matatizo  katika  ini  na  kansa.


Mmea  wa  Lusangalala

Lusangalala  ni  mmea  mdogo unao  kua  hadi  kufikia  urefu  wa  mita  5  hadi 8.

Mmea  wa  Lusangalala, umegawanyika  katika  spishi ( species)  mbalimbali, ambazo  idadi  yake  hufikia  mia  sita  ( 600 ).

Spishi  hizo  zipo  katika  mfumo  wa  miti  na  vichaka

Faida  Za  Kitabibu  Za  Mmea  wa  Lusangalala

Mmea  wa  Lusangalala, hutumika  katika   tiba  ya  magonjwa  mbalimbali, kama  vile pumu, mkamba,magonjwa ya ngozi, magonjwa  mbalimbali  ya  zinaa  na  matatizo  katika  ini, kwa kutaja  machache.

Waluguru, wenyeji  wa  mkoa  wa  Morogoro  nchini  Tanzania, hutumia  mizizi  ya  mmea  wa  Lusangalala  kutibu  homa,  malaria  sugu, matatizo ya  hedhi, kifua  kikuu,anemia,  magonjwa  na  matatizo  mbalimbali  katika  ini.

Vile  vile, mizizi  ya  mmea  huu  hutumika  kama  tiba  ya  kuimarisha  kinga  ya  mwili  kwa  ujumla.


Wakati  mbegu  za  mmea  huu, husagwa  na  unga  wake  hutumika  kama  kinywaji, kutibu  tatizo  la  Asthma.

Maua  ya  mmea  huu, hutumika kutibu  tatizo  la  Mkamba (bronchitis )

Majani  ya  mmea  huu  hutumika kutibu   kaswende & kisonono, homa,maambukizi  katika  njia  ya  mkojo, pamoja  na  matatizo   mbalimbali ya  hedhi  kwa  wanawake.
Majani  ya  mmea  huu, hutumika  pia  katika  tiba  dhidi  ya  tatizo la  maumivu  kwenye  njia  ya  mkojo, na  tatizo  la  kukosa  choo  kwa  watoto  wadogo.
Chai  iliyo  tengenezwa  kwa  kutumia majani  ya  mmea  huu, hutumika kama  tiba  dhidi ya  tatizo  la  maumivu  ya  tumbo  kwa  watoto  wachanga.
Majani mabichi  ya  mmea  huu, hutumika  kama  tiba  ya  kuondoa  minyoo  wa  tumboni.
Majani  yaliyo kaushwa  ya  mmea  huu,  huchemshwa  halafu  chai yake, hutumika  kumkanda  mgonjwa  ,  katika  tiba dhidi   ya  matatizo  ya  ngozi, majeraha  ya kwenye  ngozi, fangasi  wa  kwenye  ngozi, bacteria  wa  kwenye  ngozi,  pamoja  na  tatizo la  kuvimba  kwa  ngozi.


Orodha  Ya  Magonjwa Na  Matatizo  Ya  Kiafya  Yanayo Tibiwa kwa  mmea  wa  Lusangalala


Kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za  kitabibu, mmea  wa  Lusangalala, una  uwezo  wa  kutibu  magonjwa  yafuatayo :

1.     Hutibu  pumu
2.     Hutibu  tatizo  la  mkamba
3.     Huzuia  tatizo  la  kuziba kwa  njia  ya hewa  kwenye  mapafu
4.     Hulinda  ini.
5.     Husaidia  kuondoa  na  kupunguza  maumivu  mwilini.
6.     Huondoa   sumu kwenye ini
7.     Huondoa  uvimbe kwenye  ngozi
8.     Huua  bacteria  wa  kwenye  ngozi
9.     Huua  vimelea  wa  kansa
10.                        Huua  fangasi
11.                        Hutibu  homa
12.                        Huua  virusi  wa  aina  mbalimbali
13.                        Hupunguza  shinikizo la  damu
14.                        Huondoa  minyoo  wa  tumboni
15.                        Huongeza  na  kuimarisha  kinga ya  mwili
16.                        Husafisha  damu
17.                        Huondoa  sumu  mwilini
18.                        Huua  vijidudu  wa  kinywani
19.                         Huimarisha  mfumo  wa  upumuaji
20.                        Hutumika  kuua  wadudu
21.                        Hutibu  matatizo  mbalimbali  ya  hedhi
22.                         Hutumika  kupanga  uzazi
23.                        Hutumika  kutibu  majeraha ya  mikwaruzo
24.                        Husaidia  kuimarisha  afya  ya  wanawake  wajawazito; hutumika  kama  tiba  ya kumsaidia  mama  mjamzito  kujifungua  salama.
25.                         Hutibu tatizo  la  kukosa  choo  au  kupata  choo  ngumu
26.                         Hutibu  matatizo  mbalimbali  ya  macho
27.                        Hutumika  kutibu  matatizo  mbalimbali  ya moyo
28.                        Hutibu tatizo  la  moyo  kwenda  mbio
29.                        Hutumika  kutibu  tatizo  la  maumivu  kwenye  mgongo
30.                        Pamoja  na  magonjwa  mengine  mengi.

Makala  Haya  Yameandaliwa  na  Kutayarishwa  na  Neema  Herbalist  Blog, kwa  msaada  mkubwa  wa   Neema  Herbalist &  Nutritional  Foods  Clinic, duka  la  kuuza  dawa  mbalimbali  za  asili.
Linapatikana  UBUNGO  jijini  Dar  Es  Salaam,  jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING,   nyuma  ya  jengo  la UBUNGO  PLAZA.
Kwa  mahitaji  yako  ya  dawa  ya  Lusangalala, pamoja  na  dawa  nyinginezo  za  asili, wasiliana  nasi  kwa  simu  namba:
0766  53  83  84

Na  kwa taarifa  zaidi, kuhusu  dawa  mbalimbali  za  asili, tembelea kila siku


Comments

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ya  kupata  wapenzi  wa  kike  ama  kuoa  na  wengine  huendelea  na  tabia  hiyo  hata  baada  ya  kuoa .  Zipo  sababu  mbalimbali  zinazo  wapelekea  wanaume  kupiga  punyeto, ila  kubwa  kati  ya  hizo  ni  pamoja  na  kutokuwa  na  wapenzi, kutokuwa  na  wapenzi  wanao  kidhi vigezo  vyao, kuwa  katika  mazingira  yasiyokuwa  na  wanawake  ( mfano  katika  shule  za  sekonda

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS

Dawa ya TONSILS ni (kugargar)  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto. Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia. Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako. Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafanya ka

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na  kuwa  mgumu  kama  msumari. Na  hatua  ya  pili   ni  lazima, uume  wake  uendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa  STRONGER  AND  LONGER  ERECTION JINSI  HATUA  ZA  KUSIMAMA  KWA  UUME  ZINAVYO  TOKEA. 1. HATUA    YA  KWANZA: DAMU  KUTIRIRIKA  KWA