Skip to main content

TIBA ASILIA YA UGONJWA WA PUMU



Lugole; mmea  wenye  mchango  mkubwa  sana  katika  tiba  ya  ugonjwa  wa  pumu


Utangulizi

Kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za  kitaalamu, ugonjwa wa pumu ni ugonjwa ambao huathiri sehemu ya kupitisha hewa kwenda kwenye mapafu ya binadamu zinazojulikana kitaalamu kama
 bronchioles. 


Tunda  la  mmea  wa  Lugole.

Mtu mwenye pumu huwa na mcharuko mwili sugu (chronic Inflammation) kwenye mirija yake ya 
kupitishia hewa
 (bronchioles tubes) hali ambayo husababisha kuvimba kwa kuta za mirija hii, kujaa kwa ute mzito (mucus) na kupungua kwa njia ya kupitishia hewa, hali ambayo humfanya muathirika kushindwa kuvuta na kutoa hewa  nje na hivyo kupumua kwa shida sana.


Mmea  wa  lugole, mbali  na  kutumika  katika  tiba  dhidi  ya  pumu, mmea  huu  pia  unatumika  katika  tiba  ya  magonjwa  mengine  mengi kama  vile  maumivu, homa  na  malaria  sugu, ukoma, kolera, anemia, magonjwa  ya  zinaa  na  hedhi  isiyo koma  kwa  kutaja  machache.

Hali hii inaweza kudumu kwa muda mfupi au mrefu kiasi cha kuhitaji tiba ili kumuwezesha mgonjwa kupata nafuu. 

Kutokana na kuwepo kwa msuguano na uzuiaji wa kupitisha hewa wakati wa kupumua kwa nje, pumu hujulikana pia kama obstructive lung disease .

Mmea  wa  Hambamti  ukiwa  umetoa  matunda


Matunda  ya  mmea  wa  Hambamti, ambayo  hayaiva vizuri.
Hambamti
Mtu aliye na pumu, huwa nayo kipindi chote cha maisha yake. 




Makundi ya Pumu
:Yapo  makundi  makuu  mawili  ya  pumu. Makundi  hayo  ni  kama  ifuatavyo:

  • Pumu ya ghafla (Acute asthma): Wagonjwa wanaopatwa na kundi hili la pumu huwa na hali ya kawaida katika njia zao za hewa isiyobadilika kati ya shambulizi moja na jingine.
 
Kinzasu

  • Pumu sugu (Chronic Asthma): Kundi hili la pumu huwa na tabia ya kuwa na njia nyembamba za kupitisha hewa na kadiri jinsi mgonjwa anavyoendelea kupata matukio zaidi ya pumu, njia za hewa huzidi kuwa nyembamba zaidi.
Kinzasu


Aina za ugonjwa wa pumu 

Bila kujalisha mgonjwa anaingia katika kundi gani, ugonjwa wa pumu unaweza kugawanywa katika aina kuu nne, ambazo ni
 1.Pumu inayobadilika (brittle asthma): Kulingana na tabia ya kujirudia rudia kwa matukio ya ugonjwa huu na madhara yake kwa mgonjwa, aina hii ya pumu inaweza kugawanywa zaidi katika aina nyingine mbili, ambazo ni




Kinzasa

  • Aina ya kwanza ya pumu inayobadilika (type 1 brittle asthma) ni pumu yenye tabia ya kuwa na matukio na mashambulizi ya kubadilika kila mara japokuwa mgonjwa anaweza kuwa anapata matibabu kadhaa.



Kinzasa

  • Aina ya pili ya pumu inayobadilika (type 2 brittle asthma) ni pumu ambayo mgonjwa anatokea kupata shambulizi la ghafla(asthmatic attack) wakati hapo awali ugonjwa wake uliweza kuthibitiwa kwa matibabu.
2.Pumu hatari isiyobadilika (status asthmaticus): Hii ni aina ya pumu iliyo hatari zaidi kwa mgonjwa. Pamoja na  matumizi ya dawa kadhaa,zikiwemo vitanua njia za hewa (bronchodilators) na vipoza mcharuko mwili (steroids), mgonjwa wa aina hii ya pumu anaweza asipate nafuu ya haraka, na anaweza kupoteza maisha. 



Lusangalala

3.Pumu  inayosababishwa na mazoezi (Exercise Induced Asthma): Hali hii husababishwa na ufanyaji wa kupitiliza wa mazoezi ya viungo. Kwa kawaida wakati wa kufanya mazoezi mtu hupumua kwa kutumia pua na kupitia mdomoni.


Lusangalala

Hata hivyo wakati  mwingine hutokea hewa aivutayo huingia ndani ikiwa haijapozwa vya kutosha puani na hivyo kusababisha ongezeko la mtiririko wa damu katika mishipa inayosambaza damu katika mirija ya kupitisha hewa.


Lusangalala

Hali hii husababisha kuvimba   kwa kuta za mirija hiyo na muhusika kupata shambulizi la pumu. Aina hii ya pumu yaweza kudhibitiwa na dawa. Inashauriwa sana kwa watu wenye matatizo kama haya kupasha moto misuli kwa mazoezi mepesi (warming up) kabla ya kuanza mazoezi mazito na ya muda mrefu. 


Mdaa

Mdaa
Mdaa
Mti  wa  Mdaa
4.Pumu inayosababishwa na aina ya kazi afanyayo muhusika (Occupational Induced Asthma): Wakati fulani, mazingira ya kazi yanaweza kusababisha kutokea kwa pumu hata kwa baadhi ya wafanyakazi wasio na tatizo hili. Mara nyingi aina hii huweza kuwatokea watu wanaofanya kazi kwenye viwanda vya kutengeneza matairi, vigae, rangi, kemikali mbalimbali, mbolea, chuma, unga na mbao. 

Pumu husababishwa na nini?
 

Kwa  mujibu  wa  tafiti  za  kisayansi, kuna  mambo kadhaa yanayoweza kusababisha kutokea kwa pumu au yanayohusishwa na shambulizi lake. Mambo hayo ni pamoja na


1.   Matatizo ya kinasaba: Matatizo ya kinasaba yamehusishwa na kutokea kwa karibu asilimia 90 ya ugonjwa wa pumu hususani kipindi cha utoto.

2.   Uvutaji wa sigara au tumbaku kipindi cha ujauzito pia unahusishwa na kusababisha pumu kwa mtoto atakayezaliwa.

3.   Maendeleo ya kiuchumi: Ugonjwa wa pumu umeonekana sana kwenye nchi zilizoendelea kiuchumi ikilinganishwa na nchi zenye maendeleo na hali duni ya kiuchumi.

4.   Magonjwa ya mapafu kama bronchitis


5.   Vyanzo vya mzio (allergens)kama vile vumbi, vinyesi vya wanyama na baadhi ya vyakula.

6.   Uchafuzi wa mazingira kama moshi na baadhi ya harufu kali.


7.   Baadhi ya kemikali kwenye maeneo ya kazi hasa kwenye viwanda kama vya rangi, chuma, sementi na vigae.

8.   Baadhi ya wagonjwa wanaotumia dawa za kushusha shinikizo la damu zilizo katika jamii ya beta-blockers kama vile propanololwapo katika hatari ya kupata shambulio la ugonjwa wa pumu.


9.   Magonjwa kwenye mfumo wa kupumua yasabishwayo na baadhi ya virusi na bakteria kama vile rhinovirus, Chlamydia pneumoniaau Bordetella pertusis.

10.                Matumizi ya mapema sana ya baadhi ya dawa hasa antibiotiki kwa watoto yanaweza kubadilisha mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa na hivyo kumfanya mtoto kuwa katika hatari ya kupata pumu.


11.                Ongezeko la msongo wa mawazo huweza kusababisha pumu na matatizo katika mfumo wa upumuaji

12.                Upasuaji wakati wa kujifungua (caesarian section): Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa kujifungua kwa njia ya upasuaji huongeza uwezekano wa kupata pumu kwa vile njia hiyo yaweza kuathiri mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya maradhi.

Vihatarishi vya ugonjwa wa pumu 

Uwezekano wa kupata ugonjwa wa pumu huongezeka iwapo mtu


1.   Atakuwa na magonjwa ya mzio kama vile magonjwa ya ngozi (eczema) au homa isababishwayo na aina fulani ya vumbi (hay fever)

2.   Atavuta chavu (pollen) kutoka kwenye maua au miti


3.   Atajihusisha na uvutaji sigara

4.   Ana historia ya ugonjwa wa pumu au mzio kwenye familia


5.   Utumiaji wa dawa aina ya aspirin

6.   Ana msongo wa mawazo
7.   Ana uambukizi wa magonjwa ya virusi kamarhinovirus

8.   Anaishi sehemu zenye baridi

9.   Mazoezi  mazito

10.                Ana matatizo katika njia yake ya chakula (Gastroesophageal reflux disease au GERD)

Dalili za ugonjwa wa pumu
 

Dalili za ugonjwa wa pumu ni pamoja na


1.   Kuishiwa na pumzi na kupumua kwa shida (shortness of breath)

2.   Kutoa sauti kama mtu anayepiga miluzi wakati wa kupumua (wheezing)


3.   Kukohoa sana (chronic cough) hasa nyakati za usiku au asubuhi. Aidha kikohozi huambatana na kutoa makohozi mazito, yasiyo na rangi au yenye rangi ya njano.

4.   Kubana kwa kifua.


5.   Kwa mtu aliyepata shambulizi kubwa la pumu (severe asthmatic attack) anaweza kushindwa kuzungumza na pia kuwa na hali kama ya kuchanganyikiwa.

Vipimo na Uchunguzi 

Pamoja na daktari kutaka kufahamu historia ya mgonjwa, anaweza pia kuamua kufanya vipimo vifuatavyo ambavyo vitamsaidia kufahamu chanzo na madhara ya ugonjwa wa pumu kwa muathirika.


1.   Kipimo cha damu (complete blood count) msisitizo ukiwa kwenye wingi wa seli za damu aina ya eosinophils ambazo uhusika na kuwepo kwa shambulio la mzio.

2.   Kipimo cha kuchunguza uwezo wa mgonjwa kutoa hewa nje mara baada ya kuivuta (spirometery). Aina hii ya uchunguzi hufanyika kabla ya mgonjwa kupewa dawa kwa kutumia nebulizer.


3.   Kipimo cha kuchunguza kiwango cha hewa ya oksijeni kilichopo kwenye damu ya mgonjwa (oximetry).
4.   Kipimo cha kuchunguza uwezo wa mgonjwa kupumua hewa nje wakati wa shambulizi la pumu (Peak flow meter).

5.   X-ray ya kifua kwa ajili ya kutofautisha pumu na magonjwa mengine yenye dalili za kufanana kama vile ugonjwa wa moyo(congestive heart failure), magonjwa sugu ya kuziba kwa njia za hewa (COPD kama vile chronic bronchitis na emphysema) na magonjwa mengine ya kuzaliwa kama vile cystic fibrosis.


6.   Kipimo cha mzio cha ngozi (skin allergy test) kwa ajili ya kutambua aina ya mzio inayomsababishia mgonjwa shambulizi la pumu.

Matibabu ya Pumu 

Kwa ujumla matibabu ya pumu hujumuisha kuepuka visababishi vya ugonjwa huu na matumizi ya madawa kwa walio na hali mbaya. Aidha, kwa wanaopata ugonjwa huu kwa sababu ya msongo wa mawazo hupewa ushauri nasaha kwa ajili ya
 kusaidia kutatua matatizo yanayowakabili.

Vilevile inashauriwa kwa wenye tatizo hili, kuwa na dawa karibu muda wote kwa ajili ya matumizi pindi shambulizi litakapotokea.

Pia inashauriwa sana kuepuka mazingira na hali za baridi ambazo huweza kuchochea kutokea kwa shambulio la ugonjwa huu.

Matibabu ya kutumia dawa hujumuisha matumizi ya dawa za kusaidia kupunguza na kuondoa makohozi (expectorants), dawa zinazosaidia kutanua mirija ya hewa (bronchodilators), dawa za kuondoa mcharuko mwili kama vile cortisone ya drip (hasa wakati wa dharura) au nebulizer, na dawa za kuzuia mzio (antihistamine drugs).

 Hata hivyo, kuna matibabu ya ziada kulingana na hali ya mgonjwa pamoja na kundi na aina ya pumu inayomuathiri mgonjwa.

 Kwa wagonjwa wenye pumu ya ghafla na wenye hali mbaya (acute asthma) matibabu hujumuisha matumizi ya dawa za kutanua mirija ya hewa (bronchodilators) pamoja na kuongezewa hewa ya 
oksijeni, dawa za kutuliza mcharuko mwili
 (steroids) pamoja na dawa za kutuliza kukakamaa kwa misuli ya mwili (intravenous muscle relaxants).

Aidha kwa vile mara nyingi shambulizi hili laweza kuwa la hatari sana, mgonjwa hulazwa hospitali na huongezewa hewa ya oksijeni, na kwa wagonjwa wasioweza kupumua kabisa, husaidiwa kufanya hivyo kwa kutumia mashine maalum iitwayo (mechanical ventilator). 

Kwa wagonjwa wenye pumu sugu, jambo la muhimu ni kuepuka visababishi vya pumu na kuendelea na matumizi ya dawa zinazosaidia katika kutanua mirija ya hewa.

Kwa wagonjwa wanaopata mashambulzi ya mara kwa mara wanaweza kushauriwa na daktari kutumia dawa kadhaa zikiwemo zile zinazopunguza mcharuko mwili(mast cell inhibitors, inhaled steroids au oral steroids), pamoja na dawa za kutuliza kukakamaa kwa misuli ya mwili (muscle relaxants).

 Aidha ni vema pia kutibiwa na kuthibiti kutokea kwa magonjwa yote yahusuyo mfumo wa hewa. Matumizi ya chanjo ya magonjwa kama influenza na pneumococcal pneumonia nayo husaidia sana katika uthibiti wa kutokea kwa pumu. Ni vema pia kuepuka matumizi ya dawa za jamii ya beta-blockers kwa wagonjwa wenye shinikizo la damu na ambao pia wana pumu.

Nini madhara ya pumu kwa mama wajawazito?
 

Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa takribani theluthi moja ya wajawazito wenye pumu hupata nafuu kipindi cha ujauzito, theluthi nyingine hupata matatizo kipindi hiki na theluthi iliyobakia huwa na hali ya kawaida kama kabla ya ujauzito.
 

Kwa kawaida dalili za pumu hujirudia kama awali miezi mitatu baada ya kujifungua.
 Dalili za pumu kwa mjamzito zinaweza kuwa mbaya zaidi kuanzia wiki ya 24-36 (mwezi wa sita mpaka wa nane).

Ni mara chache sana mjamzito anapata shambulizi la pumu wakati wa kujifungua. Inakisiwa kuwa, ni asilimia 10 tu ya wajawazito wenye pumu wanaopata shambulizi la pumu wakati wa kujifungua. 

Baadhi ya dawa zinazotumika wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua huongeza madhara ya pumu, hivyo ni vizuri kumueleza daktari kwamba una pumu kabla ya kupewa dawa. Aidha na si vyema kunywa dawa kwa mazoea. 

Wanawake wenye pumu isiyoweza kuthibitiwa kipindi cha ujauzito hupata madhara ya kuzaa mtoto njiti (premature baby), kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo, kifafa cha mimba, shinikizo la damu(Hypertension), na iwapo atapata shambulizi hatari wakati wa ujauzito mtoto anaweza kufa kwa kukosa hewa ya oksijeni. 




UGONJWA  WA  PUMU  KWA  WATOTO  WADOGO

Nini maana ya Pumu?


Pumu ni hali ambayo huathiri njia za hewa, njia hizi za hewa pia huitwa mirija ya kupumulia. Mirija hii huanzia kwenye njia ya hewa(trachea) hadi kwenye mapafu.

Mchakato wa kupumua kwa watoto walio wengi ni rahisi : Watoto huingiza hewa kupitia puani au mdomoni na hewa huingia kwenye njia ya hewa(trachea) na kuelekea kwenye mapafu. Lakini Kwa watoto wenye pumu, hupumua Kwa shida Kwa sababu njia ya hewa hushindwa kupitisha hewa kwa sababu ya njia yao kuwa imehathiriwa na hali ya pumu.

Shambulio la pumu (Asthma attack) ni nini?


Hii ni hali ambayo hutokea wakati njia ya hewa inapo vimba na kuwa nyembamba na inakuwa vigumu kwa hewa kuingia na kutoka kwenye mapafu.

Wakati mwingine njia za hewa zinapokuwa zimevimba hutoa majimaji mfano wa makamasi, hali ambayo husababisha mchakato mzima wa mabadlishano ya hewa katika mapafu kuwa mgumu na hii hali ndo inapelekea tatizo zima la mtotoanapo patwa na pumu kushindwa kupumua vizuri.

Wakati ugonjwa huu unaanza, upumuaji kwa mtoto unaweza kuwa wa kawaida na kuonekana kama vile hakuna tatizo, Lakini kipindi ugonjwa unapoanza, unaweza kuhisi kwamba mtu anapumua kupitia kwenye mrija. Mtoto mwenye pumu anaweza kutoa mlio kama wa filimbi (anapopumua), kukohoa, na kusikia kifua kubana.

Wakati shambulio la ugonjwa wa pumu(asthma attack), hali inaweza kuwa mbaya zaidi kama mtoto hatatumia dawa sahii za pumu. Baada ya kutumia dawa na kupata matibau sahii wakati wa shambulio la ugonjwa wa pumu, njia ya hewa mara nyingi hurudia hali yake ya kawaida, ingawa inaweza kuchukua muda mrefu kidogo wakati mwingine.

Pumu huwapata watu gani?

Pumu ni ugonjwa ambao huwapata watu wengi zaidi ya unavyo weza kufikiri.Karibia watoto milioni sita nchini marekani wanaumwa ugonjwa wa pumu(Hatujui hapa kwetu Tanzania ni idadi gani?)
Ugonjwa wa pumu humpata mtoto mmoja hadi wawili katika kila watoto 10 kwa marekani. Hii ina maana kwamba kama una watoto 20 darasani, watoto 2-4 kati yao wanaweza kuwa na ugonjwa wa pumu.
Ugonjwa wa pumu unaweza kumshika mtu katika umri wowote- kuanzia mtoto mchanga hadi mtu mzima-lakini huwashika zaidi watoto wenye umri wa kwenda shule(kuanzia miaka sita na kuendelea)

Hakuna anayejua kwa uhakika kwa nini ugonjwa huu unampata mtu mmoja na kuacha mwingine, lakini tunajua kwamba ugonjwa wa pumu unatokea ndani ya familia zetu. Hii ina maana kwamba kama mtoto ana pumu, yeye pia anaweza kuwa na mzazi, ndugu, mjomba au jamaa mwingine mwenye pumu au alikuwa na ugonjwa huu wakati bado mtoto.

Ugonjwa wa pumu unapoanza,huonyesha kama vile ni mafua,ambayo huambatana na kikohozi chenye kutoa mlio wa filimbi,lakini ugonjwa wa pumu siyo wa kuambukizwa. Huwezi kuambukizwa Kama unavyopata mafua

Ni sababbu zipi zinazopelekea Kupata shambulio la ugonjwa wa pumu (Asthma attack)?

Visababishi  hutofautiana kutoka mtoto mmoja hadi mwingine. Sababu zipo nyingi.Baadhi ya watoto huwa na mzio(allergy), kwa vile vitu ambavyo huathiri njia ya hewa. Mara nyingi vitu vinavyoleta mzio kwa watoto wenye pumu ni vijidudu vidogo jamii ya mchwa vinavyopatikana kwenye vumbi, harufu mbaya (kama ulikuwa karibu na dimbwi na kuvuta harufu hiyo), mbelewele(pollen) kutoka mitini, majani na kwenye magugu.

Watoto wengi hupata shambulio la pumu wanapokuwa karibu na wanyama wenye manyoya kama Paka na mbwa,baadhi watoto wanapovuta hewa iliyochanganyika na chembechembe za manyoya hawa wanaweza pata shambulio la pumu.

Visababishi vingine ni pamoja na marashi(perfumes), vumbi la chaki, na uvutaji wa sigara. Uvutaji wa sigara sio mzuri hasa kwa mtu mwenye pumu.

Wakati mwingine maambukizi mbalimbali yanaweza kusababisha kulipuka kwa ugonjwa wa pumu,maradhi kama mafua, Kwa baadhi ya watoto, hali ya hewa yenye baridi inaweza kusababisha kulipuka kwa ugonjwa huo,baadhi ya watoto hupatwa na matatizo ya pumu wanapokuwa wanafanya mazoezi,hii ni aina ya pumu inayosababishwa na mazoezi.

Jinsi gani unaweza kutibu ugonjwa wa pumu kwa watoto?

Watoto wenye ugonjwa wa pumu wanatakiwa kujaribu kuepuka visababishi vyote vinavyoweza kuwasababishia shambulio la hewa.Ingawa kuna baadhi ya visababishi kama vumbi la chaki ni vigumu kuviepuka katika mzaizngira yetu hasa shuleni,lakini mtoto,wazazi na walimu wajaribu kuwasaidia watoto wenye matatizo haya.

Sura ya ugonjwa wa pumu hutofautiana kutoka kwa mtoto mmoja hadi mwingine, hivyo kuna dawa mbalimbali za kutibu ugonjwa wa pumu,na matibabu haya hutofautiana kati ya mtoto mmoja na mwingine hii ni baada yake daktari kujaribu kufuatilia sababu zilizopelekea ugonjwa huo, ni kwa kasi gani ugonjwa umetokea, na kiwango cha madhara ya ugonjwa huo. Hapo ndipo ataamua tiba ipi itakuwa sahii na bora kwa mtoto.

Baadhi ya watoto wanatakiwa wameze dawa za pumu mara kwa mara punde wanapopata ugonjwa huu. Hii huitwa dawa ya dharura kwa sababu hufanya kazi ya kufungua njia ya hewa ili mtu aweze kupumua. Watoto wengine wanatakiwa kutumia dawa za kudhibiti ugonjwa wa pumu kila siku,Dawa hizi huzuia shambulio la ugonjwa(asthma attack) kutokea.Kwa hiyo matibabu ya Pumu yanatofautina kutoka mtoto mmoja na mwingine.

Kwa watoto walio wengi ugonjwa wa pumu hupona au hupata nafuu wanapokua wakubwa. Baadhi ya madaktari wanadai kwamba hii hutokea kwa sababu, njia ya hewa hupanuka kadri mtoto anavyokua mkubwa. Njia ya hewa inapopanuka, hewa huingia na kutoka kiurahisi

Baadhi ya watu wazima hupata ugonjwa wa pumu, lakini hii haiwasumbui.Wanariadha wengi katika mbio za olimpiki na magwiji wengine wa michezo wanaweza kuendelea na michezo hata wanapokuwa na ugonjwa wa pumu.

UJUMBE WA KUPELEKA NYUMBANI:


Mzazi au mlezi anayeona mtoto mwenye dalili za ugonjwa wa pumu kama nilivyouelezea hapo juu kitu cha kwanza cha kufanya ni kumwaisha Katika kituo chochote cha Afya au Hospitali iliyo karibu nae.

Na kwa wale watoto walikwisha gundulika tayari na ugonjwa huu wa Pumu ni kuhakikisha wanafuta masharti yote ya Matibabu ili kuzuia shambulio la ugonjwa huu.

Mtoto anayejua mapema kwamba kuna vitu vinamletea madhara katika njia ya hewa au sababu nyingine anaweza kutumia dawa mapema zitakazosaidia kufanya njia ya hewa iendelee kuwa wazi.Mtoto ambaye hupata pumu anapofanya mazoezi anaweza kutumia dawa kabla ya kufanya mazoezi ili waweze kumaliza mbio au michezo vizuri.

Kwa watoto walio wengi ugonjwa wa pumu hupona au hupata nafuu wanapokua wakubwa. Baadhi ya madaktari wanadai kwamba hii hutokea kwa sababu, njia ya hewa hupanuka kadri mtoto anavyokua mkubwa. Njia ya hewa inapopanuka, hewa huingia na kutoka kiurahisi

Baadhi ya watu wazima hupata ugonjwa wa pumu, lakini hii haiwasumbui.Wanariadha wengi katika mbio za olimpiki na magwiji wengine wa michezo wanaweza kuendelea na michezo hata wanapokuwa na ugonjwa wa pumu.

MATIBABU   ASILIA   KWA  WAGONJWA  WA  PUMU
Ipo  mimea  mbalimbali, inayo  tumika  katika  tiba  dhidi  ya  ugonjwa  wa  pumu.
Hii  ni  mimea  iliyo  fanyiwa  utafiti  wa  kisayansi na  kuthibitishwa  kuwa  na  mchango  mkubwa  katika  tiba  dhidi  ya  pumu.
Katika  makala  haya, tutaangalia  baadhi  ya  mimea inayo  tumika  katika tiba dhidi ya  ugonjwa  wa pumu.
Mimea  hiyo  ni  kama  ifuatavyo :
1.   Mmea  wa  Simsim  ama Ufuta : Mmea  wa  ufuta  umethibitishwa  kisayansi kuwa  na  mchango  mkubwa  katika  tiba  dhidi  ya  ugonjwa  wa  pumu. Mbegu  za  ufuta  zina  kiwango  kikubwa  cha  madini  ya  Magnesium, ambayo  ni  muhimu sana  katika  tiba  dhidi  ya  pumu.

 Madini  ya  Magnesium   ni  muhimu  sana  katika  tiba  dhidi  ya ugonjwa  wa  pumu, pamoja  na  matatizo  mengineyo  katika  mfumo  wa  mapafu  na  upumuaji kwa ujumla, kwa  sababu  yanasaidia  kuzuia  kuziba  kwa  njia  za  kusafirisha  hewa  kwenye  mapafu.


JINSI  YA  KUTUMIA  UFUTA KATIKA  TIBA  DHIDI  YA  PUMU

   Mgonjwa anashauriwa,  kula  walau  vijiko  viwili  vikubwa  vya ufuta, mara  tatu  kwa siku, asubuhi mchana  na  jioni  mpaka, atakapo  pata  nafuu. Na  kama  wewe  upo  katika  mazingira hatarishi ya  kupatwa  na  pumu, unashauriwa kujenga  mazoea  ya  kuwa  unakula  ufuta  mara kwa  mara  kila  upatapo nafasi.

2.   LUGOLE : Huu  ni  mmea  wenye  faida  lukuki  kwa  afya  ya  mwanadamu. Mmea  huu  umethibitishwa  kisayansi kuwa  na  uwezo wa  kumsaidia  mgonjwa  wa  pumu  kwa  kiasi  kikubwa  sana.  Mbali  na  pumu, mmea  huu  hutumika  katika  tiba  ya  magonjwa  mengine mengi  kama  vile maumivu  ya  kifua, homa, malaria,ukoma, kipindupindu, anemia, magonjwa  ya  akili, kuzuia  kuchoropoka  kwa  mimba, nakadhalika.
Kujitibu  tatizo  la  pumu, chemsha mizizi  ya  mmea  huu  kisha  tumia  kunywa, kikombe kimoja  mara  mbili  kwa  siku, asubuhi  na  jioni  kwa siku  thelathini. Utapata  matokeo  mazuri  sana.

3.    HAMBAMTI : Hambamti  ni  mti  ulio fanyiwa utafiti  wa  kisayansi na kuthibitika kuwa  na  msaada  mkubwa  kwa  wagonjwa  wa pumu. Mbali na  kutibu  pumu, mmea  wa  Hambamti  unatumika  pia  katika  tiba  dhidi ya  tatizo  la maumivu kwenye  kifua.
 Kujitibu  tatizo  la  pumu  kwa  kutumia  mmea, wa  Hambamti  katamatawi  yaliyo komaa  ya  mti  wa  Hambamti  kisha  chemsha  na  maji  halafu  tumia  kunywa  maji  yake, mara  tatu kwa  siku asubuhi, mchana  na  jioni. Utapata  nafuu  kubwa  sana.  Unaweza  pia  kukausha  matawi  hayo na  kisha  kusaga  kupata  unga  wake, halafu unakuwa  unatumia  kulamba  unga  wake  au  unachemsha  kwenye  maji  ya  moto  au  uji.


4.   KINZASU ;  Huu  ni  mmea  ulio fanyiwa  utafiti  wa  kisayansi  na  kuthibitika  kuwa  na  mchango  mkubwa  katika  tiba  dhidi  ya  pumu. Jinsi  ya  kutumia  mmea  huu katika  tiba dhidi  ya  pumu, chukua  majani  yake, yatwange  kisha  yatwange  halafu chemsha  na  maji, kisha  tumia  kunywa  mara  mbili  kwa  siku  kwa  siku  ishirini  na  moja. Hakika  utapata  matokeo  mazuri  sana.

5.    LUSANGALALA ; Huu  ni mmea ambao  pia  umefanyiwa  utafiti  wa  kisayansi  na  kuthibitika kuwa  na  mchango  mkubwa  sana  katika  tiba  dhidi  ya  ugonjwa  wa  pumu. Kujitibu   ugonjwa  wa  pumu  kwa  kutumia  mmea  huu, mgonjwa anashauriwa  kuchukua  majani  ya  mmea  huu  na  kuyachemsha  kwenye  maji  kisha  kutumia  kwa  kunywa  mara  tatu  kwa  siku  kwa  siku  ishirini  na  moja. Hakika  utapata  matokeo  mazuri  sana.

Mbali  na  kutumika  katika  tiba  dhidi  ya  ugonjwa  wa  pumu. Mmea  wa  Lusangalala  una  tibu  magonjwa  mengineyo  kama  vile; maumivu, homa na  malaria,ukoma, upele,kipindupindu,anemia,magonjwa  ya  zinaa, magonjwa  ya  akili, kuzuia  kuchoropoka  kwa  mimba,mkamba, mapigo  ya moyo  kwenda  mbio  na kutokwa  na  damu  nyingi  wakati  wa  hedhi.

6.    MDAA  :  Huu  pia  ni  mmea  uliothibitika  kisayansi  kuwa  na  mchango  mkubwa  katika  tiba  dhidi  ya  ugonjwa wa  pumu. Mgonjwa  anashauriwa  kuchemsha  mizizi  ya  mmea  huu na  kisha  kutumia  kunywa  mara  tatu  kwa  siku  kwa  muda  wa siku  thelathini. Hakina  utapata  nafuu  kubwa sana.
Mbali  na   kutumika  katika  tiba  dhidi  ya  ugonjwa  wa pumu, mmea  wa  Mdaa, una  uwezo  wa  kutibu  magonjwa  na  matatizo  mbalimbali  ya  kiafya  kama  vile; saratani, kuzuia  kuchoropoka  kwa  mimba ( miscarriage ), homa  ya  manjano, vidonda vya tumbo, ukoma, majeraha, maumivu ya viungo, sumu ya  nyoka, maumivu  ya  kichwa, maumivu  ya  meno na  gonorrhea.
Hiyo  ni  baadhi  ya  mimea,ambayo  ina  mchango  mkubwa  katika  tiba  dhidi  ya  ugonjwa  wa  pumu.
Dawa  za  asili  zitokanazo  na  mimea  hii, zinapatikana  katika  duka  la kuuza  dawa  za  asili  la,   NEEMA  HERBALIST.

Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR  ES  SALAAM, jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING,  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

Wasiliana  nasi  kwa  simu  namba
                  0766  53 83 84.

Kwa  mteja  uliepo jijini  Dar  Es  Salaam, ambae  hauna  nafasi  ya  kufika  ofisini  kwetu, utaletewa  dawa  mahali  ulipo
( HOME  & OFFICE  DELIVERY )

Kwa  wateja  waliopo  mikoani, watatumiwa dawa  kwa njia  ya  mabasi  mbalimbali.

Kwa  wateja  waliopo  Zanzibar, watatumiwa  dawa  kwa njia  ya  usafiri wa  boti.
Kwa  wateja  waliopo Mombasa, watatumiwa dawa  kwa  njia  ya  mabasi ya TAHMEED.

Kwa  wateja  wa  Nairobi, watatumiwa  dawa  kwa  basi  la  DAR EXPRESS.

Na  kwa  wateja  wa  ughaibuni, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  au DHL.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee  kila  siku  katika  blogu  yetu.

                          SIMU :  0766  53  83  84


Facebook :  www.facebook.com/neemaherbalist

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ya  kupata  wapenzi  wa  kike  ama  kuoa  na  wengine  huendelea  na  tabia  hiyo  hata  baada  ya  kuoa .  Zipo  sababu  mbalimbali  zinazo  wapelekea  wanaume  kupiga  punyeto, ila  kubwa  kati  ya  hizo  ni  pamoja  na  kutokuwa  na  wapenzi, kutokuwa  na  wapenzi  wanao  kidhi vigezo  vyao, kuwa  katika  mazingira  yasiyokuwa  na  wanawake  ( mfano  katika  shule  za  sekonda

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS

Dawa ya TONSILS ni (kugargar)  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto. Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia. Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako. Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafanya ka

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na  kuwa  mgumu  kama  msumari. Na  hatua  ya  pili   ni  lazima, uume  wake  uendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa  STRONGER  AND  LONGER  ERECTION JINSI  HATUA  ZA  KUSIMAMA  KWA  UUME  ZINAVYO  TOKEA. 1. HATUA    YA  KWANZA: DAMU  KUTIRIRIKA  KWA