Skip to main content

Sarah Nkuki : Mwanamitindo Chipukizi mwenye ndoto za kufika mbali katika fani ya mitindo.




Fani  ya  mitindo  inazidi  kukua  kwa  kasi  nchini  Tanzania, huku  wasichana  wengi  wakijitokeza  kuonyesha  vipaji  vyao  katika  fani  ya  mitindo.  Sarah  Nkuki,( 19 )  mkaazi  wa  Iringa, ni miongoni  mwa  mabinti  wa  kitanzania  wanao  jitokeza  kuonyesha  mapenzi  makubwa  katika  fani  ya  mitindo.




Akiwa  mtoto  wa  mwisho  kati  ya  watoto  watatu  kwa  upande  wa  baba  na  mama  yake, Sarah  anasema  ameanza  kuhusudu   kuwa  mwanamitindo  tangu  akiwa  anasoma  shule  ya  msingi.
Kwa  sasa, Sarah  anachukua  Certificate  ya  Inforamation Technology ( IT)  katika  chuo  kimoja  kilichopo  mjini  Iringa.














Katika  tasnia  ya  mitindo, Sarah  anavutiwa  zaidi  na  Hamisa  Mobeto  kwa  hapa  Tanzania, na  nje  ya  nchi  anavutiwa  na  Naomi  Campbell.
Sarah  anasema  changamoto kubwa  anayo  ipata ni  kutokuwa  na  management  nzuri  itakayo  weza  kusimamia  kazi  zake  na  kumuendeleza   katika  fani  ya  mitindo.












Makala  haya  yameandaliwa  na  Neema  Herbalist  Blog  kwa  udhamini  wa  NEEMA  HERBALIST  & NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  duka  linalo  jihusisha  na  uuzaji  wa  dawa  mbalimbali  za  asili, linalopatikana  UBUNGO  jijini  DAR  ES  SALAAM, jirani  na  Shule  Ya  Msingi  Ubungo  National  Housing  nyuma  ya  jengo  la  Ubungo  Plaza

Comments