Skip to main content

BAADHI YA MAGONJWA YA WATOTO YA KUAMBUKIZA NA MATIBABU YAKE


SHAYIRI



TETEKUWANGA:
Ugonjwa wa tetekuwanga husababishwa na vijidudu vidogo sana aina ya vijasumu. huanza wiki 2 hadi 3 baada ya mtoto kukaa na mtoto mwingine ambaye tayari anao ugonjwa huu.
Kwanza kabisa, madoadoa au vipele vidogo sana vyekundu na ambavyo huwasha, huanza kutokea.
Hivi, hubadilika na kuwa malengelenge na mwishowe, kufanya ganga vyote kwa wakati mmoja.
Kawaida huanza kwenye mwili na baadaye hutokea kwenye uso, mikono na miguu.
Kunaweza kukawa na vipele, malengelenge, na ganga vyote kwa wakati mmoja. Kwa kawaida homa ni kidogo tu.

Tiba:

Ugonjwa hupona baada ya wiki moja. Mkogeshe mtoto kila siku kwa sabuni na maji ya uvuguvugu ili kupunguza kuwasha. Tumia nguo baridi zilizoloweshwa kwenye maji yaliyotokana na shayiri iliyochemshwa na kukamuliwa.
Kata kucha za mikono ziwe fupi kabisa. Kama ganga zinapata ugonjwa, paka gentia violet (g.v) au mafuta ya kuua vijidudu.

SURUA
Ugonjwa huu mkali ambao husababishwa na vijasumu pia ni wa hatari sana kwa watoto wenye utapiamlo au kifua kikuu.
Huanza siku 10 baada ya kukaa karibu na mtu mwenye surua, kwa dalili za mafua homa, makamasi, macho mekundu na kikohozi.
Mtoto huzidi kuwa na hali mbaya. Mdomo unaweza kuwa na vidonda sana na anaweza akaanza hata kuharisha.
Baada ya siku mbili au tatu, madoadoa meupe kama chembe za chumvi hutokea mdomoni. Siku ya kwanza na ya pili baadaye, vipele hutokea. Kwanza kabisa, nyuma ya masikio kwenye shingo, halafu kwenye uso na kwenye mwili na mwisho kabisa, hutokea kwenye mikono na miguu.
Baada ya vipele kutokea, kwa kawaida mtoto huanza kupata nafuu. Vipele huchukua siku tano.

MATIBABU:
Mtoto ni lazima apumzishwe kitandani, apepeswe maji ya kutosha na chakula bora. Kama mtoto hawezi kunyonya kutoka kwa mama, basi mpe mtoto maziwa yaliyokamuliwa kutoka kwa mama kwa kijiko.
Kwa homa na maumivu, toa "asetominofeni" au asprini. Kama anapata ugonjwa wa sikio, toa dawa ya kuua vijidudu.
Kama dalili za kichomi, ugonjwa wa uti wa mgongo au maumivu makali ya sikio au tumbo yanatokea, tafuta msaada wa mganga haraka sana.

KINGA YA SURUA.
Watoto wenye surua ni lazima wakae mbali na watoto wazima. Hasa ni muhimu sana kujaribu kuwazuia watoto wenye utapiamlo au mwenye kifua kikuu au ugonjwa mwingine wa muda mrefu kuchanganyika na watoto wazima.
Watoto kutoka familia zingine wasiruhusiwe kwenda nyumba ambayo kuna surua.
Ikiwa watoto wengine kwenye familia ambayo kuna ugonjwa wa surua, bado hawajaugua surua, ingefaa wasiruhusiwe kwenda shuleni, sokoni au madukani kwa muda wa siku kumi.
Ili kuzuia surua isiwauwe watoto, hakikisha kuwa wanakula chakula bora na cha kutosha. Watoto wazindikwe kuzuia surua wakati wanapofikia umri wa miezi nane hadi kumi na nne.

SURUA YA KIJERUMANI (German measles or Rubella).
Surua ya Kijerumani si kali kama surua ya kawaida, huchukua siku tatu au nne. Vipele vichache mara nyingi tezi zilizo nyuma ya kichwa na shingo huvimba na kuuma.
Mtoto ni lazima apumzike kitandani na atumie asprini kama ni lazima.
Wanawake ambao huugua surua ya Kijerumani katika miezi mitatu ya kwanza ya mimba wanaweza wakajifungua watoto wenye hitilafu au kilema.
Kwa sababu hii, wanawake wenye mimba ambao hawajawahi kuugua surua ya Kijerumani au hawana uhakika ni lazima wakae mbali sana na watoto wenye aina hii ya surua.

MUMPS
Dalili ya kwanza huanza wiki mbili au tatu baada ya kukaa karibu na mtu ambaye ana mumps.
Mumps huanza kwa homa na maumivu wakati wa kufungua kinywa au kula, baada ya siku mbili uvimbe laini hutokea chini ya masikio kwenye pembe za taya. Kwanza, upande mmoja na baadaye upande mwingine.

TIBA:

Uvimbe hupona wenyewe baada ya siku 10 bila hata ya kutumia dawa.
Aspirini inaweza kutumiwa kwa sababu ya homa na maumivu, mpe mtoto chakula bora kilicho na maji maji na weka kinywa chake safi wakati wote.

HATARI:
Kwa watu wazima na watoto walio na umri zaidi ya miaka kumi na moja, huweza kukawa na maumivu ya tumbo au uvimbe unaouma kwenye makende(wanaume) au matiti (wanawake).
Watu wenye uvimbe huu ni lazima wapumzike kitandani kabisa na kuweka mabonge ya barafu au nguo baridi zilizolowanishwa kwenye sehemu zilizovimba ili kusaidia kupunguza maumivu na uvimbe.
Kama dalili za ugonjwa wa uti wa mgongo zinatokea jaribu kupata msaada wa mganga.

KIFADURO:
Kifaduro hutokea wiki moja au mbili baada ya kukaa karibu na mtu aliye nacho. Huanza kama mafua kwa homa, makamasi hutoka puani, na kikohozi.
Wiki mbili baadaye, kifaduro hutokea.

Ghafla, mtoto huanza kukohoa haraka haraka sana bila ya kuvuta pumzi mpaka kohozi linapovutika hutoka, na hewa huingia haraka kwenye mapafu yake kwa mlio wa ajabu unaoitwa kifaduro.
Baada ya hiki kifaduro, anaweza kutapika katikati ya nyakati hizi za kukohoa mtoto huwa mzima kabisa.
Kifaduro huchukua miezi 3 au zaidi.
Kifaduro ni cha hatari hasa kwa watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja kwa hiyo wazindikwe mapema.
Watoto wadogo hawapati kikohozi chenye kifaduro kamili kwa hiyo ni vigumu kuwa na uhakika kama wana kifaduro au hapana.
Ikiwa mtoto mchanga anazimia anapokohoa au macho yake yamevimba panapokuwepo wagonjwa wa kifaduro kwenye sehemu yake mtibu kama mgonjwa wa kifaduro mara moja.

TIBA:
Katika hatua za mwanzo za kifaduro, erythoromycin, tetracyline au ampisilini zinaweza kusaidia. Chroramphenicol husaidia pia lakini, ina hatari zaidi. Ni muhimu.
Kwa wagonjwa wa kifaduro ambao wamezidiwa sana, phenobarbital inaweza kusaidia hasa ikiwa kikohozi kinamzuia kulala au kinasababisha degedege.
Ili kuzuia kupungua kwa uzito na hatimaye utapiamlo, ni lazima mtoto apate chakula bora na ale mara baada ya kutapika.
Wakinge watoto wako wasipatwe na kifaduro hakikisha kuwa wanazindikwa kuzuia kifaduro wanapofikia umri kutokifunga.

DIPHTHERIA.
Ugonjwa huu huanza kama mafua na homa, kuumwa na kichwa na maumivu ya koo. Ganga lililo kama ngozi la rangi ya kijivujivu au njano huweza kutokea kwenye koo na mara nyingine kwenye pua au midomo. Pumzi hunuka sana.
Ikiwa unashuku kuwa mtoto ana Diphtheria:-

Mweke kitandani kwenye chumba tofauti na watu wengine.
Tafuta msaada wa mganga haraka sana. Kuna dawa maalum (antitoxin) kwa diphtheria.
Toa penisilini kidonge kimoja cha uniti 400,000 mara tatu kila siku kwa watoto wakubwa

asukutue mdomo kwa maji yenye chumvi kidogo, Avute mvuke wa maji moto mara kwa mara.
Kama mtoto anaanza kupaliwa au kugeuka rangi na kuwa bluu, jaribu kuondoa ganga kutoka kwenye koo ukitumia kitambaa cha nguo kwenye vidole vyako.
Diphtheria ni ugonjwa wa hatari unaoweza kuzuiliwa kwa urahisi kabisa kwa zindiko la DPT hakikisha kuwa watoto wako wamezindikwa.

POLIO (ugonjwa wa kupooza wa watoto):
Polio hutokea zaidi kwa watoto walio na umri chini ya miaka miwili.
Ugonjwa huu unaosababishwa na vijidudu vya virus, huanza kama mafua kwa homa, hutapika na maumivu ya misuli.

Mara nyingine, hizi ndizo dalili zinazoonekana tu.
Lakini, wakati mwingine sehemu fulani ya mwili hulegea au kupooza.
Mara nyingi hii hutokea kwenye mguu au mkono mmoja. Baada ya muda mguu au mkono uliopooza huwa mwembamba na haukui kwa haraka kama huo mwingine.

TIBA:
Ikiwa ugonjwa umekwishaanza hakuna dawa itakayoweza kuondoa kupooza. Dawa za kuua vijidudu hazisaidii. Tuliza maumivi kwa asprini au astaminofeni na kukanda misuli inayouma kwa maji moto.

KINGA:

Mweke mtoto mgonjwa kwenye chumba tofauti mbali na watoto wengine. Mama ni lazima anawe mikono kila mara baada ya kumgusa. Kinga iliyo nzuri kuliko zote kwa polio, ni zindiko la polio.
Hakikisha kuwa watoto wamezindikwa kuzuia polio kwa matone akiwa na umri wa miezi miwili, mitatu na minne.

Mtoto aliyelemazwa na polio ni lazima ale chakula bora na kufanya mazoezi ili kuipa nguvu misuli iliyobaki. Kwa mwaka wa kwanza, nguvu inaweza kurudi kidogo.
Msaidie mtoto ajifunze kutembea kwa jinsi anavyoweza. Weka nguzo mbili ili aweze kuegemea. Baadaye, mtengenezee magongo ya kutembelea.

IMEANDALIWA  NA  NEEMA  HERBALIST. SIMU  0766538384

Comments

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ...

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na...

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS

Dawa ya TONSILS ni (kugargar)  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto. Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia. Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako. Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafany...