Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2014

BAADHI YA MAGONJWA YA WATOTO YA KUAMBUKIZA NA MATIBABU YAKE

SHAYIRI TETEKUWANGA : Ugonjwa wa tetekuwanga husababishwa na vijidudu vidogo sana aina ya vijasumu. huanza wiki 2 hadi 3 baada ya mtoto kukaa na mtoto mwingine ambaye tayari anao ugonjwa huu. Kwanza kabisa, madoadoa au vipele vidogo sana vyekundu na ambavyo huwasha, huanza kutokea. Hivi, hubadilika na kuwa malengelenge na mwishowe, kufanya ganga vyote kwa wakati mmoja. Kawaida huanza kwenye mwili na baadaye hutokea kwenye uso, mikono na miguu. Kunaweza kukawa na vipele, malengelenge, na ganga vyote kwa wakati mmoja. Kwa kawaida homa ni kidogo tu. Tiba: Ugonjwa hupona baada ya wiki moja. Mkogeshe mtoto kila siku kwa sabuni na maji ya uvuguvugu ili kupunguza kuwasha. Tumia nguo baridi zilizoloweshwa kwenye maji yaliyotokana na shayiri iliyochemshwa na kukamuliwa. Kata kucha za mikono ziwe fupi kabisa. Kama ganga zinapata ugonjwa, paka gentia violet (g.v) au mafuta ya kuua vijidudu. SURUA Ugonjwa huu mkali ambao husababishwa na vijasumu pia ni wa hatari sana kwa wa...

ZIJUE FAIDA ZA KIAFYA ZA APPLE, NDIZI MBIVU, MAHARAGE, KABICHI, KAROTI, KAHAWA NA VYAKALA VYA NAFAKA.

APPLE (Tufaha) • Dawa nzuri ya ugonjwa wa moyo • Hushusha kolestro • Hushusha shinikizo la damu • Huimarisha kiwango cha sukari katika damu • Huongeza hamu ya kula • Linakemikali yenye uwezo wa kuzuia saratani • Juisi yake inaua virusi vinavyoambukiza magonjwa BANANA (NDIZI MBIVU) • Huzuia na kutibu vidonda vya tumbo • Hushusha kolestrol katika damu BEANS (MAHARAGE YA AINA ZOTE) • Hupunguza aina mbaya ya mafuta mwilini • Hudhibiti kemikali mbaya za saratani • Hudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu • Hushusha shinikizo la damu • Hurekebisha mwenendo wa utumbo mkubwa • Huzuia na kutibu ukosefu wa choo • Huzuia kutokwa damu kwenye haja kubwa (haemorrhoids) na matatizo mengine ya tumbo CABBAGE (KABICHI) • Hupunguza hatari ya kupata saratani, hasa ya utumbo • Huzuia na kutibu vidonda vya tumbo (hasa juisi yake) • Huchangamsha mfumo wa kinga ya mwili • Huua bakteria na virusi mwilini • Huharakisha ukuaji wa mwili CARROT (KAROTI) • Inaaminika kuzuia s...

Ijue Faida ya kula samaki

SAMAKI (FISH) •  Huyayusha damu, huifanya kuwa nyepesi• Huilinda mishipa ya damu isiharibike• Huzuia damu kuganda• Hushusha shinikizo la damu• Hupunguza hatari ya kupatwa na mshituko wa moyo na kiharusi• Hutuoa ahueni kwa wenye ugonjwa wa kipandauso• Husaidia kuzuia uvumbe mwilini• Huendesha mfumo wa kinga ya mwili• Huzuia saratani• Hutoa ahueni kwa wenye pumu• Hupambana na dalili za awali za ugonjwa wa figo• Huongeza nishati ya ubongo KITUNGUU SAUMU (GARLIC) •  Hupambana na maambukizi• Ina kemikali zenye uwezo wa kudhibiti saratani• Hufanya damu kuwa nyepesi• Hupunguza shinikizo la damu na kolestro• Huamsha mfumo wa kinga ya mwili• Huzuia na kutoa ahueni kwa kikohozi kilaini.• Huweza kutumika kama dawa ya kifua TANGAWIZI (GINGER) •  Huzuia ugonjwa wa kutetemeka• Hufanya damu kuwa nyepesi ZABIBU (GRAPE) • ina uwezo wa kufanya  virusi  visifanyekazi • Huzuia meno kuoza•  Ina mchanganyiko wenye uwezo wa kuzuia saratani PILIPILI HOHO (GREEN ...

KULA NYANYA UJIEPUSHE NA KIHARUSI

SOTE tunajua ugonjwa wa kiharusi (stroke) ni miongoni mwa magonjwa hatari kwani ukikupata unaweza kudhoofisha baadhi ya viungo vyako vya mwili kama siyo vyote na kukufanya ushindwe kufanya kazi zako za kawaida na kuwa mtu wa ndani tu kwa maisha yako yote. Lakini unaweza kujiepusha na ugonjwa huo hatari kwa kuzingatia ulaji wa vyakula sahihi pamoja na kufanya mazoezi. Utafiti wa hivi karibuni umebaini kwamba nyanya (tomatoes) hutoa kinga mwilini dhidi ya ugonjwa wa kiharusi au kupooza kama unavyojulikana na wengine. Hivi karibuni, watafiti wa nchini Finland walifanya utafiti wa kina na kutoa taarifa kuhusu kirutubisho aina ya ‘lycopene’ kinachopatikana kwa wingi kwenye nyanya, matikitimaji na pilipili.  Wamesema katika taarifa yao kuwa watu zaidi ya 1,000 waliowafanyia utafiti wenye kiwango kingi cha ‘lycopene’ kwenye mfumo wa damu zao, hawakuonesha dalili kabisa za kupatwa na kiharusi. Aidha, Chama cha Taifa cha wenye Kiharusi cha nchini Marekani (The Nati...

UTAFITI : Machungwa, Zabibu Hupunguza Uwezekano wa Kupata Kiharusi?

Utafiti mpya uliofanyika nchini Marekani umesema ya kwamba kula machungwa na zabibu kunaweza kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi ( Stroke ). Utafiti huo uliangalia faida za matunda chachu (Citrus Fruit) pekee kwa mara ya kwanza tofauti na tafiti nyingi ambazo tumezizoea zinazoangalia umuhimu wa matunda na mboga za majani kwa afya kiujumla. Utafiti huu umehusisha maelfu ya wanawake wanaoshiriki katika tafiti ya manesi Nurse’s Health Study lakini wataalamu wanaamini faida hizo za machungwa na zabibu pia zinapatikana kwa wanaume. Timu ya watafiti katika chuo cha Norwich Medical School katika Chuo Kikuu cha East Anglia wamechunguza umuhimu wa kemikali aina ya flavonoids ambayo ni jamii ya antioxidant (kemikali zinauwa kemikali hatari za kwenye mwili) inayopatikana katika matunda, mboga za majani, chocolate nyeusi na wine nyekundu. Utafiti huu ulifuatilia takwimu za miaka 14 za wanawake 69,222 ambao walikuwa wakishirki katika tafiti kwa kuandika kiwango chao cha kula matund...