Skip to main content

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS





Dawa ya TONSILS ni (kugargar) kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto.

Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia.

Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako.

Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafanya kazi na mdomo uko wazi basi pia unaweza kuumwa na Tonsils.

Vile vile kutoka nje kwenye joto kisha ukaingia pahala baridi huwa inasababisha Tonsils na maradhi mengine kama flu na kuumwa na kichwa..n.k

Au hii Dawa ya Maradhi ya Tonsils. Tonsil husababishwa na sababu nyingi tu. Pia husababishwa na upungufu wa white blood cells katika mwili ambazo cells hizi ndio hupigana na vidudu vyote venye kuleta maradhi ndani ya mwili sasa vinaposhindwa kufanya kazi lymph zinavimba na husababisha Tonsils.

Kila mtu na ukuwaji wake wa mwili, wapo ambao wanapata tonsils kwa kunywa maji ya baridi ambayo maji ya baridi huwa ni moja katika chanzo cha kupata tonsils, mavumbi huchangia vile vile pilipili na vitu vikali kama vile embe mbichi limau pia huwa ni sababu kuu ya kupata tonsil.

Wakati unapokuwa na tonsils muhimu zaidi kuacha maji ya baridi na vitu vyote vikali, zaidi utumie maji ya moto .
.
  Dawa  ya  asili  ya  maradhi  ya  tonsils  ambayo  hufanya  kazi  mara  moja  ni  hii  hapa  chini.
 : Kamua ndimu moja katika glass yako kisha tia maji ya Uvuguvugu (warm water) na baadae tia vijiko vinne vidogo vya asali na kijiko robo cha chumvi kuroga uzuri na unywe pole pole.


MAKALA   HAYA   YAMEANDALIWA   NA   NEEMA  HERBALIST. TUNAPATIKANA   JIJINI   DAR   ES   SALAAM  KWA  SIMU  0766538384.

Comments

  1. Assalamualaikum Mimi matonsis yananisukbua nataka kutumia iyo dawa lakini asali ukitumia na ndimu wanasema ni simu ,je ni kweli?

    ReplyDelete
  2. Habari jaman mm.usiku ndo huwa nabanwa sana mpaka nakohoa je tatizo ni nini

    ReplyDelete
  3. Habar,mmm pia nasumbuliwa na tonsils asante kwa dawa nitatumia ila unatumia kwa muda gani???

    ReplyDelete
  4. Me mpaka sasa yananisumbua nikienda hospital damu safi kichwa kinauma kinaacha na koo haliumi nikimeza mate in kuzito hatar

    ReplyDelete
  5. Koo haliumi lakin nikuzito ninapo meza mate

    ReplyDelete

Post a Comment