GONJWA hatari kuliko UKIMWI, limeuvamia Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, anzania ikiwamo, ambapo waathirika wengi ni watoto, wanaoanzwa kwa kutikisa vichwa kabla ya kupoteza maisha. Kwa mujibu wa watalaamu wa afya, kutikisa kichwa ni dalili za awali za maradhi hayo yanayo itwa kitaalamu “ NODDING DISEASE” au “ NODDING SYNDROME “ na kufuatiwa na mtoto kudumaa kimwili na kiakili, kushindwa kuongea na hatimaye kifo. Wataalamu wa Shirika La Afya Duniani ( WHO ), wanasema maradhi hayo yaliyo anzia Sudan ...