GONJWA
hatari kuliko UKIMWI, limeuvamia Ukanda
wa Afrika Mashariki
na Kati, anzania ikiwamo, ambapo waathirika
wengi ni watoto, wanaoanzwa kwa
kutikisa vichwa kabla
ya kupoteza maisha. Kwa
mujibu wa watalaamu
wa afya, kutikisa kichwa
ni dalili za
awali za maradhi
hayo yanayo itwa
kitaalamu “ NODDING
DISEASE” au “ NODDING
SYNDROME “ na kufuatiwa
na mtoto kudumaa
kimwili na kiakili, kushindwa kuongea
na hatimaye kifo.
Wataalamu
wa Shirika La
Afya Duniani ( WHO
), wanasema maradhi hayo
yaliyo anzia Sudan
miaka ya 1960, kabla
ya kupotea na
kuibuka tena Afrika
Mashariki hivi karibuni
kwa kiasi kikubwa
yanaathiri watoto wenye
umri wa kati
ya miaka 5
hadi 15. Pia wameitaja
Tanzania kama moja
ya maeneo yenye
maradhi hayo.
Mtoto
anapopatwa na maradhi
hayo kwa mara
ya kwanza, mara nyingi
anaanzwa anapokuwa anakula
chakula. Anapokamatwa na maradhi
hayo, wakati huo akila, hali
hiyo humwachia kwa
muda usiopungua nusu
saa baada ya
kumaliza kula. Kwa mujibu
wa mtaalamu wa
magonjwa ya akili
kutoka Marekani, Dk. Peter
Spencer, maradhi haya humwathiri
mtoto kiakili na
kimwili na mara
nyingi hayamchukui mtoto
zaidi ya miezi
mitatu baadaye hufa.
CHANZO
CHA MARADHI
Chanzo hasa cha
maradhi haya kitaalamu
hakijajulikana, lakini kwa mujibu
wa mtaalamu wa
afya, Profesa James Tumwine
wa Chuo Kikuu
cha Makerere, Uganda aliyeshiriki
katika timu ya
wachunguzi wa WHO
walio fuatilia chanzo
cha maradhi hayo nchini
Sudan, huenda chanzo cha maradhi
hayo ni minyoo
aina ya ONCHOCECRA
VOLVULUS , kwani ilionekana kwa
wingi katika maeneo
yote yaliyo athirika. Minyoo hiyo
inaaminika kuwa huwa
inabebwa na inzi
weusi wanaopatikana kwa
wingi kwenye ardhi oevu. Inakisiwa hivyo
kwa sababu katika
Ukanda wa Afrika Mashariki
na Kati, maeneo yaliyo
athireika ni yale
yanayo patikana na
mito na maeneo
ya majimaji. Dk. Scott Dowell, Mtafiti Mwandamizi
wa Kituo Cha
Utafiti na Udhibiti
wa Magonjwa cha
Marekani ( USCDC ), alisema “
bado ina tatiza , maana katika
Ukanda wa Afrika
Mashariki na Kati, kuna maeneo mengi yenye
minyoo ya Onchocerca
Volvulus, ambayo hayana maradhi
haya “.
Profesa
Andrea Winkler, aliyefanya utafiti
wa maradhi hayo nchini Tanzania, kwa upande
wake, alisema bado chanzo
cha maradhi haya
ni kitendawili, kwa sababu
vyanzo wanavyo dhani
ndivyo visababishi vipo
maeneo mengi ambayo
hayaja athiriwa na
maradhi hayo.
USHUHUDA WA
ALIYE UGUA
Timu ya watafiti
wa WHO iliyo fanya
utafiti wa maradhi
haya katika kijiji
cha Tumangu, kaskazini mwa
Uganda ilikutana na
mzazi wa mtoto
Patrick, 17 aliye athiriwa
na maradhi hayo. Mzazi huyo
Bi. Grace Aber aliiambia
timu hiyo hivi
karibuni kuwa mtoto
wake alianza kushikwa
na tatizo la
kutikisa kichwa, hali iliyo mfanya
awe kama amechanganyikiwa huku
akiwa anazungumza mwenyewe
kabla ya kuanza
kusitisha kuongea. Mama huyo
alisema baada ya
Patrick kukumbwa na
maradhi hayo wiki
moja baadaye dada
yake naye alishikwa
na kuanza kutikisa
kichwa. “ Moyo wangu unaogopa, naomba mtueleze
chanzo cha maradhi
haya ambayo hospitalini
wananiambia hawayajui zaidi
ya kupewa dawa
ambazo hazijasaidia kitu “
alisema mama huyo.
Kwa mujibu wa
Wizara ya Afya
ya Uganda, zaidi ya
watoto 2000, wameathiriwa na
maradhi haya tangu
yalipoibuka mwishoni mwa
mwaka 2012. Wakati
Wizara ya Afya
ya Uganda ikisema
hivyo, nchini Tanzania kwa
mujibu wa Kaimu
Mkurugenzi Msaidizi Ufuatiliaji
na Udhibiti wa
Magonjwa katika wizara
ya Afya , Dk. Janeth
Mghamba , maradhi haya ambayo
yanaonekana kama mapya nchini
Tanzania yaligunduliwa nchini
tangu mwaka 1960. Maeneo
yaliyo athirika ni
Mahenge mkoani Morogoro,
ambako pia kuna
hospitali inayo shughulikia
waathirika wa tatizo
hilo.
MAKALA HAYA
YANATOKA KWENYE GAZETI
LA NYAKATI, TOLEO na. 674,
LA JUMAPILI, OKTOBA 27-NOVEMBA
2, 2013.
Comments
Post a Comment