Rev. John Komanya. |
Mwimbaji
anayetamba na wimbo wa "Zawadi gani nitamtolea BWANA" ambaye pia ni
mtume akichunga kanisa jijini Dar es Salaam John Komanya amepata ajali mbaya
juzi mchana maeneo karibu na daraja la Mto Wami akiwa njiani kuelekea mkoani
Arusha kukutana na viongozi wanaohudumu na mwalimu Christopher Mwakasege, kwa
ajili ya mkutano wa injili ambao utakuwa na lengo la kuombea taifa kwa siku nne
mwezi Disemba.
Akizungumza
na GK mtume Komanya amesema lengo lilikuwa ni kupeleka barua kwa viongozi hao
ili wamfikishie mwalimu Mwakasege kwaajili ya mkutano huo. Amesema akiwa njiani
katikati ya Msata na Wami na wakati huo hakuwa amefunga mkanda wa gari, ndipo
akasikia sauti ya Roho Mtakatifu ikimwambia kwa upole afunge mkanda lakini
akawa anapuuzia na kuanza kujiuliza kwanini, sauti ikarudia tena kwa upole
ikimwambia afunge mkanda akiwa bado anajiuliza ndipo anasema akasikia sauti ya
Mungu ikizungumza kwa haraka na ukali "John funga mkanda" ndipo
akafunga mkanda.
Mtume
Komanya amesema akiwa anateremka kuelekea wami akiwa katika mwendo wa 180
wakati akipita katika kona kulikuwa na malori matatu mbele yake kukawa na lori
lingine likifuatiwa na mabasi matatu yakipandisha kutoka Arusha kuja Dar, kwa
wakati huo aliona malaika saba ambapo walishuka mithili ya makomandoo
washukavyo kutoka kwenye kamba ya helikopta, mmoja akiwa amekaa kwenye boneti
mbele, mwingine kulia, kushoto na mwingine nyuma yake ambaye alimwambia Komanya
afuate maelekezo yake, anasema akiwa anamwangalia malaika aliyekaa karibu naye
katika kiti cha dereva aliambiwa afuate maelekezo anayopewa na malaika wa nyuma
yake.
Alipokuwa
akiangalia mbele akaona gari linayapita mengine kwa spidi hali iliyomfanya
Komanya kutaka kuingia katikati ya magari mengine lakini malaika akamwambia
afuate maelekezo yake na kuambiwa aachie uskani jambo ambalo alilipinga kwakuwa
aliona kifo mbele yake na kutaka kuingia katikati ili kukwepa, lakini malaika
akamwambia ukiingia katikati utakufa, wewe achia usukani kama ninavyokwambia
kwakuwa wametumwa kumlinda, akawa bado anatafakari kutokana na kuliona korongo
kubwa upande wake huku malaika wakimwambia asiguse kitu chochote ikiwemo
kutokanyaga breki lakini bila kusikia akakanyaga na kusababisha gari kuyumba
sana, malaika akamwambia tena aachie breki na kuweka mikono yake kifuani.
Anasema alipoweka mikono kifuani aliona wakiligonga lori huku malaika akiwa
ameshika usukani na kuonyonga sana huku yeye akisema alijikuta akiwekwa kwenye
kitu kama chupa ya maji, na yeye kwa wakati huo kuona kama vile yupo ndani ya
glasi ya maji, ila anaona kinachoendelea.
Kisha
baada ya hapo, upande wake wa usukani ndio uliogongwa, mara baada ya malaika
kuchezesha usukani kidogo ili kuepusha madhara zaidi, na kisha ile
semi-trailler ikamtupia kwenye korongo na kubinuka mara tatu hewani kabla ya
kutua chini kwa mara ya nne, ambapo gari ilikuwa juu chini, yaani matairi
yakiwa yanatazama juu.
Baada
ya hapo kilichofuata ni kuendelea kusikiliza malaika wasemacho, ambapo hapo
alisikia sauti ikisema fungua mkanada utoke, na kwa wakati huo kulikuwa na
moshi ullioanza kutoka kwenye gari - na hapo akapewa dakika 12 kuchukua baadhi
ya vitu alivyokuwa navyo kwenye gari. Maajabu ya Mungu, hakuna kitu chochote
kilichogusa mwili wake, na wala hakuna damu iliyovuja kutokana na gari hilo
kupindukia kwenye korongo.
Hakika
utukufu ulimrudia Mungu kwa wakati huo kwani baadhi ya mashuhuda walikiri
hapohapo ya kwamba hakuna mtu anayeweza kusalimika kwenye ajali hiyo, bali ni
lazima tu mkono wa Mungu umehusika hapo kuokoa.
Baadhi
ya mashuhuda ambao walikuwapo kwenye mabasi ya mkoa (hadi mkoa) walimtambua
mtumishi wa Mungu ya kwamba ni John Komanya na hatumaye kumshukuru Mungu
hapohapo, ambapo baadae Polisi walifika kwa ajili ya kazi yao - lakini hilo
halikumzuia Mchungaji Komanya kupiga magoti na kumshukuru Mungu licha ya umati
wa watu - na tukio hilo liliambatana na yeye kuisikia sauti ya Mungu ikimwambia
"Nimekupa kazi ya kutengeneza kanisa langu,... usiogope nitakulinda,
ila kuwa mwaminifu na nitakuweka kwenye uaminifu"
Sauti
hiyo ilitoka kwa kiumbe ambacho kilikuwa na muonekano wa malaika, Pastor
Komanya anaieleza GK na kusema kuwa sauti yake ilikuwa ya tofauti, na mavazi
yake yalikuwa ni meupe na kwamba alielezwa dhahiri kuwa hiyo semi trailer
ilikuwa imetumwa kummaliza, lakini ndio maana malaika walitumwa kumlinda.
"Zawadi
Gani" kama ambavyo alikuwa akiitwa akiwa hospitali ya Muhimbili,
alifanyiwa vipimo na kuonekana ya kwamba hana shida yoyote. Na hili
linadhihirika hata pale alipotoka kwenye gari lililopiinduka, kwa kuwa alitoa
vifaa vyake na kuanza pia kupiga picha, picha ambazo kama mtu akiziona zote,
hakika hawezi kuamini kama kuna kusalimika hapo.
Mwisho
wa yote Mchungaji Komanya anakiri kuwa amepona kwa rehema ya Mungu, na baada ya
hapo amemuahidi kumtumikia kwa kazi aliyompa licha ya kwamba ni ngumu na ina
vikwazo vingi. Jumapili hii, Mchungaji Komanya ataimba wimbo mpya kumshukuru
Mungu kutokana na kumuepusha na kifo. Kwa wasafiri wote, hapa kuna funzo la
kujikabidhi mikononi mwa BWANA kila mara safari inapotokea, katu tusienende kwa
mazoea.
INATOKA : www.gospelkitaa.blogspot.com
Comments
Post a Comment