Skip to main content

GONJWA LA KUTIKISA KICHWA LAVAMIA AFRIKA MASHARIKI

GONJWA  hatari  kuliko  UKIMWI, limeuvamia  Ukanda  wa  Afrika  Mashariki  na  Kati, anzania  ikiwamo, ambapo  waathirika  wengi  ni  watoto, wanaoanzwa  kwa  kutikisa  vichwa  kabla  ya  kupoteza  maisha. Kwa  mujibu  wa  watalaamu  wa  afya, kutikisa  kichwa  ni  dalili  za  awali   za  maradhi  hayo  yanayo  itwa  kitaalamu    NODDING  DISEASE”  au  “ NODDING  SYNDROME “  na  kufuatiwa  na  mtoto  kudumaa  kimwili  na  kiakili, kushindwa  kuongea  na  hatimaye  kifo.

Wataalamu  wa   Shirika  La  Afya  Duniani  (  WHO ), wanasema  maradhi  hayo  yaliyo  anzia  Sudan  miaka  ya  1960, kabla  ya  kupotea  na  kuibuka   tena  Afrika  Mashariki   hivi  karibuni  kwa  kiasi  kikubwa  yanaathiri    watoto  wenye  umri   wa  kati  ya  miaka  5  hadi  15. Pia  wameitaja  Tanzania  kama  moja  ya  maeneo  yenye  maradhi  hayo.

Mtoto  anapopatwa  na   maradhi  hayo  kwa  mara  ya  kwanza, mara  nyingi  anaanzwa  anapokuwa  anakula   chakula. Anapokamatwa  na  maradhi  hayo, wakati  huo  akila, hali  hiyo  humwachia  kwa  muda  usiopungua  nusu  saa  baada  ya  kumaliza  kula. Kwa  mujibu  wa  mtaalamu  wa  magonjwa  ya  akili  kutoka  Marekani,  Dk. Peter  Spencer, maradhi  haya  humwathiri  mtoto  kiakili  na  kimwili  na  mara  nyingi  hayamchukui  mtoto  zaidi  ya  miezi  mitatu  baadaye  hufa.

                                CHANZO  CHA  MARADHI

Chanzo  hasa  cha   maradhi  haya  kitaalamu  hakijajulikana, lakini  kwa  mujibu  wa  mtaalamu  wa  afya, Profesa  James  Tumwine  wa  Chuo  Kikuu  cha  Makerere, Uganda  aliyeshiriki  katika  timu  ya  wachunguzi  wa  WHO  walio  fuatilia  chanzo  cha  maradhi hayo  nchini  Sudan, huenda   chanzo cha  maradhi  hayo  ni  minyoo  aina  ya  ONCHOCECRA  VOLVULUS , kwani  ilionekana  kwa  wingi  katika  maeneo  yote  yaliyo  athirika. Minyoo  hiyo  inaaminika  kuwa  huwa   inabebwa  na  inzi  weusi  wanaopatikana  kwa  wingi  kwenye   ardhi  oevu. Inakisiwa  hivyo  kwa  sababu  katika  Ukanda wa  Afrika  Mashariki  na  Kati, maeneo  yaliyo  athireika  ni  yale  yanayo  patikana  na  mito  na  maeneo  ya  majimaji. Dk. Scott  Dowell, Mtafiti  Mwandamizi  wa  Kituo  Cha  Utafiti  na  Udhibiti  wa  Magonjwa  cha  Marekani  ( USCDC ), alisema    bado  ina  tatiza , maana  katika  Ukanda  wa  Afrika  Mashariki  na  Kati, kuna maeneo  mengi yenye  minyoo  ya  Onchocerca  Volvulus, ambayo  hayana  maradhi  haya “. 

Profesa   Andrea  Winkler, aliyefanya  utafiti  wa  maradhi  hayo   nchini Tanzania, kwa  upande  wake, alisema  bado  chanzo  cha  maradhi  haya  ni  kitendawili, kwa  sababu  vyanzo  wanavyo  dhani  ndivyo  visababishi  vipo  maeneo   mengi  ambayo  hayaja  athiriwa  na  maradhi  hayo.

 

                      USHUHUDA   WA  ALIYE  UGUA

Timu  ya  watafiti  wa WHO  iliyo  fanya  utafiti  wa  maradhi  haya  katika  kijiji  cha  Tumangu, kaskazini  mwa  Uganda  ilikutana  na  mzazi  wa  mtoto   Patrick, 17  aliye  athiriwa  na  maradhi  hayo. Mzazi  huyo  Bi. Grace  Aber  aliiambia  timu   hiyo  hivi  karibuni  kuwa  mtoto  wake  alianza  kushikwa  na  tatizo  la  kutikisa  kichwa, hali iliyo  mfanya  awe kama  amechanganyikiwa   huku  akiwa  anazungumza  mwenyewe  kabla  ya  kuanza  kusitisha  kuongea. Mama  huyo  alisema  baada  ya   Patrick  kukumbwa  na  maradhi  hayo  wiki  moja  baadaye  dada  yake  naye   alishikwa  na  kuanza   kutikisa  kichwa. “  Moyo wangu  unaogopa, naomba  mtueleze  chanzo  cha  maradhi  haya  ambayo  hospitalini  wananiambia  hawayajui  zaidi  ya  kupewa   dawa  ambazo   hazijasaidia  kitu “  alisema  mama  huyo.  Kwa  mujibu  wa  Wizara  ya  Afya  ya  Uganda, zaidi  ya  watoto  2000, wameathiriwa  na  maradhi  haya  tangu  yalipoibuka  mwishoni  mwa  mwaka  2012.  Wakati  Wizara  ya  Afya  ya  Uganda  ikisema  hivyo, nchini  Tanzania  kwa  mujibu  wa  Kaimu  Mkurugenzi     Msaidizi  Ufuatiliaji  na  Udhibiti  wa  Magonjwa  katika  wizara  ya  Afya , Dk.  Janeth  Mghamba , maradhi  haya  ambayo  yanaonekana  kama mapya  nchini  Tanzania  yaligunduliwa   nchini  tangu  mwaka  1960. Maeneo  yaliyo  athirika  ni  Mahenge mkoani  Morogoro, ambako  pia  kuna  hospitali  inayo  shughulikia  waathirika  wa  tatizo  hilo.

MAKALA  HAYA  YANATOKA  KWENYE  GAZETI  LA  NYAKATI, TOLEO  na. 674,  LA  JUMAPILI, OKTOBA  27-NOVEMBA  2, 2013.

Comments

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ya  kupata  wapenzi  wa  kike  ama  kuoa  na  wengine  huendelea  na  tabia  hiyo  hata  baada  ya  kuoa .  Zipo  sababu  mbalimbali  zinazo  wapelekea  wanaume  kupiga  punyeto, ila  kubwa  kati  ya  hizo  ni  pamoja  na  kutokuwa  na  wapenzi, kutokuwa  na  wapenzi  wanao  kidhi vigezo  vyao, kuwa  katika  mazingira  yasiyokuwa  na  wanawake  ( mfano  katika  shule  za  sekonda

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS

Dawa ya TONSILS ni (kugargar)  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto. Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia. Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako. Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafanya ka

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na  kuwa  mgumu  kama  msumari. Na  hatua  ya  pili   ni  lazima, uume  wake  uendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa  STRONGER  AND  LONGER  ERECTION JINSI  HATUA  ZA  KUSIMAMA  KWA  UUME  ZINAVYO  TOKEA. 1. HATUA    YA  KWANZA: DAMU  KUTIRIRIKA  KWA