Skip to main content



Majani  ya  mti  wa  mwarobaini.
Mti  wa  mwarobaini.
TUMIA  MWAROBAINI  KUJITIBU  MAGONJWA  YA  NGOZI.

Mwarobaini (Azadirachta indica) ni mti unaofahamika kwa uwezo wake wa kutibu magonjwa ya aina mbalimbali. Inaaminika kuwa mti huu umetoka huko India  na Burma . Mwarobaini hushamiri zaidi katika nchi za tropiki  na una uwezo mkubwa wa kuhimili ukame. Nchini  Tanzania, mti  wa  mwarobaini  huweza  kupatikana  kwa  urahisi  kabisa  katika  maeneo  mengi  ya  mijini  na  vijijini.

Jina “mwarobaini” linatokana na imani kuwa mti huu una uwezo wa kutibu magonjwa yapatayo arobaini. Majani na mbegu za mwarobaini vimekuwa vikitumiwa kama tiba kwa miaka maelfu  katika  nchi  mbalimbali  duniani.

Kati ya magonjwa ambayo mti huu umetumika kutibu au kupoza ni pamoja  na  matatizo ya kusaga chakula tumboni, kisukari, kansa, magonjwa ya ngozi, malaria, ukungu (fungus), n.k. Matawi yake hutumiwa kama mswaki na magome yake hutumiwa kama dawa ya kusafisha meno.

Mafuta ya mibegu ya mwarobaini hutumika kutengenezea vipodozi na sabuni. Kiziduo cha mibegu au mafuta yake hutumiwa kama dawa ya kuulia wadudu wanaoharibu mimea shambani.

Tumekwisha   ziona  faida  mbalimbali  za  mti  wa  mwarobaini,  leo  nitakufundisha  namna  ya  kutumia  mti  wa  mwarobaini  kujitibu  magonjwa  ya  ngozi.

 

                        MAHITAJI :

i.             Majani  ya  mti  wa  mwarobaini.

ii.          Sufuria

iii.        Mwiko

iv.         Jiko  la  gesi, mkaa  au  jiko  la  mafuta.

                       HATUA   ZA  KUFUATA:

1.  Chukua   majani  mabichi   ya  mti   wa  mwarobaini  na  uyaweke   kwenye   sufuria.

2.  Chukua  sufuria   yako  yenye  majani  ya  mti  wa  mwarobaini  na  ui injike  kwenye  jiko lenye  moto  wa  wastani.

3.   Chukua  mwiko  wako  na  uanze  kuyakoroga  majani  yako  taratibu  hadi  yakauke   bila  kuungua.

 

Majani  yako  yakiisha  kauka, ipua sufuria  yako, chukua  majani  yako  yaliyo  kauka, yasage  kisha  hifadhi  unga  unga  wako  kwenye  chombo  cha  plastiki.

                              MATUMIZI :

Tumia    vijiko  viwili  vya  chai  kwenye  kikombe  cha  robo  lita  chenye  maji  ya  moto, mara  mbili  kwa  siku  kwa  muda  wa  siku  ishirini  na  moja.


UTAPATA  MATOKEO  MAZURI   SANA. NGOZI  YAKO  ITAKUWA  LAINI, NYORORO  NA  YENYE  AFYA.

Makala  haya  yameandaliwa  na  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC.  Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu   huduma  zetu wasiliana  nasi  kwa  SIMU : 0766538384.

Comments