Wale wapenzi wa mapishi unaweza achana na matumizi ya sukari ya mezani na kutumia ASALI katika shughuli zako za uokaji vitu mbalimbali kama mikate, maandazi, keki n.k
Asali ni nzuri zaidi katika uokaji kwasababu
1. Inaongeza SHELF LIFE(mda wa bidhaa kukaa bila kuharibika) kwasababu asali inazuia mazalia ya bakteria.
2. Inaongeza ulaini
3. Inaongeza AROMA
4. Inaleta FLAVOUR nzuri zaidi
VITU VYA KUZINGATIA
Vifuatavyo ni baadhi ya vitu vya kuzingatia utumiapo asali badala ya sukari
1. Punguza kipimo cha asali kwa 1/3 au nusu kutoka matumizi ya kawaida ya sukari. Mfano kama ulikua unatumia sukari 1 KG basi asali tumia NUSU KILO kwasababu asali ni tamu zaidi.
2. Punguza kiwango cha maji utakachotumia kwa upishi angalau kwa 1/5 kwasababu asali tayari ina maji angalau 18%.
3. Punguza joto la OVEN yako angalau kwa 4 centigrade.
4. Ongeza nusu kijiko cha BAKING soda kwa kila kikombe kimoja cha asali unachoweka
5. Paka mafuta kidogo chombo utakachotumia kupimia asali ili iweze kutiririka vizuri
Makala
haya yameandaliwa na HONEY SPRING, wauzaji wa
asali orijino. Kwa mahitaji
yako ya asali
orijino, wasiliana nao kwa simu 0769129351
au 0683370065 .
Comments
Post a Comment