Skip to main content

AUNT EZEKIEL ; Mafuta Ya Nazi Ni Siri Ya Urembo Wangu.




Aunty  Ezekiel
Msanii  wa filamu, Aunt  Ezekiel  leo  yupo  kwenye  safu  hii akielezea  mawili  matatu  kuhusiana  na  urembo  wake.
Wapo  wanao  tamani  kuwa  kama  yeye  lakini  huenda  hawajui  siri  inayo mfanya  anaonekana  bomba wakati  wote.
Staa  huyu  ana  choyo, leo  anakupa  kwa  kifupi  vipodozi  anavyo  tumia.

MAFUTA  :  Natumia  sana  mafuta  ya  nazi  aina  ya  ‘ Vagina Coconut’. Wengi  hawajui tu, lakini  ni  rafiki  wa  ngozi  ya  binadamu. Haya  nayapaka  kuanzia  usoni  hadi  miguuni  na  ndiyo  yanayo  nifanya  niwe  na  ngozi  nyororo.


Mafuta  Ya  Nazi.

SABUNI  : Wakati  wa  kuoga  huwa  natumia  sabuni  ya  Detto.
Make Up : Maybeline.
Masaji  Ya  Mwili  :  Katika  kuhakikisha  nauweka  mwili  wangu  katika  hali  nzuri mara kwa  mara  naufanyia  masaji  na  huwa  natumia  karafuu  ya  madonge.


Karafuu

Nawashauri   wasichana  kutotumia  mkorogo  kwa  sababu licha  ya  kwamba   utaonekana  mrembo  leo  lakini  baada  ya  muda  madhara  yataonekana  ikiwa ni  pamoja  na  ngozi  kusinyaa  kwa  kuchoshwa  na  vipodozi  vikali.
SOURCE :  Gazeti  La  Ijumaa. Toleo   Na. 865, Februari 7,2014.

Comments