Nimekutana na makala haya mtandaoni, nikaona ni vyema ku share na wasomaji wetu.
Ni mara chache mno kukutana na mwanamke
anayependa mwanaume mchafu, anayenuka jasho mwenye aleji na maji
vijana wanapenda utanashati ili wawe kivutio kwa wengine hasa wanawake, lakini kuna watanashati lakini sio wasafi, kwa nje wamependeza lakini ndani loh...majanga full fungus ukimwambia avue soksi mtagombana.
vijana wanapenda utanashati ili wawe kivutio kwa wengine hasa wanawake, lakini kuna watanashati lakini sio wasafi, kwa nje wamependeza lakini ndani loh...majanga full fungus ukimwambia avue soksi mtagombana.
UWAPO MTANASHATI ZINGATIA PIA HAYA YA USAFI
1:MAPELE USONI, ni tatizo kwa wanaume wengi na wanafikiri ni maradhi kumbe ni uchafu
kidevu kinabeba nongo jasho na mafuta yote yanayotiririka usoni hivyo unyoapo zingatia haya
_usitumie wembe zaidi ya mara mbili
_safisha kidevu chako kwa maji ya moto kabla na baada ya kushave
_kiwembe cha kidevuni usikitumie kunyoa kwingineko
_tumia gillete au bic au brand nyingine yoyote nzuri
_safisha kidevu kila ulalapo
_kama una dalili ya mapele kidevuni, kisugue kidevu kwa mswaki laini kisha paka ndimu
_paka mafuta ya nazi
2:FUNGUS SEHEMU ZA SIRI, hii husababishwa na uchafu, unaoga mwili wote lakini huko chini unakusahau, fanya hivi kutibu tatizo
_usivae chupi mbichi au yenye unyevu
_shave at least twice a week
_usivae chupi zaidi ya mara moja
_oga kila ulalapo
_kina uogapo sugua kende na maeneo yanayozizunguka kwa kitaulo kisha suuza vema
_kausha vizuri paka mafuta ya nazi
_lala uchi au vaa bukta nyepesi kuvipa vifaa nafasi ya kupumua
_usilale bila kujiswafi ufanyapo ngono
3:FUNGUS MIGUUNI NA MIGUU KUNUKA, hali ya TANZANIA ni ya kitropiki hivyo kuna joto mno, viatu tuvaavyo vingi ni semi leather hivyo kuifanya miguu ipumue mno
fanya hivi
_ jitahiti kuwa na pair zaidi ya moja za viatu
_usirudie soksi
_usivae soksi mbichi au nyevu
_kila uogapo jitahidi kusugua kati kati yavidole kwa kitaulo kidogo
_hakikisha unakausha miguu vizuri kabla ya kuvaa soksi
-paka mafuta ya nazi
kwa jinsi hiyo utakuwa umetatua matatizo makubwa matatu na kuokoa pesa nyingi, utaulamba kwa nje lakini pia ndani utakuwa uko njema, hata sweetie akitaka kuzama hutaona noma kupanua miguu, au ukienda kwa mama mkwe hutaona noma kuvua viatu
SOURCE : Jamii Forums
Comments
Post a Comment