Papai |
KAMA UNA KISUKARI CHUKUA TAHADHARI: NI MUHIMU KUJUA KWAMBA
UNAKABILIWA NA HATARI MARA 3 ZAIDI YA KUKUMBWA NA SARATANI KULIKO MTU AMBAYE
HANA KISUKARI.
Tafiti zinaonyesha kwamba kuna wakati saratani ni matokeo ya mchakato wa ukarabati wa seli zilizoharibika ndani ya mwili.
Tafiti zinaonyesha kwamba kuna wakati saratani ni matokeo ya mchakato wa ukarabati wa seli zilizoharibika ndani ya mwili.
Tafiti hizi zinaonyesha kwamba mimba inapotungwa seli katika
mimba hiyo changa hugawanyika haraka sana na kutengeneza makundi mawili ya seli
zenye maumbile na kazi tofauti.
Nanasi |
Kundi la kwanza la seli hizo (Kiini tete, au embryo kwa lugha
ya kitaalamu) huendelea kugawanyika na kubadilika likiwa safari kutengeneza
kiumbe ambacho hatimaye kitazaliwa kama mtoto.
Hali kadhalika kundi la pili nalo hundelea kugawanyika na
kubadilika na hatimaye kutengeneza kondo la uzazi (placenta) ambalo kazi yake ni
kulizingira lile kundi la kwanza.
Kila moja ya seli katika kundi hili la seli ambalo sasa limetengeneza kondo la
uzazi ina gamba ambalo limebeba umeme hasi.
Seli hizi kitaalamu huitwa Trophoblasts. Kazi ya hizi
Trophoblasts ni kutoa ulinzi kwa kiini tete kisiweze kushambuliwa na mfumo wa
kinga za mwili za mama!
Bila seli hizi
chembechembe nyeupe za damu katika mwili wa mama ambazo huunda sehemu kubwa ya
jeshi la kinga katika mwili wa mwanadamu zingeshambulia kiini tete hicho na
kukiharibu kwa dhana kwamba ni adui ailiyeingia mwilini! Kinachotokea ni kwamba
kwa kuwa chembechembe hizi nyeupe za damu nazo zimebeba umeme hasi kama zilivyo
Trophoblasts, zinapokaribia eneo kiliko kiini tete umeme hasi wa Trophoblasts
na ule wa chembechembe cheupe husukumana (repels each other) na hivyo
kusababisha chembechembe hizo nyeupe kusogezwa mbali na kiini tete.
Tafiti zinaonyesha kuwa
ulinzi huu wa Trophoblasts hukoma ghafla katika juma la nane la ujauzito.
Tafiti zinaonyesha kuwa sababu ya hatua hii ni kwamba katika kipindi hiki kiumbe kinachoendelea kukua na kubadilika tayari kina ngongosho linalofanya kazi na kongosho hili huzalisha kiasi kikubwa cha vimeng’anyo (pancreatic enzymes) ambavyo haviruhusu trphoblasts au chembechembe nyeupe za damu kutoka kwa mama kusogea katika eneo hilo.
Vimeng’enya hivi vina uwezo wa kuchakatua na kuyeyusha protini
(digest) hivyo basi chembechembe yoyote nyeupe katika eneo hilo, au seli ya
trophoblast itaharibiwa kwa protini yake kuchakatuliwa na kuyeyushwa na
vimeng’enya hivyo.
Tafiti zinaonyesha kuwa mwili unapositisha uzalishaji wa trophoblasts, chache ya hizi seli hubakia zikiogelea kwenye damu katika kipindi chote cha maisha ya kiumbe. Kazi ya hizi trphoblasts ni kusaidia katika ukarabati wa seli za mwili zinazoharibika kwa sababu mbalimbali.
Katika eneo ambalo seli
zimeharibika na zinahitaji kukarabatiwa seli chache za trophoblasts huenda
katika eneo hilo na kuanza kugawanyika kwa kasi inayozifanya kuongezeka kwa
wingi ndani ya muda mfupi, huku zikifanya kazi ya kusadia ukarabati.
Tatizo linakuja pale ambapo uharibifu wa seli husika ni
kitendo endelevu na pengine cha kudumu. Kwa mfano, kwa wavutaji wa sigara wa
muda mrefu ambapo uharibifu wa seli za mapafu yao ni endelevu.
Hii ina maana kwamba
katika eneo husika trophoblasts zitakuwa zinajigawanya kwa kasi na zitaongezeka
kupindukia mipaka (out of control growth).
Uchunguzi wa kimaabara unaonyesha kuwa seli za trophoblasts zinazojikuta katika mazingira ya aina hii hufanana kwa kila hali na seli za saratani!
Hii imepelekea baadhi ya wanasayansi kuamini kuwa saratani
chanzo chake ni nia nzuri na jitihada ya mwili kutaka kurekebisho kasoro
zinazojitokeza katika seli za mwili.
Jitihada zinapokwenda mrama kutokana na uharibifu katika seli
husika kuwa endelevu basi saratani hujitokeza.
Imethibitika kuwa vimeng’enyo vinavyozalishwa na kongosho (pancreatic enzymes) ni msaada mkubwa wa kuzuia trophoblasts kutengeneza saratani mwilini.
Imethibitika kuwa vimeng’enyo vinavyozalishwa na kongosho (pancreatic enzymes) ni msaada mkubwa wa kuzuia trophoblasts kutengeneza saratani mwilini.
Ugunduzi huu ulifuatia jitihada kubwa za Dr. William D. Kelly wa kule nchini Marekani ambaye aliamini kuwa saratani ni zao la mwili kushindwa kuchakatua vizuri vyakula vya jamii ya protini kutokana na upungufu wa vimeng’enya vinavyozalishwa na kongosho, hususan vile ambavyo kazi yake ni kuchakatua na kuyeyusha protini (proteolitic enzymes).
Ili kuusadia mwili kufanya kazi hiyo kwa ufanisi Dr. Kelly alipendekeza mfumo wa tiba kwa wagonjwa wake ambao ulijumuisha marekebisho katika lishe, matumizi ya tiba-lishe (nutritional suppliments), na uondoshaji wa sumu mwilini. Dr. Kelly ambaye alipingwa sana na madaktari wa mfumo (conventional cancer doctors) alisafishwa na Dr. Nicholas Gonzales wa Newyork ambaye alifanya kazi kubwa ya kutafiti kesi moja moja ya wagonjwa wa Dr. Kelly kwa udhamini wa taasisi ya Memorial Sloan - Kettering Cancer Center. Ripoti ya kazi ya Dr. Gonzales, iliyokuwa na kurasa 500, ilithibitisha kuwa tiba ya Dr. Kelly ilikuwa kweli inafanya kazi katika saratani za aina nyingi mwilini.
Utafiti wa ziada uliofanywa katika kazi ya Dr. Kelly na wengine waliomfuata umethibitisha bila shaka kuwa uchache wa vimeng’enya vya kongosho ni sababu ya msingi ya kuibuka kwa saratani mwilini; na kuwa wagonjwa wa ugonjwa wa kisukari ambao kimsingi kongosho zao zinazalisha kiwango kidogo cha hivi vimeng’enya, wako katika hatari mara tatu zaidi ya kupata ugonjwa wa saratani.
Hii ina maana kuwa mgonjwa wa kisukari anatakiwa achukue tahadhari mara tatu zaidi kuliko mtu wa kawaida katika kulinda seli zake za mwili zisiharibike na kujenga mazingira ya trophoblasts kuzaliana kwa wingi. Uharibifu huu ni ule unaoweza kufanywa na uvutaji wa sigara, ulaji wa vyakula vilivyotunzwa kwa kemikali, matumizi ya vipodozi bandia (synthetic cosmetics), matumizi ya nyama zilizochakatuliwa na kuhifadhiwa kwa kemikali, matumizi ya nyama za kuchoma zilizoungulia na kufanya mkaa, nakadhalika.
Aidha mgonjwa wa sukari anahitaji kutumia nyongeza/tiba- lishe
(nutritional supplements) za vimeng’enya, hususan vile ambavyo kazi yake kubwa
ni kuchakatua na kuyeyusha protini.
Vimeng'enywa vilivyotengenezwa viwandani wakati mwingine ni ghali kuliko uwezo wa walio wengi. Kama hali ni hii basi ni vema kula vyakula vinavyoweza kukupatia vimeng'enya hivi.
Tunda kama papai ni chanzo kizuri sana ya kimeng'enya
kinachoitwa papain. Kigogo kilichoko katikati ya tunda la nanasi ni chanzo
kizuri sana cha kimeng'enya kinachoitwa bromelain.
Kongosho bichi
lililotoka kwenye mnyama mchanga ni chanzo kikubwa mno kwa vimeng'enya vya aina
tofauti tofauti vya protini.
CREDIT
: HERBAL IMPACT
Comments
Post a Comment