Habari yako msomaji,
Natumaini uko vema, unaendelea na kusaka mahela hapa duniani lakini usimsahau MUNGU katika kusaka na kutumia mahela.
Leo tuyakumbuke haya mafuta mazuri mno, ya nyonyo. Wengi tunaoyafahamu haya mafuta tunayajua kwa kazi yake kwenye kutatua tatizo la kutopata choo; yanafanya kazi vizuri tu nyanja hiyo.
Mafuta ya Nyonyo katika Kukuza Nywele
Mafuta ya nyonyo yanakuza nywele haraka, ukiyapasha joto kidogo kabla ya kupaka, kisha unapaka kwenye ngozi ya kichwa na kuyatawanya vizuri katika ngozi taratibu kama una massage kichwa chako pia bila kupasha kule kumassage kunayongezea joto linayoyapa uwezo wa kupenya vizuri. Unapopaka na kutawanya vizuri unasaidia kuongeza mzunguko wa damu kichwani hivyo virutubisho vinavyoletwa na damu kukuza nywele zako vinafika kwa utoshelevu. Mafuta haya yana virutubisho mbali mbali ikiwemo Omega 6 fatty acids ambazo huongeza virutubisho vinavyoleta afya katika nywele zako.
Iwapo unataka utumie kama conditioner basi ukimaliza kupaka kwenye ngozi paka katika ncha zako pia kisha vaa kikofia cha plastiki kisha baadae uzioshe nywele zako vizuri kuondoa mafuta kwa kuwa ulipaka mengi kama conditioner.
Mafuta ya nyonyo ni mazito sana, iwapo utaona una nywele nyepesi na hutaki ziligee kwa uzito wa mafuta pale unapopaka basi changanya na mafuta mengine hasa mafuta ya nazi kwa uwiano wa 1:1.
Mafuta ya nyonyo yanatibu mba na matatizo mengine ya ngozi ya kichwa.
Mafuta haya huwa na sifa ya kuwa na uwezo wa kuua bacteria na fangasi ambao huweza kuleta matatizo yanayosababishwa na vimelea hivi ikiwemo mba.
Iwapo una nywele kavu na una mba basi changanya mafuta ya nyonyo na ya mzaituni kidogo kisha paka kichwani pako kwa mfululizo mpaka shida yako ipungue au iishe.
Iwapo una mba na nywele zina mafuta mengi basi changanya hivi: kijiko kimoja kimoja cha mafuta ya nyonyo, asali na ute ute wa aloevera na maji ya nusu limao. Paka kwenye mizizi ya nywele yani kwenye ngozi kaa nayo dakika 30 kisha osha mchanganiko utoke kwenye nywele yako.
Pamoja na kutibu mba michanganyiko hii hurutubisha nywele na kufanya zing'ae.
Yanajaza nywele Zako
Mafuta ya nyonyo yana omega 6 na omega 9 acids ambazo ni virutubisho vinavyosaidia katika afya ya nywele yako. Ukitumia mara kwa mara mafuta ya nyonyo yanasaidia kuotesha nywele na kuzipa nguvu(kuzinenepesha) nywele zako ambazo tayari ni ndefu.Unaweza kutumia kama conditioner
Unapaka na kuvaa plastiki kisha unaosha, unaweza kulala nayo kichwani mpaka asubuhi. Pia unaweza kuchanganya na conditioner au steaming yako unayotumia.Yanarudisha mng'ao wa nywele zako
Iwapo utayachanganyana mafuta mengine au utayatumia yenyewe yana virutubisho vinavyoiacha nywele yako iking'aa.Iwapo unasumbuliwa na ncha za nywele zako hii ni dawa
paka mafuta ya nyonyo kabla ya kuosha nywele zako na shampoo, shampoo inamaliza baadhi ya mafuta ya asili kwenye nywele na kukupa ncha kavu zinazosababisha kuchomoka nywele zako unapochana.Yanasadia kutibu chunusi
Haya mafuta yana kiungo chenye uwezo wa kuua bacteria wanaosababisha chunusi.Pishana na uzee kwa mafuta ya nyonyo
Yanasaidia kuondoa vikunyanzi vidogo vidogo usoni vinavyotokea kwenye ngozi ya watu wenye umri mkubwa. Imeonekana mafuta haya ya kirutubisho kinachosadia kubalance collagen katika ngozi yako, collagen ndio kirutubisho kinachotunza ngozi ya ujana.Kuza kope na nyusi kwa mafuta ya nyonyo
Inasemekana yamekuwa na mafanikio pia katika kukuza/kujaza kope na nyusi.kupaka machoni |
Upatikanaji wake
Mafuta ya nyonyo yapo yanayochujwa kwa njia ya kawaida kama ya nazi, mbegu za nyonyo hupondwa na kupikwa. Kuna haya maarufu kama 'Jamaican Castor Oil' haya huandaliwa kwa kukaanga kwanza zile mbegu kisha yanachujwa hivyo hutoka meusi. ni vema upate yaliyoandaliwa kiasili yasiwe super refined au yameongezewa kemikali.mmea wake( mti wa nyonyo) |
mbegu za nyonyo(castor beans/seeds)
|
Jamaican Version |
Tahadhali
Mafuta ya nyonyo yana harufu kali hivyo unaweza kuchanganya na kitu kingine kama mdalasini au mafuta mengine kupunguza harufu.Jaribu uone haya mafuta yanavyofanya kazi.
CREDIT : www.centilicious.blogspot.com
yanapatikana wapi na kwa bei gani...??
ReplyDeleteyanapatikana wapi na kwa bei gani...??
ReplyDeleteNaweza Pata Email zenu au namba zenu??
ReplyDelete