Habari za leo, ninaitwa Beka, naishi Ukonga, Dar Es Salaam, ninasumbuliwa na tatizo la mwili kuwaka moto. Ninaomba kujua nifanye nini ili niondokane na tatizo hili.
===================================================
Ndugu Beka, zipo tiba mbalimbali za asili, zinazo weza kusaidia kutibu tatizo la mwili kuwaka moto. Kati ya tiba hizo, ifuatayo ni miongoni mwa tiba asilia za tatizo la mwili kuwaka moto ambazo zimeonekana kuwa na mafanikio makubwa zaidi.
MAHITAJI :
i. Mafuta ya nyonyo (Castor Oil )
ii. Mafuta ya mzeituni.
MATAYARISHO :
Changanya mafuta ya nyonyo robo lita na mafuta ya mzeituni robo lita, kisha koroga hadi mchanganyiko wako uchanganyikane, halafu hifadhi kwenye chupa ama kopo safi.
MATUMIZI : Tumia kujichua mara tatu kwa siku, asubuhi mchana na jioni. Utaendelea kujichua hadi tatizo litakapo isha. Kama tatizo lako litaendelea kuwepo bila kupata nafuu yoyote, unashauriwa kufika katika kituo cha afya kwa ajili ya vipimo zaidi.
IMEANDALIWA NA NEEMA HERBALIST BLOG......0766 53 83 84.
Comments
Post a Comment