Kuwa na uso wenye ngozi laini ni ndoto ya kila mwanamke duniani. Unaweza kuifanya ngozi ya uso wako kuwa laini, bila kulazimika kutumia dawa zenye kemikali.
Mdalasini ya unga |
Mafuta ya Mzeituni |
Mafuta ya Habbat Sodah. |
Kama unataka kulainisha ngozi ya uso wako kwa njia asilia, njia zisizo na madhara yoyote kwenye afya yako, fuata maelekezo yafuatayo :
1. MAHITAJI :
i. Unga wa mdalasini gramu 250.
ii. Mafuta ya Habbat Sodah milimita 250.
iii. Mafuta ya mzeituni milimita 250.
2. MATAYARISHO :
Changaya unga wa mdalasini, mafuta ya Habbat Sodah, na mafuta ya mzeituni kisha koroga kwa pamoja hadi zichangamane, halafu hifadhi kwenye chombo kisafi.
3. MATUMIZI : Tumia kujipaka mara mbili kwa siku asubuhi na jioni kwa muda wa siku thelathini, na ngozi yako itakuwa nyororo na yenye kuvutia sana.
IMEANDALIWA NA NEEMA HERBALIST BLOG ....0766538384, DAR ES SALAAM.
Comments
Post a Comment