Utangulizi
•
Rosella ni mmea wenye virutubisho vingi km vitamini, na madini ya chumvichumvi
•
Hutumika kutengenezea juisi, jam, jellies, sauces, na mvinyo (pombe)
•
Hutumika kuukinga mwili na magonjwa km saratani, ini na ukosefu wa lishe
•
Unapunguza rehamu, unatibu presha
•
Mmea wa Rosella wenye maua mekundu hujulikana kama choya-Dodoma
•
Huitwa mkakaka(pwani) na wengine huutumia kama kiungo cha mboga(ndimu)
•
Majani yake yanaweza kuliwa kama mboga vilevile
•
Ni zao la biashara na hutumiwa nyumbani Mrosela
•
Mmea huu hukua na hufikia urefu wa mita 3.5 kwa msimu
•
Mti pamoja na matawi yake vimenyooka • Majani yamepishana kimpangilio na
kugawanyika katika sehemu 3 – 7 pembeni yakiwa kama msumeno
•
Una rangi ya kijani, nyeusi hadi nyekundu
•
Maua ni makubwa yenye rangi nyekundu hadi njano
•
Una mzizi mrefu na hutoa maua wakati wa kiangazi.
•
Pia unavumilia ardhi yenye tindikali ya juu na ya chini pamoja na magonjwa
Aina Za
Rozela
•
Kuna aina 2 za Rozela
i.
: – Hibiscus sabdariffa yenye vikonyo
vya rangi nyekundu hadi njano ambavyo vinaliwa
ii.
Hibiscus altissima Webster ambayo
hupandwa zaidi kwa ajili ya kamba kamba (fibres) zake lakini vikonyo haviliwi
Mahitaji ya Mrosela
• Hali ya Hewa:
i.
Maeneo ya tropiki yenye mvua kati ya
1500 – 2000 mm kwa mwaka
ii.
Mwinuko wa hadi meta 600 kutoka usawa wa
bahari
iii.
Inavumilia joto na hali ya unyevunyevu
iv.
Hupendelea udongo wa mchanga wenye
rutuba ambao hupenyeka kwa urahisi
v.
Hata hivyo unaweza kukua kwenye aina
mbalimbali za udongo
vi.
Huhitaji palizi ya mara kwa mara ili
kuondoa kivuli na majani
vii.
Huvumilia mafuriko, upepo mkali na maji
yaliyotuama
·
Ulimaji wa
Rozela
Uchaguzi wa eneo, utayarishaji wa
eneo, uchaguzi wa mbegu
•
Mahitaji ya bustani : vikapu, mbolea, udongo, mchanga
•
Tifua ardhi vizuri kwenda chini kama sentimeta 20
•
Piga mashimo ya ukubwa wa sm15 X sm 15 na kina cha sm 5
•
Panda mbegu kilo 11 – 22 kwa hekta
•
Ni vyema kupanda mbegu kwa mistari
•
Palizi katika mwezi wa kwanza ni muhimu sana
•
Mbolea za asili zinafaa kutumika na husaidia sana
•
Mtindo wa kubadilisha mazao (crop rotation) hutumika hasa kwa ajili ya mdudu
anayeshambulia mmea huu kwenye mizizi (root knot nematode) Heleredera
radicicola
•
Unaweza kubadilisha na mazao ya kijani kama kunde, mahindi
•
Mashamba madogo nyumbani: – Panda mistari halafu ikisha ota punguza iwe katika
mistari ya meta 1 x meta 1.
•
Mashamba makubwa: – Mbegu zioteshwe kwenye kitalu halafu zipandwe shambani kwa
upana wa meta1.3 hadi 2.6 na mistari ya upana wa meta 2-3.3 Magonjwa • Fungi:
fangas (ukungu) mbalimbali hushambulia kwenye mizizi na majani – Nyunyiza dawa,
fungicides Kumbuka: Uangalizi wa shamba unahusisha; – Palizi, Kukata mapukutu,
kufyeka – Kunyweshea – Uwekaji mbolea – Uwekaji dawa kwa wadudu waharibifu
Uvunaji wa
Rozela
•
Uvunaji wa matunda na vikonyo hufanyika majuma 3 baada ya maua kuchipua.
•
Inashauriwa vikonyo viondolewe baada ya kupika matunda
•
Kwa Rosela ya kamba: kupanda hadi kuvuna ni miezi 3-4 na ivunwe wakati mimea
inatoa maua –
Mimea
ikatwe chini kabisa na kisha kuning’iniza ili kamba ziachane na mti – Kamba
zioshwe na kuanikwa juani – Mashine zipo na zinaweza kutumika kwa ajili ya
kutenganisha kamba na mti • Ukaushaji Unafanywa kwa kutumia – solar dryer –
chekecheke – Kuanika moja kwa moja juani – Kutumia majamvi kwa kukaushia
matunda yenye mbegu
Maandalizi:
•
Andaa turubai, jamvi, mkeka nk
•
Bandua vikonyo
•
Hifadhi matunda yenye mbegu Kuhifadhi
•
Weka rosela iliyokauka kweye mifuko safi ya nailoni au viroba
•
Hifadhi mifuko kwenye chumba kisafi chenye mzunguko mzuri wa hewa na kisiwe
chenye unyevunyevu
·
Uvunaji
wa kiuchumi
•
Uvunaji wa vikonyo kilo 1.5-7.5 kwa mmea
•
Kilo 17000-19000 kwa hekta
•
Uzalishaji wa kamba ni kg 1700 – 3500 kwa hekta
•
Kiasi cha kamba kwenye rosela ni 5%
Matumizi
ya Rosela – Majani, matunda, maua, vikonyo, mbegu,
mizizi
i.
Vikonyo vya matunda hutumika
kutengenezea jams, jellies, sauces na mvinyo
ii.
Vikonyo pia hutumika kuweka rangi na
ladha kwenye vyakula
iii.
Majani machanga huliwa kama mboga
iv.
Mbegu hutumika kwa ajili ya kuongeza
nguvu za kiume
v.
Matunda yake yanaliwa
vi.
Kamba zake hutengenezea vitu mbali mbali
vii.
Rosela pia hutoa mafuta
viii.
Inatumika kutengeneza
mvinyo mzuri sana.
Matumizi Ya
Rozela kama dawa asilia
i.
Huongeza nguvu za kiume
ii.
Hutibu magonjwa ya tumbo, majipu,
matatizo ya moyo, kikohozi, kansa (vikonyo), homa homa, na magonjwa ya akili
iii.
Hupunguza kiwango cha kulewa kwa mtu
anapokunywa pombe
iv.
Maua yake ni mazuri sana katika
kupunguza lehemu ( Kolestrol ) kwenye damu.
·
Hitimisho
Comments
Post a Comment