Carlina White |
Tarehe
18 Agosti 1987 ilikuwa
ni siku mbaya
kabisa kuwahi kutokea
katika familia ya Bi
Joy White na
Carl Tyson.
Carlina White na mama yake mzazi. |
Mtoto wao
kipenzi aliyekuwa na
siku kumi na tisa
tu tangu aanze
kuvuta pumzi alitekwa
katika hospitali ya Harlem Hospital Center, New
York City, Marekani.
Wazazi wa Carlina mwaka 1987 |
Hata hivyo, miaka
ishirini na moja
baadaye mtoto huyo
alikuwa na re united
na wazazi wake
katika namna iliyo
staajabisha kabisa.
Ilikuwaje ?
Fuatana name katika
simulizi hii ya
kusisimua.
Tarehe 15
Julai 1987 ilikuwa
siku ya furaha sana
kwa wanandoa Joy White
na mume wake Carl
Tyson kwa sababu ilikuwa
ni siku waliyo
barikiwa kupata mtoto
wao wa kwanza. ( Ndoa ilikuwa
imejibu )
Kwa
furaha aliyokuwa nayo, baba
wa mtoto alimpa
mtoto wake jina
linalo fanana na
lake. Baba aliitwa Carl, so mtoto
akamuita Carlina. Kama angekuwa
anaitwa Joseph basi
bila shaka angemuita
Josephina.
Mtoto alizaliwa
salama na baada ya masaa
24 tangu ajifungue
mzazi aliruhusiwa kurudi nyumbani. Lakini siku moja tangu
waruhusiwe kurudi nyumbani, mtoto alianza
kulia kwa nguvu
bila kukoma jambo lililo wafanya wazazi wake
wamrejeshe hospitalini hapo
haraka sana, ambapo alifanyiwa
vipimo.
Ilionekana
kuwa mtoto Carlina
alimeza maji maji
wakati wa kujifungua
na kupata maambukizi. So mama
pamoja na mtoto
wake wakalazwa kwa
matibabu ya mtoto.
Siku mbili
baadaye mwanamke mmoja
kwa jina Annugetta
“ Ann” Pettway alianza kuzoeana
na mama Carlina. Ann
alijifanya ni nurse
lakini haja ajiriwa katika
hospitali hiyo, ila yupo hapo
kwa shughuli ambazo
mama Carlina hakuzielewa.
Ann aliendelea
kuonekana katika hospitali
hiyo kwa wiki tatu
mfululizo na katika kipindi
hicho cha wiki
tatu alifanikiwa kumshawishi mama
Carlina kiasi cha kumfanya
amuamini.
Siku moja
mama Carlina alipata
udhuru na kumuomba
Ann amsaidie kumuangalia mtoto
wake ( Carlina ). Hilo
lilikuwa ni kosa
kubwa sana katika maisha
yake.
Alfajiri ya
siku hiyo majira
ya saa nane, wakati
wa kubadilishana shift
kwa wafanyakazi, Ann alifanikiwa
kutoroka na mtoto
Carlina.
Kulikuwa na
Video Surveilance lakini
wakati Ann anatoroka
na Carlina zilikuwa
hazifanyi kazi. Hakukuwa na picha
yoyote ya Ann
wala hakukuwa na
namna yoyote wangeweza
kujua sura ya Ann
isipokuwa kwa maelezo
waliyo pewa na
Joy White na
Carl Tyson, ambao ni wazazi
wa Carlina.
Ilipofika saa
mbili za asubuhi, uongozi wa Harlem
Hospital Center aligundua
kukosekana kwa mtoto
Carlina.
Muda mchache
baadaye, habari ziliwafikia wazazi
wa Carlina, ambao walipanic
na kwenda hospitalini
hapo only to prove
that their lovely baby
was missing.
NYPD walitangaza
kupotea kwa mtoto, na
kuahidi zawadi ya
dola elfu kumi
kwa mtu atakaye
fanikisha kupatikana kwa
mtoto Carlina.
Picha ya
mtoto Carlina pamoja
na picha ya kubuni na
Ann zilisambazwa nchi
nzima lakini hata
hivyo hazikuzaa matunda.
Mwaka 1989
wazazi wa Carlina walifungua
kesi ya madai
ya ya fidia
ya Dola Milioni
Mia Moja dhidi
ya Harlem Hospital Centre na
mwaka 1992 mahakama
iliamua walipwe DOLA
LAKI SABA NA
NUSU ambazo walilipwa mwaka
huo huo.
BAADA
YA
KUMTEKA CARLINA.
Baada ya kumteka Carlina , Ann
alipanda treni na
kuelekea kwenye jiji
la Bridgeport, Connecticut,
kilo mita chache
kutoka New York.
BAADA YA KUFIKA
CONECTICUT.
Baada ya
kufika Connecticut, Ann alimlea Carlina kama
mtoto wake wa
kumzaa. Kabla ya
yote alimbadilisha jina
na kumuita Nejdra
“ Netty” Nance.
Mwaka 1993, ikiwa
ni miaka nane tangu
amteke mtoto Carlina, Ann alihamia Atlanta
na kuendelea na
maisha yake kama
kawaida.
CARLINA AANZA
KUMTILIA SHAKA ANN.
Akiwa na
umri wa miaka
23, Carlina alianza kumtilia
shaka Ann kama
ni mama yake
mzazi kweli. Sababu
zilizo mfanya awe
na mashaka ni
kwanza; kutokuwa na ufanano
wowote kati yake
na mama yake, lakini
pili ni kutokuwepo
na nyaraka muhimu
zinazo thibitisha kama Ann
ni mama yake
kweli, kama vile
cheti cha kuzaliwa
na Social Security
Card.
Siku
moja, Carlina alikuwa na
issue ambayo ilimhitaji
apelike cheti chake
cha kuzaliwa ambapo
alimfuta Ann na
kumtaka ampe cheti
hicho, Ann alitoa cheti
cha kughushi na
Carlina alipokipeleka kilichunguzwa
kwenye data base
na kuonekana kuwa
hakuna mtoto aliyezaliwa
mwaka 1987 mwenye jina
lake ( Nejdra Nance ), si
Atlanta wala si
Connecticut.
Carlina alirejea
kwa mama yake
wa kughushi ( Ann ) akiwa ame
fyumu na
kumtaka amuonyeshe cheti
chake cha kuzaliwa.
Ann akaamua
kumwambia ukweli kuwa, yeye
( Ann ) si mama yake
mzazi, akamdanganya kuwa mama
mzazi wa Carlina alikuwa muathirika
wa dawa za
kulevya,na alimuachia yeye (
Carlina ) amtunze bila kumpa documents
zake muhimu kama
cheti cha kuzaliwa nakadhalika.
UAMUZI
WA CARLINA :
Carlina alianza
kufanya upelelezi wake
binafsi, ambapo kwa msaada
mkubwa sana wa
kituo cha National Center for
Missing and Exploited
Children alifanikiwa
kuunganishwa na wazazi wake.
Ann Pettway
alikamatwa, kushitakiwa na kufungwa
miaka kumi na
mbili, kifungo anacho kitumikia
tangu mwaka 2010.
KITU GANI
KILIMFANYA ANN ACHUKUE
UAMUZI WA KUMTEKA
MTOTO MCHANGA NA
KUMLEA KAMA MTOTO
WAKE.
Tatizo lililo
mfanya Ann amteke
mtoto mchanga ni
kuchoropoka kwa mimba ( miscarriage )
Ilifahamika kuwa, Ann
kabla hajafikia uamuzi
wa kumteka Carlina
alibeba mimba nne
na zote zilikuwa zikichoropoka.
Mwezi huo
huo wa saba
1987 Ann alijifungua (mimba yake
ya nne )
lakini mtoto alikufa
wakati wa kujifungua.
Ann alikata
tama ya kuzaa
mtoto na kutaka
kurudi nyumbani kwao
na hadhithi ile
ile iliyozoeleka, kwamba
ujauzito umeharibika, alicho kifanya
ni kwenda kwenye
hospitali ya mji
mwingine, kuiba mtoto na
kurejea nae nyumbani
kwao akijifanya kuwa
ni mtoto wake
wa kumzaa.
Ndugu zake
hawakuwa na mashaka
yoyote na mtoto
huyo kwa sababu Ann aliondoka
nyumbani kwao na
ujauzito wa miezi
tisa akiwa
anaelekea hospitali kujifungua.
TUKIO HILI
LA KUSISIMUA LIMETENGENEZEWA FILAMU
INAYO ITWA : ABDUCTED : THE
CARLINA WHITE STORY.
Unaweza kuitafuta
kwenye maduka mbalimbali
ya filamu au
kwenye internet
Mahojiano
kati ya
Carlina White na
vyombo vya habari baada
ya kuwa reunited
na wazazi wake , unaweza kuya
cheki hapa:
KAMA NA WEWE
UNAYE SOMA HABARI
HII, UNA TATIZO LA
KUCHOROPOKA KWA MIMBA, TEMBELEA http://neemaherbalist.blogspot.com/2013/12/dawa-asilia-ya-kuzuia-kuchoropoka-kwa.html
Comments
Post a Comment