Skip to main content

RACHEL WA THT : SIJAWAHI KUTEMBEA NA MWANAUME MWEUSI NA WALA SINA MPANGO WA KUTOKA KIMAPENZI NA MWANAUME MWEUSI.







Akifanya  interview  na   Sporah  Show, Msanii  wa  muziki  wa  Bongo  Flava, Rachel  amefunguka  kuwa  hajwahi  kutoka  kimapenzi na  mwanaume mweusi  na wala hana mpango  wa  kutoka  kimapenzi na  mwanaume mweusi.


Rachel  alisema  tangu  aanze  kujihusisha  na  mahusiano  ya  kimapenzi,amekuwa  akitoka  na wanaume wa kiarabu,kihindi,nakiburushi.


Aliongeza  kuwa  mpenzi  wake wa mwisho  ambaye  alikuwa  muhindi, alitaka  kumchumbia,lakini  Rachel  hakukubaliana  naye  kwa  sababu ya  tofauti  za  kidini  na  kiutamaduni.
Alipoulizwa  kama  amewahi  kuwa  na  mpenzi  ‘mswahili’ , Rachel  alikataa  kata  kata,na alipoulizwa   kama  anaweza kutoka  kimapenzi  na  mwanaume  mswahili,alisema  hawezi  kufanya  hivyo.

Sporah :  Hao  wanaume  wa kiarabu  na kihindi  huwa  unawafuata  mwenyewe  au  wana  kufuata  wenyewe.

Rachel  :Huwa  wananifuata  wenyewe.
Sporah :  Unadhani  kwa nini  wanakufuata  ?
Rachel  : Sijui,labda  kwa  sababu  ya  aina  ya  muziki  ninao  ufanya  ndio  unawavutia.

Sporah  :Kwa nini  huwapendi  wanaume  weusi,wamekuumiza  sana  kiasi  cha  kuwachukia  ama ?
Rachel : Sijui, labda  kwa  sababu  nimekuwa  na  ukaribu  zaidi  na hao wanaume wa kiarabu,kihindi  na  kiburushi.




Comments