Ipo idadi kubwa ya watu duniani ambao wana sumbuliwa na tatizo la kutokwa na harufu mbaya ya kinywa. Miongoni mwao wapo ambao tatizo hilo limekuwa sugu kwa maana ya kwamba licha kuzingatia kanuni zote za usafi wa kinywa pamoja na kutumia dawa za aina mbalimbali ili waweze kujitibu tatizo lao lakini tatizo linabaki kuwa pale pale. Hakuna tatizo linalo fedhehesha kama tatizo la kutokwa na harufu mbaya ya kinywa. Jambo hili humkosesha mtu raha na amani na humfanya akose confidence ya kuingia katika mahusiano ya kimapenzi. Kuna watu tatizo hili ni kubwa kiasi kwamba hata akiwa amekaa na mtu lets say kwenye meza wanazungumza basi ile harufu mbaya kutoka kinywani kwake huweza kusikika. Je tatizo hili husababishwa na kitu gani haswa? 1.Harufu mbaya ya kinywa husababishwa na aina ya bacteria anayeishi kwenye tishu...