Awali ya
yote kabla ya habari ya Msechu, ukitaka kufahamu
zaidi namna kitambi kinavyo tokea
kwenye mwili wa
mtu, tembelea link hii hapa
chini:
https://neemaherbalist.blogspot.com/2015/11/fahamu-jinsi-kitambi-kinavyo-patikana.html
Haya sasa
endelea na habari
ya Peter Msechu, namna
anavyo teswa na tatizo la kitambi.
Peter Msechu amefanyiwa matibabu ya kuweka puto tumboni ili kupunguza
uzito na unene inayoendelea kutolewa katika hospitali ya Mloganzila.
Peter Msechu amefunguka machache kuhusiana na
changamoto ya kuwa na uzito wa kupitia kiasi kama ifuatavyo
"Watu wananisema sana mtandaoni kuwa Mimi ni mnene na siwajibu. Mimi
niliamua kuishi maisha yangu. Lakini nimekuwa kila siku nikitafuta tiba mbadala
ya kuondoa unene. Natamani Sana kupungua. Sijawahi kujua kushiba kukoje.
Nimekuja hapa Mloganzila ili nifanyiwe hili zoezi la kuwekewa puto tumboni ili
nipungue na nitafanyiwa leo na watu wataona" amesema Peter Msechu.
"Nafanya kazi sana na Serikali na ninaposafiri huwa naendesha gari mwenyewe
kuna wakati mwingine nakuwa kwenye mazingira magumu, nisafiri nifanye kazi,
niimbe halafu nisafiri tena nirudi Dar. Kwa sababu huwa sipendi kulala hotelini
nahisi sio pasafi napenda kulala nyumbani kwangu kwahiyo nikisafiri lazima
nirudi Dar.
"Juzi nilisafiri kwenda Mbeya nilipomaliza kazi nilirudi Dar. Hii nayo ni
changamoto ya unene, unakuwa mtu wa kuchagua sana. Na wakati mwingine nahofia
kuvunja vitanda vya a hotel kwa sababu nilishavunja Sana, hasa hizi chaga.
Inanibidi niombe radhi pale reception"
"Watu wanene wapo na wanajigundua Wana changamoto ambazo wanapitia na zipo
nyingi. Ukiwa na uzito mkubwa kuna baadhi ya vitu unashindwa kufanya mwenyewe.
Nimeshaingia hasara ninaweza kuwa pale nyumbani nafanya kazi zangu kwenye
kompyuta nikaona kwenye bustani yangu nataka nikakate majani niko radhi nitoe
Elfu 20 nimwite kijana akate majani kitu ambacho ningekata mwenyewe kwa dakika
Tatu. Ukipiga hesabu hizo na vitu ambavyo nimepoteza tayari nimeshaingia
hasara" amefunguka Peter Msechu.
Credit kuhusu habari ya Peter Msechu : Mitandao mbalimbali
ya kijamii.
Comments
Post a Comment